Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Niliwahi kimsikia Mzee wa upako kuwa nguruwe hachinjwi
 
Toa Tangazo, Ripoti Polisi,

Pandisha Bei Kutoka 8000-11000 au Uza 12000 Toa Nyongeza Kilo Moja Kwa Mteja Anayenunua Kuanzia kilo 5
Tafuta Njia Nzuri Ya Kubakiza Wateja Kwa Mfano Toa Zawadi ya limao,Vifungashio Na Fanya derivery kwa wateja wakubwa.
Na hapo haya mapuuzi yatamfuata tu! Akilegeza msimamo tu imekula kwake! Yatampangia masharti tena hakuna kutoa limau, wala vifungashio!
 
Mimi nimekueleza punguzo la bei kwa aslimia, ndio nikakuambia kutoka 1000 hadi 500 ni punguzo la asilimia 100

Kutoka 12000 hadi 8000 ni punguzo la asilimia 50. Nakufundisha hesabu ndogo tu, sijui Kama kichwa yako ipo vizuri. Ila utaelewa

Price percentage

Original Value - New Value ÷ New Value × 100

Hapo ndio unatapa asilimia la ongezeko la bei au punguzo

Kwenye 1000 na 500 unafanya hivi

1000 - 500÷500 × 100
= 100%

Kwenye 12000 na 8000 unafanya hivi

12000 - 8000÷8000 × 100
= 50%
 
Yeah, hao jamaa wanaomtisha ni mabumunda hayajui biashara inasemaje! Mkuu Kahama hata pale Old Traford jamaa kilo wanapiga elfu 14 iliyokwanguliwa mafuta wakati wengine wanauza elfu 10 lakini wateja wanajaa na anamaliza mzigo! Waache ujinga! Mwamba asiwalegezee!
 
Upo sahihi ila haitoshi kuipa nguvu hoja yako.
 
Achana na hiyo mbwiga anajifanya kujua wakati hajui! Anatukana watu wanaotoa ushauri! Kwa ni watu wampangie bei kama anaona kwake inamlipa? Kama huko wanakochukulia mzigo wanapigwa si wawe wateja wake jamaa awauzie kwa bei ya jumla jumla!
 
Kama vipi achana na nyama wewe wauzie hao wapuuzi Ngurue,
Au wauzie bei unayonunulia mkose wote😜😜😜, jokin.

Humu kila mtu mbabe, acheni utani, huyu jamaa kama yupo serious watampeleka pluto ujuee, kumbuka ni mgeni, hata hajui pale wana backup gani, maana mpk kumtishia mtu uhai yahitaji kujiamini kwa kitu flani na Kwa mtu anayejielewa HUWEZI mtishia mtu uhai kwa utani..
Ripoti polisi, ukiweza weka hata tangazo nje la kutishiwa uhai sbb ya kuwauzia nyama bei hio..
 
Natamani ningekutana na huo ugomvi. Kuna kitu ningewafundisha hao mazezeta.

Sasa hivi nchi nzima ni mwendo wa kuvunja bei tu, sijui hao wapumbavu wapo Kijiji gani bado wanatishiana kizembe hivyo.

Leo hii hadi wanaouza magari yard nao wanashindana kwenye Bei. Kuna yard ipo Morocco pale wao wameamua kuuza IST mil 12, wakati yard zingine za jirani hapo wanauza mil 15. Na hakuna kutishana Wala kuingiliana, kila mtu ashinde mechi zake.

Kuna Pub mpya ilifunguliwa tabata wakawa wanauza bia 1500, wakati wengine wa pembeni wanauza 2000. Na hakuna noma yoyote.

Vunja Bei katoboa sababu ya kuuza nguo bei ndogo pale sinza, na hata mikoani alipoenda bado alishusha bei zaidi. Mbona hawaendi kumtishia kumuua

Huyu jamaa inabidi aseme yupo Kijiji gani ili tuone namna ya kumsaidia kupambana na mafala mazezeta kama hayo.
 
Hakuna ugeni wowote, huyo ni muoga tu. Hakuna kitu watafanya. Kuna rafiki yangu Kuna mkoa alienda kuweka biashara ya spare za magari, lakini akawa anauza kwa bei ndogo, wakaanza kutaka kuleta hayo maneno, mbona mwisho wa siku walinywea. Mtaji wangu, Kodi nalipa Mimi, alafu Bei anipangie fala mmoja hivi.

Ndio maana watu wanaamua kuwekeza dar zaidi kuliko huko vijijini sababu ya upumbavu Kama huo. Dar hata uamue kugawa bure ni wewe tu
 
Mkulungwa ni mjuaji useless. Point kuu ni mfanya biashara mmoja kushusha bei zaidi ya mwenzake ili ku win wateja wengi zaidi ya mshindani wake.

