Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Heri ya Pasaka!

Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.

Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.

Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.

Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.

Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.
Niliwahi kimsikia Mzee wa upako kuwa nguruwe hachinjwi
 
Toa Tangazo, Ripoti Polisi,

Pandisha Bei Kutoka 8000-11000 au Uza 12000 Toa Nyongeza Kilo Moja Kwa Mteja Anayenunua Kuanzia kilo 5
Tafuta Njia Nzuri Ya Kubakiza Wateja Kwa Mfano Toa Zawadi ya limao,Vifungashio Na Fanya derivery kwa wateja wakubwa.
Na hapo haya mapuuzi yatamfuata tu! Akilegeza msimamo tu imekula kwake! Yatampangia masharti tena hakuna kutoa limau, wala vifungashio!
 
Kwanza kutoka 1000 mpaka 500 hujaeleza ni 50% of what??? Umeiweka kienyeji na ina hang! Kitaalamu hutakiwi kuwa careless kwenye calculations kama ulivyofanya.

Na una uhakika kweli kuwa punguzo la 4000 kutoka 12000 ni asilimia hizo ulizotaja?

NB: weka wazi which is which, usi hang.
Mimi nimekueleza punguzo la bei kwa aslimia, ndio nikakuambia kutoka 1000 hadi 500 ni punguzo la asilimia 100

Kutoka 12000 hadi 8000 ni punguzo la asilimia 50. Nakufundisha hesabu ndogo tu, sijui Kama kichwa yako ipo vizuri. Ila utaelewa

Price percentage

Original Value - New Value ÷ New Value × 100

Hapo ndio unatapa asilimia la ongezeko la bei au punguzo

Kwenye 1000 na 500 unafanya hivi

1000 - 500÷500 × 100
= 100%

Kwenye 12000 na 8000 unafanya hivi

12000 - 8000÷8000 × 100
= 50%
 
Uko sahihi kabisa naheshimu theory na waliozidevelop sio wajinga, wafanyabiashara wanaomake almost wanacheza na hizo theory, basi tuje uraiani unalotaka wewe, ngoja nijikite sehemu nilipo mara nyingi yaani kahama na mbogwe, mfano choma zone hapa kahama office yake kaibrand kuwa ni v.i.p and luxury hapo theory ya regressive of demand and supply imetiki, pale jamaa nyama choma nusu anauza elf9 na siku za weekend huwa anamaliza ngo'mbe mzima pamoja na bei kuwa juu. Jiulize kwanini haendi kuhangaika na Kuwatisha wachoma nyama wa pale stendi CDT wakati nusu wanauza elf5 na wakati mwingine ukihataji hata Kwa elf2 na ugali wanakubalansia? Twende mbogwe pale kitimoto sehemu nyingi nusu ni elf4 Ila kuna sehemu moja ni VIP kimtindo nimepasahau nusu ni elf6 na wala hafikirii kwenda Kuwatisha hao wanaouza elf4. Hapa kahama sehemu nyingi na hasa stend ndogo nusu ya kitimoto ni elf5 Ila twiga si mbali na stendi wanauza nusu elf7 na hawajawahi kutishia mtu kisa anauza bei ya chini. Nisikukatalie Sana hii kutishiana Kwa sehemu za vijijini huwa inatokea na tena si bei tu hata kuanzisha biashara inayofanana na taikoni wa kijiji Kwa kweli utapata tabu kiroho na kilaivulaivu kabisa.
Yeah, hao jamaa wanaomtisha ni mabumunda hayajui biashara inasemaje! Mkuu Kahama hata pale Old Traford jamaa kilo wanapiga elfu 14 iliyokwanguliwa mafuta wakati wengine wanauza elfu 10 lakini wateja wanajaa na anamaliza mzigo! Waache ujinga! Mwamba asiwalegezee!
 
