Nimepigwa na mume

Nimepigwa na mume

leirilwa

Senior Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
118
Reaction score
22
Jamani wadau,

Naomba msaada,

Nimepigwa na mume na kuumia vibaya.

Sheria iko vipi katika hili?
 
Ndo Mara ya kwanza kukupiga? Huwezi me mchukulia Sheria then mkaendelea ishi! Kama umechoka ishi naye sema tukushauri
 
Sheria ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake ipo.bt kama ni mara ya kwanza mvumilie akizidi kukufanyia hivyo una haki ya kwenda kumstaki"!
 
Hakuna anayepigwa pasipo sababu ndio useme ulimfanya nn
 
fanya hivi,
kama una majeraha ama ushahidi nenda polisi dawati la jinsia utapata msaada.
Au siku nyingine akitaka kukupiga akikisha umemtia jeraha hakika hatorudia tena.ila na wewe ataweza kukuchukulia hatua za kisheria pia.
 
Ndio hivyo labda umejiandaa kuachana nae dadangu vinginevyo vumilianeni ndio maisha ya ndoa
 
Pole sana,naomba nikulize hii ndio mara yako ya kwanza kupigwa? amekupiga kosa nini? mumeo ni mtu wa wapi? umesha zaa nae? wazazi wenu wako hai?
 
Pole sana dada.

Wanaume wanaopiga wanawake wengi wao wana shida kwenye uanaume wao au aina ya malezi waliyopata. Kama sio ana ishu ambayo inampunguzia uanaume wake(kama vile matatizo ya nguvu za kiume,uume mdogo,kuonewa na wanaume wenzake physically);-->Wenye shida hizi huhisi kama vile ili ku-prove uanaume wao(male ego) ambao unakuwa umeshuka kwa kasi ya ajabu, basi ni lazima na muhimu wawanyanyase na kuwapiga viumbe ambao ni dhaifu kwao(wanawake, watoto); Na huwa wanakuwa wakali wakali muda wote bila sababu yoyote ya msingi.

Au utakuta something went wrong wakati wa malezi yake(malezi ya mzazi mmoja,mama yake kunyanyaswa na baba yake mbele yake alipokuwa mdogo, historia ya kuwa sexually abused alipokuwa mdogo, malezi ya kimila ambayo yanasisitiza katika kuwaona wanawake kama sio binadamu au kama vile watoto).

Ni ukale wa kizamani sana kupiga mwanamke karne hii(japokuwa nakubali asilimia 100 kuwa mara nyingine wanawake huwa wana tempt sana uwapige---lakini hii kwa mwanaume wa kawaida asie na shida kisaikolojia atajizuia, na akizidiwa sana atampiga mwanamke kofi moja au mawili; Na sio kufikia extent ya kumpiga hadi kumtoa ngeu)
 
Hakuna anayepigwa pasipo sababu ndio useme ulimfanya nn
sikumtukana hataki nimrekebishe akikosea na hataki na mtoto akifanya kosa hataki nimuadhibu au kumgombeza mbele yake sasa kichapo kilianza pale nilipojaribu kumkosoa
 
Hiyo ni kama kupigwa na mtu yeyote. Ni jinai inayopaswa kuripotiwa Polisi na baadaye mhusika apelekwe mahakamani. Acheni kuficha jinai kwenye kichaka cha ndoa
 
Pole sana,naomba nikulize hii ndio mara yako ya kwanza kupigwa? amekupiga kosa nini? mumeo ni mtu wa wapi? umesha zaa nae? wazazi wenu wako hai?
nimezaa naye watoto watatu,mume wangu ni mtu wa manyara,wazazi wako hai,kosa alilonipiga nilimkosoa kwa alichokifanya ambacho hakikunifurahisha mimi
 
ssa unataka utaka sheria ili ufanyeje??? Km umeweza kumkosoa kaa nni na hilo usimshaur?
 
Kosa la jinai tafuta Penal Code ni kosa sawa na kupigwa na mtu yeyote yule peleka malalamiko polisi nao watafungua kesi andaa ushahidi anapelekwa segerea asubuhi na mapema! Hawezi kuichezea jamhuri hivihivi
 
Back
Top Bottom