Nimepooza kiuno hadi chini, msaada tafadhali

Nimepooza kiuno hadi chini, msaada tafadhali

Usiamini sana shuhuda hizi. Mtu atakwambia fulani alienda kwa fulani akapona, kuna tabibu wa kichina, wa kikorea, Ndodi, Mwamposa, wa kisuna nk nk. Wengi huwa ni wasio na huruma wanaokula pesa za watu wenye matatizo. na ukiwa mgonjwa utajaribu kila kitu kujitibu. Kama hospitali imeshindikana ni ngumu kutibika huko nje.

Mkuu unaishi ulaya au Amerika? Au sio mswahili mwenzetu!?…..ushawahi kuumwa au kuuguza kweli?
 
Hizi hospital kubwa siyo za kuziamini sana nilichogundua madokta huwa hawaendi mbali na jibu linalotoka kwenye kipimo.

Mdogo'angu ameumwa mwaka mzima nikazunguka nae hospital kubwa kasoro MNH sikufika akafanyiwa MRI majibu yakatoka hana anachoumwa aliniacha hoi doctor bingwa wa magonjwa ya mishipa pale KCMC aliposoma MRI results na kumhakikishia dogo huku akiwa macho makavu kwamba yupo fit kuliko u-fit wenyewe mwili wake hauonyeshi ishara ya maradhi yoyote lakini anayeambiwa hivyo analalamika maumivu
Stori yako imeishia katikati
 
Usiamini sana shuhuda hizi. Mtu atakwambia fulani alienda kwa fulani akapona, kuna tabibu wa kichina, wa kikorea, Ndodi, Mwamposa, wa kisuna nk nk. Wengi huwa ni wasio na huruma wanaokula pesa za watu wenye matatizo. na ukiwa mgonjwa utajaribu kila kitu kujitibu. Kama hospitali imeshindikana ni ngumu kutibika huko nje.
Umepinga mpaka umesahau kushauri.
 
Angalia emmanuel.tv then ulete mrejesho hapa. Ni Chanel number 390 dstv au utapata kwenye free chanels za madishi makubwa

Sent from my STK-L21 using JamiiForums mobile app
Huu ushauri mkuu CHIZI VITABU usiufuate. Huwezi kuwa unaugua eti ufungulie TV uangalie kisha upone. It's unthinkable man.

Nimejaribu kufuatilia swali uliloulizwa kuhusu sababu ya kupooza kwako sijaona ukijibu (sijasoma comments zote). Kama kuna uwezekano unge update uzi wako ukaweka sababu za wewe kuwa na hiyo hali basi ingekuwa rahisi zaidi kupata msaada kwakuwa watu wengine hawawezi ku scroll through all comments.

All in all, nakutakia upate ahueni ya unayopitia mkuu. Usikate tamaa kwakuwa hiyo hali yaweza kumfika kila mwanadamu.
 
Hizi hospital kubwa siyo za kuziamini sana nilichogundua madokta huwa hawaendi mbali na jibu linalotoka kwenye kipimo.

Mdogo'angu ameumwa mwaka mzima nikazunguka nae hospital kubwa kasoro MNH sikufika akafanyiwa MRI majibu yakatoka hana anachoumwa aliniacha hoi doctor bingwa wa magonjwa ya mishipa pale KCMC aliposoma MRI results na kumhakikishia dogo huku akiwa macho makavu kwamba yupo fit kuliko u-fit wenyewe mwili wake hauonyeshi ishara ya maradhi yoyote lakini anayeambiwa hivyo analalamika maumivu

Namfahamu dogo mmoja akiwa na umri around miaka 10 alipata a minor accident.

Tembeaji yake ikawa ya shida kupita maelezo kupelekea kufikishwa hospitali. Vipimo vyote MRI, X-ray vilisemekana kutoa majibu kuwa hakuwa na shida yoyote mwilini.

Ilikuwa hadi Consultant Physician - beberu aliyekuwapo alipoamua kuchukua bakora na kutaka kumcharaza kibazazi ndipo dogo alipotimua mbio kuliko mtu mwingine aliyekuwapo hapo, akitokomea kuondoka hospitalini hapo. 🤣🤣

Huo ukawa mwisho wa ugonjwa wa dogo.

Hii mambo ya magonjwa wakati mwingine huwa kuna siri kubwa.

Jeshini wakiita malingering.
 
Back
Top Bottom