Mimi nimekueleza punguzo la bei kwa aslimia, ndio nikakuambia kutoka 1000 hadi 500 ni punguzo la asilimia 100

Kutoka 12000 hadi 8000 ni punguzo la asilimia 50. Nakufundisha hesabu ndogo tu, sijui Kama kichwa yako ipo vizuri. Ila utaelewa

Price percentage

Original Value - New Value ÷ New Value × 100

Hapo ndio unatapa asilimia la ongezeko la bei au punguzo

Kwenye 1000 na 500 unafanya hivi

1000 - 500÷500 × 100
= 100%

Kwenye 12000 na 8000 unafanya hivi

12000 - 8000÷8000 × 100
= 50%
Upo sahihi ila haitoshi kuipa nguvu hoja yako.
 
Umetoka kulalamika juu kuwa jamii forums imekosa watu great thinkers sababu ya ushauri wanaoutoa, lakini kwa comment yako hii basi niseme una shida kuliko unaowalalamikia

Kutoka sh 1000 hadi sh 500, na kutoka sh 12000 hadi sh 8000, unasema lipi ni ongezeko kubwa? Hapa kwanza ncheke[emoji23][emoji23], hata hesabu za asilimia tu zimekupiga chenga? Wewe ni sawa na wale wanaoulizwa kilo 1 ya mawe na kilo 1 ya manyoya ipi nzito

Pili unasema mengi biashara yake haikua karibu na bakhressa? Hapa napo ncheke[emoji23][emoji23], kichwani kuna medula kweli huko? Hujui hawa Wana viwanda na wanawauzia wauzaji wa jumla? Kushusha huko huoni kama wale wauzaji wa jumla wengi watakimbilia kwa bakhressa kwa kuwa itakua rahisi kwao kupata wateja wengi sababu ya Bei ndogo?
Achana na hiyo mbwiga anajifanya kujua wakati hajui! Anatukana watu wanaotoa ushauri! Kwa ni watu wampangie bei kama anaona kwake inamlipa? Kama huko wanakochukulia mzigo wanapigwa si wawe wateja wake jamaa awauzie kwa bei ya jumla jumla!
 
Kama vipi achana na nyama wewe wauzie hao wapuuzi Ngurue,
Au wauzie bei unayonunulia mkose wote😜😜😜, jokin.

Humu kila mtu mbabe, acheni utani, huyu jamaa kama yupo serious watampeleka pluto ujuee, kumbuka ni mgeni, hata hajui pale wana backup gani, maana mpk kumtishia mtu uhai yahitaji kujiamini kwa kitu flani na Kwa mtu anayejielewa HUWEZI mtishia mtu uhai kwa utani..
Ripoti polisi, ukiweza weka hata tangazo nje la kutishiwa uhai sbb ya kuwauzia nyama bei hio..
 
Yeah, hao jamaa wanaomtisha ni mabumunda hayajui biashara inasemaje! Mkuu Kahama hata pale Old Traford jamaa kilo wanapiga elfu 14 iliyokwanguliwa mafuta wakati wengine wanauza elfu 10 lakini wateja wanajaa na anamaliza mzigo! Waache ujinga! Mwamba asiwalegezee!
Natamani ningekutana na huo ugomvi. Kuna kitu ningewafundisha hao mazezeta.

Sasa hivi nchi nzima ni mwendo wa kuvunja bei tu, sijui hao wapumbavu wapo Kijiji gani bado wanatishiana kizembe hivyo.

Leo hii hadi wanaouza magari yard nao wanashindana kwenye Bei. Kuna yard ipo Morocco pale wao wameamua kuuza IST mil 12, wakati yard zingine za jirani hapo wanauza mil 15. Na hakuna kutishana Wala kuingiliana, kila mtu ashinde mechi zake.

Kuna Pub mpya ilifunguliwa tabata wakawa wanauza bia 1500, wakati wengine wa pembeni wanauza 2000. Na hakuna noma yoyote.

