Nimepoteza Kaka Yangu Niliyekuwa Namfuatia

Kazi ya Mungu haina makosa,

Mazishi ni huko huko kijijini na shughuli zimeshaanza, mwili wake utazikwa kwesho. Mimi sitahudhuruia kutokana na ufinyu wa muda, ila nitakwenda kuweka msalaba kwenye kaburi lake mwezi kesho.
Nenda ukamzike mwamba ufinyu wa muda sio sababu,labda useme uko abroad na huna nauli
 
Hapana, kwenye huu uzi kuna watu wanaangalia jambo dogo sana la kuhusu heshima ya marehemu ambaye ameshatangulia mbele ya haki na kuacha jambo kubwa linalohusu interventions kwenye maisha ya ndugu zetu. Kuficha sehemu ya ukweli hakutasaidia kupeleka ujumbe wa umuhimu wa interventions kwenye maisha ya ndugu zetu wanaopotoka hasa kwa ulevi.
 
Ni kweli alikuwa alchoholic,

Hilo ndilo tulilochelewa; Alchoholism inatibiwa kwa counseling, jambo ambalo hatukulifanya effectively. Tulimwacha ajiamulie maisha yake kuhusu pombe na ndiyo maana sasa hivi ninaomboleza hapa.



Pole , tuendelee kumuombea pumziko jema.🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Nimekuelewa
 
Nenda ukamzike mwamba ufinyu wa muda sio sababu,labda useme uko abroad na huna nauli
Huu siyo ushauri kudhani kuwa ninakosa nauli ya kwenda kumzika ndugu ninayelelama hapa kumpoteza bila kujua kuwa tayari nimeshepeleka gharama zote za kumfanyia mazishi ya heshima.

Hata hivyo asante kwa ushauri
 
Huu siyo ushauri kudhani kuwa ninakosa nauli ya kwenda kumzika ndugu ninayelelama hapa kumpoteza bila kujua kuwa tayari nimeshepeleka gharama zote za kumfanyia mazishi ya heshima.

Hata hivyo asante kwa ushauri
Uwepo wako ni muhimu,kila mtu akituma hela mwamba atajizika mwenyewe?
 
Pole sana mkuu. Mungu akupe ujasiri wa kukabiliana na huu msiba.
 
Kama huna nauli ndio tutakuelewa,ila kama ipo we nenda tu mzee mwenzangu
Ngoja nikujibu vizuri kwa vile umekazia sana hili na ninalielewa. Siwezi kuruhusiwa kuondoka kazini kwenda kuzika ndugu kwa muda wa ziadi ya siku moja, labda baba na mama na pia ni kwa utaratibu maalumu kwa vile wenzetu mazishi siyo jambo la haraka na huhairisha kufanya mazishi kwa kutunza mwili hadi muda ambo ni convenient.
 
Jaza emergency keave,Achana na tamaduni za hao wajinga,tunakusubiri msibani
 
Mwambie kwa ufupi upo nje ya mipaka.
Ni ngumu kupata tuhusa kuzika kaka, dada au rafiki.

Pole sana. Apumzike kwa amani.
 
Jaza emergency keave,Achana na tamaduni za hao wajinga,tunakusubiri msibani
Hapana; ni ngumu sana kufanya hivyo kwenye taasisi yetu ambayo ni taasisi ya serikali. Ni tofauti na makampuni binafsi ambayo yanaweza kukuruhusu kufanya kazi remote ukiwa nje ya nchi.
 
Mungu amehusikaje hapo mkuu?

Kwa hiyo Mungu ndiye aliyekuwa anamwongoza akanywe pombe ili afe

Wakati wewe mwenyewe unasema kaka yako alikuwa mlevi

Kifo chake kajitakia mwenyewe usimsingizie Mungu
Lolote lifanyikalo duniani liko chini ya control ya Mungu. Ndivyo tunavyoamini.
 
Lolote lifanyikalo duniani liko chini ya control ya Mungu. Ndivyo tunavyoamini.
Mzee kilichomua kaka yako ni pombe Mungu hajamcontrol awe mlevi.

Mungu mwenyewe amekataza ulevi halafu tena huyohuyo amcontrol awe mlevi afe? Ina make sense kweli?

Bro wako hakutii sheria ya Mungu aliyokataza ulevi.

Maandiko yanasema kile apandacho mtu lazima avune

Anyway pole kwa kumpoteza bro
 
Nakunukuu

""Ukiwa na ndugu mwenye tabia za marehemu kaka yangu, jitahidi uwe unatenga muda wa kumshauri mara kwa mara kuhusu pombe asitumbukie kwenye janga lililotufika sisi."""

pole kaka pole Sanaaaaa

Mimi na mdogo angu tumepishana tumboni miezi sita..

Watoto wote walio lala kwenye tumbo la mama angu wote Wana ELIMU za juu na Wana Maisha yao..

Mimi tangia mdogo nilikataaga kuja kua mtu wa ovyo ovyo..

mama angu juzi juzi alinambia mwanangu mwangalie mdogo ako un wonderful enough anapiga Sana tungi na kawa addicted kweli kweli sijui namsaidia vipi..

pole kaka kwa kumpoteza kaka tunapata faraja kupitia UFUNUO 14:13
 
Mwahi mdogo wako mapema usijeliia kama mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…