Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Hiyo situation ni ngumu sana kuchomoka aseeh! Jamaa sio lazma wakuombe kuchomoa line, rafiki yangu aliombwa tu simu apige.. yaan within seconds mtu kashabadili jina! Ngumu sana kuchomoka hapo japo i can't rule out uwezekano wa kucheza hiyo game
Yaani boss wanamjua namba yake na kusave jina hapo hapo wewe hujashtuka? Hata hivyo sishangai maana watz uwezo mdogo sana wa kuchakata mambo.
 
Yaani boss wanamjua namba yake na kusave jina hapo hapo wewe hujashtuka? Hata hivyo sishangai maana watz uwezo mdogo sana wa kuchakata mambo.
Kinachofanyika ni kwa mfano, mimi nasevu namba yako kama "boss bush" tapeli akichukua simu yangu anachokifanya anaedit namba tu kwa kuondoa za boss og na kuwekwa namba feki lkn jina ni lilelile, hiyo inakuwa mbaya zaidi kama boss na mfanyakazi wana kawaida ya kuwasiliana kwa kuchati
 
Aisee siku ya Jana imekuwa mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi Kwa mujibu wake huyu binti walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajifanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float

Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu.

Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu

Naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo
Inamaana aliwatumia pesa kwa kupigiwa au kwa ujumbe?
Kama ni hivyo rekebisha yafuatayo.
Asitume pesa kwako bila simu yako wewe ya kuongea 2.weka namba yako ya private yaani yako na wafanyakazi wako na ujipe jina lako la siri mfano(Tigger) that means hata mwizi aje vipi wafanyakazi wasiposikia hiyo tigger pesa hawatoi.
3.control kiasi cha pesa kwa wafanyakazi wako
4.punguza mazoea na wafanyakazi.
5.waoe semina wafanyakazi hada za utapeli
6.uyo dada usimfukuze endelea nae na uwe unamvizia unaomba cm yake binafsi uone anachart nin
 
Kinachofanyika ni kwa mfano, mimi nasevu namba yako kama "boss bush" tapeli akichukua simu yangu anachokifanya anaedit namba tu kwa kuondoa za boss og na kuwekwa namba feki lkn jina ni lilelile, hiyo inakuwa mbaya zaidi kama boss na mfanyakazi wana kawaida ya kuwasiliana kwa kuchati
Aisee hatari sana.
 
Kwanini usiongee na JB mshirikiane kutengeneza bongo movies maana kwenye kuandaa script uko vizuri sana
Uzi ulitakiwa uwe mwakani, anaeleza yaliyomsibu mwaka huu hapo sawa

Milioni 8 kibongobongo batani unaziona wapi za kuandikia uzi

Huyu katudharau sana
 
Aisee hatari sana.
Naam mkuu ndiomaana situation kama hiyo kung'amua kwa harakaharaka haiwi rahisi mzee.. ni sawa na mchepuko uondoe namba ya wife na kuweka yake kwenye namba iliyoseviwa kama wife... alafu aaanze kukuletea mitego 😂😂 lazima tu akutikise kiaina
 
Huu ni ujasusi
 
Biashara ya Wakala ni pasua kichwa asikwambie mtu....tuliamua kunyosha mikono juu....👏
 
Kuna wakati una amua kuajiri Msichana kwa sbb wengi ni waaminifu.
Lakini kwa upande mwingine ni watu rahisi sana kutapeliwa.

Mawakala wengi wanao tapeliwa ni wanawake/wasichana.
Unaweza chapisha maelekezo na kubandika sehemu anayo iona mara zote, lakinio bado anaibiwa.

Milion nane kipindi hiki ni nyingi, pole mkuu.
 
pole sana ndugu ukiwaona kupitia tv asilia utawajua.
kama inaweza kukusaidia kwanamna hiyo tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom