Aisee siku ya Jana imekuwa mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajifanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float
Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu.
Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu
Naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo