Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

J
Uyo binti inawezkana hao watu ni watu waliokuja kimazoea na kumuachia vitipu vya hapa na pale sasa akawa kawazoea ndo maana hata simu akawaachia mpaka kutokea utapeli huo ila pole sana mkuu uyu binti kama inakupendeza msamehe tu muachie Mungu atakulipa zaidi
Hakuna kitu hatari kwenye uwakala kama kuleta mazoea na wateja. Kitu ambacho watu hawajui ni kuwa hao wateja wako ndio matapeli wenyewe
 
Sio mzembe kulizwa kwenye hio biashara nje nje mkuu, mimi nilisha achana nazo hizo biashara za miamala
 
Aisee siku ya Jana imekuwa mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi Kwa mujibu wake huyu binti walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajifanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float

Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu.

Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu

Naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo
Pole,usimlaumu hua inatokea kutapeliwa,matapeli wana mbinu nyingi
Ni kukubali hasara na kujipanga upya
Kuna wakala nae alipigwa milioni 3 kwa njia hizo hizo
 
Wanaotapeliwa sio wendawazimu Mkuu,hio huo inatokea tu
Kuna mfanyakazi wangu mmoja alitapeliwa zaidi ya mil 8. Ni uwendawazimu kwa sababu mfanyakazi anafanya jambo la ajabu ambalo hata uwe na akili ya kenge huwezi kufanya jambo kama hilo.
 
Nipo na mothercity safaris na usafirishaji mizigo kutoka SA niombe kazi kwa nani tena mkuu siwezi kudhurumu masikini ili niongeze mali kwenye kampuni tunayowaachia watoto baadae wanashindwa kuendesha kampuni kumbe kulikua na hela za dhuruma ndani yake nimekwambia nina mifano ya watu kibao walikua na hiyo tabia mmoja jana nimemuona Kariakoo anaongea peke sisi huku ni Wakurungwa tunapotoa Elimu tuna mifano halisi.
We jamaa mbishi, haya nipe kazi kwenye kampuni yako basi..!! 😹
 
Kwenye pesa hapana tucheke na mengine..!!
Hapo apelekwe polisi wazazi wake km wana pesa wamtolee kufidia hasara..!!

Mtu kakatazwa usitoe simu yeye katoa, hapo nitaamini vipi km hawako wote wameshirikiana?

Hata akisema amkate mshahara hatofanya kazi kwa ufanisi, atafanya bora liende mwisho ataiba tena kwa kujua atakatwa kwa kufanyishwa kazi..!!
Dada nlikuchek kweny ile thread yangu hujanichek tena
 
Hii biashara ya mihamala ni risk sana,jamaa wanawinda kila siku nawana mbinu nyingi hatari,ila mabinti ndio wahanga wakubwa wahaya matukio. binti akisifiwa akitongozwa akili inahama washikaji wanatumia opportunity. Pole mdau
 
Biashara ya hela changamoto sana kama hukai wewe mwenyewe, watoto waliokulia mjini hata uwaeleze vipi watafanya kosa...ukiwakataza kula wakati wakimhudumia mteja...ukiwa haupo watakuwa wanakula huku wanamhudimia mteja. Pole
 
Back
Top Bottom