Habari Wana Jamvi, nahitaji msaada wenu naona kiza nimepotea kwenye msitu wenye giza na mbwa mwitu wakali.
Mimi Ni Kijana Below 25 Years, nimefanikiwa Kukwepa Anasa Zote Lakin Nimejikuta Nadumbukia Kwenye Uraibu Wa Kununua Madada Poa.
Kama Kijana Mwenye Heshima Mtaani Nisiyeacha Ibada(swala Tano) Nimeshindwa Kuwakwepa Madada Poa Tena Wa Bei Kdogo Elfu 50,70 Kwa Mwezi Naweza Nunua Hata 2 Au Nikijizua Sana Mmoja Na Huwa Sinunui Wa Bei Rahisi.
Naumia Sana Kwanza Na Hii Tabia Pili Kupoteza Pesa Tatu Napoteza Heshima Yangu Binafsi Ingali Huwa Nanunua Mbali Na Eneo Wanaonijua Naona Kama Nina Nidhamu Ya Uwoga Naonesha Heshima Kwa Watu Ikifika Usiku Nakuwa Fisi.
Pesa Yangu Haifanyi Maendeleo Zaidi Ya Hiyo Anasa. Sivuti Bangi, sigara Wala Pombe.
Naomba Kusaidiwa Kuachana Na Hii Tabia Nateseka Sina Amani Ya Moyo. Nipo Kwenye Stage Ambayo Nisiponunua Malaya Ndani Ya Mwezi Naanza Kama Kuumwa Basi Ntakopa Pesa Ili Nikanunue.
Ni Kipindi Cha Mwaka Mmoja Na Nusu Tangu Nianze Kununua Nishalala Na Wanawake 13 Au 14, kuna Kpind Niliacha.
Habari!
Pole kwa unayopitia.
Kwa kuwa umetambua tatizo, amini kwamba uko nusu ya njia ya kulitatua.
Suala la msingi ni kujenga dhamila ya MWILI na ROHO (kutoka ndani mwako na uisimamie).
Ni kweli kuwa unaweza kupata uraibu kama ulivyoutaja. Sababu kuu ni sehemu yako ya ubongo kuutegemea uraibu husika kama chanzo cha furaha yako. Na usipopata msisimko toka kwa kianzisha furaha yako basi mwili hupata mgagasiko na hapo mzunguko wa hitaji hujirudia. Hakuna kurogwa.
Kuna mambo unahitaji kuyazingatia ili kujiondoa kwenye hili:
1: Kutambua jinsi ulivyoingia. Ukipotea njia ili urejee vyema ni muhimu kujua sehemu uliyopitia na kupotea la sivyo kesho na keshokutwa utapotea tena. Tafakari na ku-internalize ni vipi uliingia huku. Hii itasaidia wewe kujiondoa kwenye visababishi. Mfano: rafiki, picha za ngono, sehemu unayoishi nk.
2: Zingatia misingi ya dini yako. Hii ina maana usifanye kufuata mambo ya dini kama mkumbo. Ongea na roho wako juu ya umuhimu wa Dini na Muumba kwenye maisha yako. Na je ufanyayo yanaendana?
Hii itakupa nguvu ya kuikataa hali husika pia.
3: Tafuta shughuli mbadala mara upatapo ushawishi au kabla. Hii ni kujijengea uwajibikaji zaidi na kutokuwa na muda mwingi wa ziada. Pia matumixi ya nguvu na akili yako. Hii itakuwa ni chanzo cha furaha yako bila kuvunja taratibu za jamii, dini na Muumba. Mfano: kusikiliza mawaidha, kusoma vitabu vya aina yoyote vivavyokuvutia, kufanya mazoezi, kufanya YOGA.
4: Kujiunga kwenye vipindi au vikundi vya kijamii na kidini vyenye dhamira njema. Hii itakusaidia kuwa busy na mambo ya kijamii na kidini. Hapa utajifunza mengi pia kukuweka busy.
5: Pata mwanasaikolojia wa afya na wa dini. Hawa wataimarisha afya yako ya mwili na roho kwenye kukuimarisha kukwepa vishawishi.
6: Tambua maisha si leo tu, hivyo elekeza pesa zako kwenye shughuli za maendeleo yako ya leo na kesho pia saidia wahitaji mbalimbali. Hii itapunguza kuona hauna wajibu wowote na matumizi yanayohitaji pesa zako (wekeza pesa zako mfano: kwenye mifuko ya hifadhi).
7: Tathmini sababu ya uumbaji wako na thamani unaoupatia. Je ndo fadhila kwa Muumba wako?
8: Tafakari kwa watu wengine wenye kipato. Je hakuna wanaokuzidi kipato? Je nidhamu yao iko kama yako? Je wewe unashindwa nini kudhibiti mwili wako?
NB: FANYA MAAMUZI SAHIHI NA UTAJIONDOA KWENYE UFUNGWA HUU ILI ULETE AMANI NA FURAHA YA KWELI NDANI YA MAISHA YAKO.