Hayo mambo ya umbali sijui nini na nini hayana maana kwasababu soko lao wote lipo dar hapo hapo, hivyo tetemeko la bei ndo kwenye maji ya uhai lazima limkumbe yeyote yule anayefanya biashara ya maji safi hapo dar.
 
Kuna jamaa anasema eti labda huko vijijini ndo wanapangiana bei ila huko mjini aliko hapangiwi.

Aende sehemu ya mabucha hukohuko mjini aliko aone kama kama bei zinatofautiana kwa zaidi ya buku.

Wauza bucha wana roho ngumu mno, wanatumia sana uchawi kwenye biashara zao.
Kuna jamaa yangu mwanae anadondosha udenda mpaka leo, mkewe alikua kila siku yuko mwezini hadi akamkimbia jamaa ndo akapona.

Mtu kaivuruga familia yake ili auze we wewe kindezi tu ushushe bei kudadadeki, lazma uonane na izraelk uso kwa macho.
 
Yamezoea kunyonya watu! Na hicho kijiji wangehamasishwa kususia kula kitimoto hapo kwa miezi mitatu ili haya mabumunda yafunge biashara! Pumbavu kabisa!
 
Aende sehemu ya mabucha hukohuko mjini aliko aone kama kama bei zinatofautiana kwa zaidi ya buku
Hakuna bwana sijui mko wapi? Mimi niko Shy hapa kuna mtaa mibucha imepangana kama 6 hivi na kuna bucha moja mpaka unapata nyama kwa elfu 4 kwa kilo wakati wengine wanauza elfu 6 na hakuna kutishana! Hawa jamaa ni waroho tu wanataka wapige super profit.
 
mpaka anatishwa jua katikisa uchumi wa watu.
Hao wanaouza 6000 na na wengine 4000 jua wote wanaweza kuuza hiyo 4000 ila ni ukilitimba tu.
Ila kwa mleta uzi hali ni mbaya, mtu anaona akiuza 8000 badala ya 12000 ni loss.
Huko shy nyie wateja ndo mmekubali kupigwa kizembe, na kama bei hiyo 4000 ipo mda mrefu na bado mnanunua kwa wale wa 6000 basi wateja vilaza ni nyie ndo maana wanauza ivo.
 
Unapata faida au hasara? Na kama hakuna ulazima wa bei kuwa 12k, kwa nini usipatane nao angalau ikawa 10k? Inaelekea wamepandisha bei kwa tamaa zao tu, haikuwa na sababu.
 
Kumbe nawe ni kiazi much know. Wote kuwa Dar haijalishi, kinachojalisha ni umbali. Kushusha bei ili ku win wateja ni hoja moja, na kuangalia mazingira ama mapatano na wenzako ambao upo nao karibu SANA, ni hoja nyingine. Kwa nature ya case hii, huyu mtoa mada yupo karibu mno kama siyo adjacent au next to his opponents kabisa, that matters!. Pia, bei ya serikali ya nyama ni kiasi gani?

Hizo sehemu mnazotoa mifano ni kuwa wanauza bei tofauti na wapo peace, hawana nongwa. Ila kwa mtoa mada wameshaanza mpaka kutishia uhai wake, then mnamvimbisha kichwa aende polisi? Polisi ni hatua ya mwisho baada ya mazungumzo ya amani ku fail, na siyo kukurupuka tu kama mnavyomshauri.

Hata kama, discount ya 4000? Kwenye biashara ya nyama? Hebu fuatilia kwa hapa Dar sehemu yoyote yalipo mabucha ya nyama yaliyo karibu kabisa, kama kuna punguzo la elfu nne! Then njoo utoe address na utoe jibu.

Next time tikisa hilo dishi lako then uje kwenye midahalo mikubwa kama hii. Punguza ulaji wa ugali. Period!.
 
Na ndicho nilichosema. Je, alifuata kanuni na taratibu za kushusha bei tena kwa sh 4000??? Issue ni uhai wa mtoa mada. Wengi humu ni wajinga wanakariri kuwa kuua ni kwa kutumia njia zinazoonekana tu hivyo wanashauri 'eti' aende polisi. Ukiangalia kipembuzi ni ushauri wa kijinga. Akae nao wajadili kama hiyo elfu nne apunguze au la, hapa ni mjini tunaishi kwa kanuni hatuishi kienyeji enyeji kama 'kolo' mmoja hapo juu alivyoongea 'utumbo' wake.

Akiuawa mtoa mada watakuwa wa kwanza kutoa RIP's za kinafiki. Na ndiyo maana nasema, humu majinga ni mengi sana tofauti na nilivyojua.

4000 discount out of 12000? Tena kwa wafanyabiashara alionao mkabala kabisa??? Ni taahira pekee anaweza kushauri huyu mtoa mada aende polisi. Kuna mengi ya ku sort kwa huyu mtoa mada before hajaenda polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…