Vunja Bei katoboa sababu ya kuuza nguo bei ndogo pale sinza, na hata mikoani alipoenda bado alishusha bei zaidi. Mbona hawaendi kumtishia kumuua

Huyu jamaa inabidi aseme yupo Kijiji gani ili tuone namna ya kumsaidia kupambana na mafala mazezeta kama hayo.
 
Kama vipi achana na nyama wewe wauzie hao wapuuzi Ngurue,
Au wauzie bei unayonunulia mkose wote[emoji12][emoji12][emoji12], jokin.

Humu kila mtu mbabe, acheni utani, huyu jamaa kama yupo serious watampeleka pluto ujuee, kumbuka ni mgeni, hata hajui pale wana backup gani, maana mpk kumtishia mtu uhai yahitaji kujiamini kwa kitu flani na Kwa mtu anayejielewa HUWEZI mtishia mtu uhai kwa utani..
Ripoti polisi, ukiweza weka hata tangazo nje la kutishiwa uhai sbb ya kuwauzia nyama bei hio..
Hakuna ugeni wowote, huyo ni muoga tu. Hakuna kitu watafanya. Kuna rafiki yangu Kuna mkoa alienda kuweka biashara ya spare za magari, lakini akawa anauza kwa bei ndogo, wakaanza kutaka kuleta hayo maneno, mbona mwisho wa siku walinywea. Mtaji wangu, Kodi nalipa Mimi, alafu Bei anipangie fala mmoja hivi.

Ndio maana watu wanaamua kuwekeza dar zaidi kuliko huko vijijini sababu ya upumbavu Kama huo. Dar hata uamue kugawa bure ni wewe tu
 
Ni wewe ndiyo wa kuelewa, siyo mimi.

"Nimekueleza kuhusu asilimia kwa sababu, huyu mmoja kashusha kwa asilimia 100, alafu huyo mwingine kashusha kwa asilimia 50.

Unasema tusilinganishe punguzo la 500 na punguz la 4000. Kwani bakhressa Hilo punguzo la 500 unafikiri lipo kwenye chupa 1 ya maji au carton 1?? Huyo aliyepunguza sh 4000 unahisi amepunguza sana kuliko va bahressa aliyepunguza sh 500 kwa mamilion ya chupa za maji anazozalisha na kuuza, huyo muuza kitimoto aliyepunguza 4000 kwa kilo wewe unahisi anakosa sh ngapi kulinganisha na bakhressa aliyepunguza sh 500 kwa chupa 1? "
[emoji115][emoji115]
Umechanganya tena madesa. Una uhakika mmoja kashusha 100% na mwingine kashusha 50% kabisa? Really??

Hujaelewa kitu kimoja, hatuzungumzii mamilioni ya chupa au maelfu ya kilo za nyama ya nguruwe. Tunazungumzia unit ya measurement ya nyama yaani Kilo na litre(kwa maji). Bado hakuna usawa miongoni mwa hawa watu. Pia hujaeleza umbali kati ya viwanda vya Mengi na Bakhresa. Eleza na hapo tumalize mjadala kitaalamu.

Distribution ya wateja inategemea umbali wa eneo la bidhaa pia, kitu ambacho nimekuuliza hujajibu, I dont know umekwepa kujibu au la.
Mkulungwa ni mjuaji useless. Point kuu ni mfanya biashara mmoja kushusha bei zaidi ya mwenzake ili ku win wateja wengi zaidi ya mshindani wake.

