Uko sahihi kabisa naheshimu theory na waliozidevelop sio wajinga, wafanyabiashara wanaomake almost wanacheza na hizo theory, basi tuje uraiani unalotaka wewe, ngoja nijikite sehemu nilipo mara nyingi yaani kahama na mbogwe, mfano choma zone hapa kahama office yake kaibrand kuwa ni v.i.p and luxury hapo theory ya regressive of demand and supply imetiki, pale jamaa nyama choma nusu anauza elf9 na siku za weekend huwa anamaliza ngo'mbe mzima pamoja na bei kuwa juu. Jiulize kwanini haendi kuhangaika na Kuwatisha wachoma nyama wa pale stendi CDT wakati nusu wanauza elf5 na wakati mwingine ukihataji hata Kwa elf2 na ugali wanakubalansia? Twende mbogwe pale kitimoto sehemu nyingi nusu ni elf4 Ila kuna sehemu moja ni VIP kimtindo nimepasahau nusu ni elf6 na wala hafikirii kwenda Kuwatisha hao wanaouza elf4. Hapa kahama sehemu nyingi na hasa stend ndogo nusu ya kitimoto ni elf5 Ila twiga si mbali na stendi wanauza nusu elf7 na hawajawahi kutishia mtu kisa anauza bei ya chini. Nisikukatalie Sana hii kutishiana Kwa sehemu za vijijini huwa inatokea na tena si bei tu hata kuanzisha biashara inayofanana na taikoni wa kijiji Kwa kweli utapata tabu kiroho na kilaivulaivu kabisa.