Alfajr ya leo kumekucha naamshwa na mke wangu, Anaomba nimpatie nauli, MDA wa Safari yake ndo huu. Nikamjibu "Nmeshaghaili, safar yako haipo Tena"
Akauliza tatizo Nini, mbona Jana tushakubaliana alfajir leo naondoka?. Nikamjibu, "Nmeshaghaili sasa, hakuna Safari yoyote ile, na sitaki unihoji maswali yoyote yale" akasema "sawa,ila unachofanya sio halali mme wangu" .Sikumjibu, nikaamka nikaoga, nikavaa na Kwenda zangu kazini
Nmefika kazini salama, nmejaribu kufanya Kazi ila haziend vizur. Kila nikijaribu kuliwazia tukio la Juzi la laini mpya, Kisha Hii presha ya wife kulazimisha hii Safari, kiukweli Moyo wangu umekua mzito Sana kumruhusu mke wangu asafiri.
Pengine sijajua kama nakosea au vipi,
Ila nmedhamiria kabisa MKE wangu hatosafiri kwenda popote pale msimu huu wote wa sikukuu.
Nawasilisha wakuu[emoji1431]