Hayo mambo ya umbali sijui nini na nini hayana maana kwasababu soko lao wote lipo dar hapo hapo, hivyo tetemeko la bei ndo kwenye maji ya uhai lazima limkumbe yeyote yule anayefanya biashara ya maji safi hapo dar.
 
kuna majitu humu ni majinga mno. JF si home of great thinkers tena kwa sababu ya wajinga na wapumbavu kama siyo mamburula wachache. Ushauri wanaompa mtoa mada ni wa kitoto sana. Sijui hata kama wanafikiria impact ya ushauri huo. Wengi mpaka sasa zaidi ya 97% wametoa ushairi wa kipuuzi na wa kimburula mno. Hii si JF ya miaka hiyo. Halafu wakishauriwa wanaleta ujuaji. Hivi ushushe bei kutoka 12000 mpaka 8000 kweli? Hao jamaa kwanza ni wastaarabu sana na walimfuata kiungwana. Wote wanategemea biashara hiyo na wana familia pia, mbaya zaidi amewakuta kwenye biashara, angeshusha atleast 1000 angepungukiwa nini? Asikaze kichwa, akae nao mezani wajadili vizuri kwa amani, wote ni wafanyabiashara. Aachane na ushauri wa mamburula wa humu.
Kuna jamaa anasema eti labda huko vijijini ndo wanapangiana bei ila huko mjini aliko hapangiwi.

Aende sehemu ya mabucha hukohuko mjini aliko aone kama kama bei zinatofautiana kwa zaidi ya buku.

Wauza bucha wana roho ngumu mno, wanatumia sana uchawi kwenye biashara zao.
Kuna jamaa yangu mwanae anadondosha udenda mpaka leo, mkewe alikua kila siku yuko mwezini hadi akamkimbia jamaa ndo akapona.

Mtu kaivuruga familia yake ili auze we wewe kindezi tu ushushe bei kudadadeki, lazma uonane na izraelk uso kwa macho.
 
Natamani ningekutana na huo ugomvi. Kuna kitu ningewafundisha hao mazezeta.

Sasa hivi nchi nzima ni mwendo wa kuvunja bei tu, sijui hao wapumbavu wapo Kijiji gani bado wanatishiana kizembe hivyo.

Leo hii hadi wanaouza magari yard nao wanashindana kwenye Bei. Kuna yard ipo Morocco pale wao wameamua kuuza IST mil 12, wakati yard zingine za jirani hapo wanauza mil 15. Na hakuna kutishana Wala kuingiliana, kila mtu ashinde mechi zake.

Kuna Pub mpya ilifunguliwa tabata wakawa wanauza bia 1500, wakati wengine wa pembeni wanauza 2000. Na hakuna noma yoyote.

Vunja Bei katoboa sababu ya kuuza nguo bei ndogo pale sinza, na hata mikoani alipoenda bado alishusha bei zaidi. Mbona hawaendi kumtishia kumuua

Huyu jamaa inabidi aseme yupo Kijiji gani ili tuone namna ya kumsaidia kupambana na mafala mazezeta kama hayo.
Yamezoea kunyonya watu! Na hicho kijiji wangehamasishwa kususia kula kitimoto hapo kwa miezi mitatu ili haya mabumunda yafunge biashara! Pumbavu kabisa!
 
Aende sehemu ya mabucha hukohuko mjini aliko aone kama kama bei zinatofautiana kwa zaidi ya buku
Hakuna bwana sijui mko wapi? Mimi niko Shy hapa kuna mtaa mibucha imepangana kama 6 hivi na kuna bucha moja mpaka unapata nyama kwa elfu 4 kwa kilo wakati wengine wanauza elfu 6 na hakuna kutishana! Hawa jamaa ni waroho tu wanataka wapige super profit.
 
mpaka anatishwa jua katikisa uchumi wa watu.
Hao wanaouza 6000 na na wengine 4000 jua wote wanaweza kuuza hiyo 4000 ila ni ukilitimba tu.
Ila kwa mleta uzi hali ni mbaya, mtu anaona akiuza 8000 badala ya 12000 ni loss.
Huko shy nyie wateja ndo mmekubali kupigwa kizembe, na kama bei hiyo 4000 ipo mda mrefu na bado mnanunua kwa wale wa 6000 basi wateja vilaza ni nyie ndo maana wanauza ivo.
 
