Nimepooza kiuno hadi chini, msaada tafadhali

Ubarikiwe mkuu
 
Msaaada jamani mwezi wa sita huu nimefanya matibabu ya kila aina,hospital paliponifilisi na mri scan,dawa za asili na kisuuna hadi maombi
Nakata tamaa sasa
Chizi vitabu.

Umesoma vitabu gani.

Na je ipoje concept yako ya Mungu na maisha kwa ujumla? 1. Je hayupo wala hana control yoyote. 2. Je ni jitu ambalo kwa sababu zisizochunguzika linafanyafanya tu jambo linalojiamulia jenyewe(shit happens). Je? 3. Linafanya mambo yake kwetu kwa kusudi maalumu (things happen for a reason). 4 Au ni sisi pamoja na Mungu tunashirikiana kufanyiza mambo yatokee maishani?(we make things happen)???

Tafadhali naomba jibu lenye mrengo wa hapo juu ndio tushauriane zaidi....
 
Asante
 
Usikate tamaa ...utapona...hakikisha unaenda hosp nyinginr kubwa
Hizi hospital kubwa siyo za kuziamini sana nilichogundua madokta huwa hawaendi mbali na jibu linalotoka kwenye kipimo.

Mdogo'angu ameumwa mwaka mzima nikazunguka nae hospital kubwa kasoro MNH sikufika akafanyiwa MRI majibu yakatoka hana anachoumwa aliniacha hoi doctor bingwa wa magonjwa ya mishipa pale KCMC aliposoma MRI results na kumhakikishia dogo huku akiwa macho makavu kwamba yupo fit kuliko u-fit wenyewe mwili wake hauonyeshi ishara ya maradhi yoyote lakini anayeambiwa hivyo analalamika maumivu
 
Ni ngumu lakini jaribu kukubaliana na hali na kupata matibabu yale ya kukufanya uishi vizuri. Si rahisi kupona kupooza. Mtu ugonjwa ukikufika lazima utajaribu kila aina ya tiba, lakini huko kote kwa kupooza utaambulia dissapointment. Ni vyema akiba yako ukaiweka na kuangalia namna utaishi comfortably.
 
Sasa iligundulilka ni nini? Pole sana
 
Sio kweli bwana....atapona ikigundulika shida nn..hijaona ushuhudahuko juu
 
pole sana mkuu yetu ni maombi tu I hope utasaidika ,never give up .
 
Sio magonjwa yote ni ya kibinadamu,magonjwa mengine mnatupiwa yanaonekana ya kawaida kumbe sio.Mpendwa kama unamuamini Kristo sali kwa jina lake utapona.My aunty alitembea na mume wa mtu akatupiwa ukimwi wa kichawi yaani ni anaumwa dalili zote za ukimwi ila akipimwa hamna kilichoonekana.Mpk alipozunguka akapata jibu mpk tunaongea leo ni mzima kabisaaa!
Nimerefer tu ila inaweza isiwe sababu ya kichawi.Ila katika shida yeyote sali Mungu atakuponya
 
Msaaada jamani mwezi wa sita huu nimefanya matibabu ya kila aina,hospital paliponifilisi na mri scan,dawa za asili na kisuuna hadi maombi
Nakata tamaa sasa
Chanzo cha kupooza ni nini pole sana
 
Sasa iligundulilka ni nini? Pole sana
Ndiyo nilimpeleka kwa huyo mkorea tatizo likaonekana kwenye pingili za shingo na mishipa ya fahamu ndo maana akawa kama anapooza upande mmoja wa kulia.

Vyote amepona shida sasa imebaki kichwani anasikia kelele kama za mtu anapiga manyanga,hiyo nayo imekuwa ngumu kutoka kila dogo akienda clinic anaambiwa itaisha though ni gharama nakomaa nae maana kidogo kwa hawa jamaa nimeona kuna mwanga wa kupona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…