Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Arsenal Gunner

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
10,891
Reaction score
17,718
Aisee siku ya Jana imekuwa mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi Kwa mujibu wake huyu binti walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajifanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float

Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu.

Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu

Naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo
 
Inasikitisha sana
img_2_1749577063094.jpg
 
Aisee siku ya Jana imekua mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajufanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu. Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo
Mungu wangu .......Pole sana Mkuu. Maumivu hayo nimeyahisi hata mimi wakati nasoma ujumbe huu.

Ni vizuri pia kufatilia kama huyo Dada hajahusika. Maana ulishamweleza tahadhari hizo.

Madogo siku hizi ni wajanja sana. Usiwaone wanajifanya washamba au wapole.
 
Back
Top Bottom