Heri ya Pasaka!

Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.

Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.

Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.

Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.

Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.
Unapata faida au hasara? Na kama hakuna ulazima wa bei kuwa 12k, kwa nini usipatane nao angalau ikawa 10k? Inaelekea wamepandisha bei kwa tamaa zao tu, haikuwa na sababu.
 
Mkulungwa ni mjuaji useless. Point kuu ni mfanya biashara mmoja kushusha bei zaidi ya mwenzake ili ku win wateja wengi zaidi ya mshindani wake.

Hayo mambo ya umbali sijui nini na nini hayana maana kwasababu soko lao wote lipo dar hapo hapo, hivyo tetemeko la bei ndo kwenye maji ya uhai lazima limkumbe yeyote yule anayefanya biashara ya maji safi hapo dar.
Kumbe nawe ni kiazi much know. Wote kuwa Dar haijalishi, kinachojalisha ni umbali. Kushusha bei ili ku win wateja ni hoja moja, na kuangalia mazingira ama mapatano na wenzako ambao upo nao karibu SANA, ni hoja nyingine. Kwa nature ya case hii, huyu mtoa mada yupo karibu mno kama siyo adjacent au next to his opponents kabisa, that matters!. Pia, bei ya serikali ya nyama ni kiasi gani?

Hizo sehemu mnazotoa mifano ni kuwa wanauza bei tofauti na wapo peace, hawana nongwa. Ila kwa mtoa mada wameshaanza mpaka kutishia uhai wake, then mnamvimbisha kichwa aende polisi? Polisi ni hatua ya mwisho baada ya mazungumzo ya amani ku fail, na siyo kukurupuka tu kama mnavyomshauri.

Hata kama, discount ya 4000? Kwenye biashara ya nyama? Hebu fuatilia kwa hapa Dar sehemu yoyote yalipo mabucha ya nyama yaliyo karibu kabisa, kama kuna punguzo la elfu nne! Then njoo utoe address na utoe jibu.

Next time tikisa hilo dishi lako then uje kwenye midahalo mikubwa kama hii. Punguza ulaji wa ugali. Period!.
 
Kuna jamaa anasema eti labda huko vijijini ndo wanapangiana bei ila huko mjini aliko hapangiwi.

Aende sehemu ya mabucha hukohuko mjini aliko aone kama kama bei zinatofautiana kwa zaidi ya buku.

Wauza bucha wana roho ngumu mno, wanatumia sana uchawi kwenye biashara zao.
Kuna jamaa yangu mwanae anadondosha udenda mpaka leo, mkewe alikua kila siku yuko mwezini hadi akamkimbia jamaa ndo akapona.

Mtu kaivuruga familia yake ili auze we wewe kindezi tu ushushe bei kudadadeki, lazma uonane na izraelk uso kwa macho.
Na ndicho nilichosema. Je, alifuata kanuni na taratibu za kushusha bei tena kwa sh 4000??? Issue ni uhai wa mtoa mada. Wengi humu ni wajinga wanakariri kuwa kuua ni kwa kutumia njia zinazoonekana tu hivyo wanashauri 'eti' aende polisi. Ukiangalia kipembuzi ni ushauri wa kijinga. Akae nao wajadili kama hiyo elfu nne apunguze au la, hapa ni mjini tunaishi kwa kanuni hatuishi kienyeji enyeji kama 'kolo' mmoja hapo juu alivyoongea 'utumbo' wake.

Akiuawa mtoa mada watakuwa wa kwanza kutoa RIP's za kinafiki. Na ndiyo maana nasema, humu majinga ni mengi sana tofauti na nilivyojua.

4000 discount out of 12000? Tena kwa wafanyabiashara alionao mkabala kabisa??? Ni taahira pekee anaweza kushauri huyu mtoa mada aende polisi. Kuna mengi ya ku sort kwa huyu mtoa mada before hajaenda polisi.
 
Back
Top Bottom