Nimepoteza marafiki kisa mke wangu!

Tatizo linakuja hapo, vijana wengi wakioa wanafikiri maisha ya usela bado yapo
Ukioa mambo mengi yanabadilika hata marafiki wanapungua automatically
Unakuwa na majukumu mengi na mke ndio anakuwa badala yao washikaji
Tafuta mda nenda nae outing, hata jioni baada ya kazi ukila tembeeni pamoja au unaona nishai

Marafiki wengi ni utoto pambana na maisha yako umekuwa sasa
Watoto wanakuhitaji zaidi ya hao marafiki
Kwa ushauri na misaada hata simu zinatosha
Familia pia muhimu ila afanye kila kitu kwa familia asiguse kabisa hiyo sekta tena usikubali kuwa dhalili kiasi hicho
Kukuachanisha na familia yako basi atakuwa mchawi huyo
Marafiki sawa ila sio familia
 
Kuna wanaume wakioa wanabadilika mpaka Kwa ndugu zao, utashangaa mpaka mawasiliano na Kwao anayakata,

Ndo maana kabla ya kuoa unashauriwa kama ulikuwa hujamaliza kuwasomesha wadogo zako umalize kwanza maana wanawake si watu wazuri sana

Kaa na mkeo umshauri, asipokuelewa mwitie ndugu zake na zako mumkalishe kikao
 
Mkeo anataka apandishwe cheo. Tena deal na rafiki zake.
 
nikuulize mkuu kwahiyo yeye mwanamke kuleta marafiki zake na ndugu zake ni sawa?
Ndugu na jamaa wa pande zote mbili wanapaswa kufika kwenu nanyi pia mnapaswa kufika kwao
Hii ni muhimu kwa watoto na nyie wanafamilia ili kujua mji na maisha yanaenda vipi
 
Sasa kama mke atakataa hadi ndugu zako hapo si unaona shida tayari ndani ya nyumba
Ndicho anachopitia mleta mada.
Katika haya maisha hususan ya ndoa kuelekezana na kufafanuliana mambo ni jambo la muhimu.
Mkeo hawaelewi jamaa zako inabidi akuite mkae akufafanulie kuwa "mumewangu kuna moja mbili tatu" mtazungumza na kuyaweka mambo vizuri zaidi.
Sio unaweka ban from no where,busara inahitajika itumike.
 
Mimi kabla sijaoa nilimuweka mkewangu wazi.
Ndugu/jamaa zangu ni wangu na ni juu yangu,yeye ashughulike na mimi na ndoa yetu,mengine hayamuhusu.
Hawezi achape lapa kabla ya ndoa.
Tusileteane upuuzi wewe umekuja ukubwani unajua hao watu nimetoka nao wapi!??
Nimekuoa leo na kesho umezingua tumepeana talaka ushanigombanisha na ndugu/jamaa mie nakua mgeni wa nani!??
 
Aisee, sometimes unaweza dhani ni Kwa heri kumbe mkeo kichwani kwake kapiga hesabu kuwa marafiki zako labda wanaweza kukuunganisha na michepuko pembeni kumbe ni hofu yake tu, nadhani umeingia kwenye mfumo wake badala ya mfumo wako, anyways Kila mtu na situation zake lakini binafsi najua rafiki zangu Fulani Fulani wapo tulipotoka na Kwa namna gani tumevuka vikwazo vingi sana.
 
Af kuna mimi ambaye ikifika Ijumaa namkumbusha my partner kwenda kunywa beer, kucheza pool, kuangalia mpira na kutizama mawowowo mengine duniani huko.
Ili nipate muda wa kupiga umbea na kusengenya na wambea wenzangu na kuingia insta kuona magauni ya kina Giggy.
 
Mueleze ukinikataza kuwa na marafiki zangu ntawatafuta rafiki zako ndio wawe rafiki zangu… then msikilize anasemaje!! Tafuta kweli namba zao anza ukaribu nao nayeye ajue kuwa kweli umeaminia upande wa rafiki zake kuwa rafiki zako
 
Nimekua muoga sana kushauri mambo ya watu hasahasa mahusiano,kaa zungumza na mkeo haya uliyoaandika hapa mwambie kwa upole atakuelewa tu
 
Familia yako ndio marafiki wa karibu na wa kweli..ni kitu cha kuzingatia
Familia yake ipi??Mke ambaye mnaweza achana wakati wowote?
Hivi haya maisha katika hii Dunia bila marafiki na ndugu na jama utafika wapi??
Family inaweza kuwa mhumi ila marafiki na ndugu ni muhimu zaidi,hata ikitokea ww na huyo Mkeo mmefariki ni hao hao ndugu ndio watawasaidia wanao.

Sasa kama nduguzo wananshindwa hata kuja kwako,siku ukifa ni nani atawasaidia hao wanao.
 
Nimekua muoga sana kushauri mambo ya watu hasahasa mahusiano,kaa zungumza na mkeo haya uliyoaandika hapa mwambie kwa upole atakuelewa tu
Hadi ameleta nae humu maana yake amisha zungumz mpaka ameshindwa afanyaje,ndio maana anataka mawazo mbadala sasa ww unasema azungumze.
 
Acha uongo mwanamke anaona mbali wapi,utafanikiwaje bila marafiki wala ndugu katika Dunia hiii??
Ni mara πŸ’― angekuwa anakataa marafiki ndugu anawakubali basi tungesema ameona hao marafiki ni chenga-sasa yy hataki wote.
 
Huyo jamaa sio wewe Mkuu ? πŸ€£πŸ˜€πŸ€£ au wewe ni Kataa ndoa
 
Mkuu, wanawake tuko hivyo japo mkeo amezidi. Kinachoumiza ni kwamba mkiwa na hao marafiki zenu mnatusahau kwa muda, kwa jinsi tunavyopenda attention hilo linaumiza.

Binafsi napendelea zaidi marafiki wa mpenzi/mume wakutane nyumbani. Tena wakija kwetu nafurahi zaidi na kuwapikia nitawapikia chakula kizuri kwa kuwa nina amani mpenzi/mume wangu yuko nyumbani na sio nje ambako nitapata mashaka.

Ninachoweza kukushauri ni kuongea na mkeo, mimi naamini katika uwazi na maongezi katika mahusiano/ndoa.
Mwambie jinsi gani hilo suala linakuumiza na linavyokukosesha furaha kuona unatengwa na marafiki.
Naamini mkeo anakupenda hivyo atakusikiliza.
 
Kama marafiki zako ni watu wa starehe na kukuingiza chaka hapo mkeo yupo sahihi

Lakini

Kama ni marafiki wa kawaida ambao mnashauriana katika mambo mazuri mkeo hayupo sahihi

Kitendo cha mkeo kukataa ndugu zako tu wakati wake wanakaribishwa nyumbani ni ubinafsi mkubwa anao,,,na kupitia kitendo hiki naamini hata kukataa marafiki zako ni ubinafsi pia

Ushauri kwa wanaume,huyu mwanamke hakuanza jambo hili ghafla bali alianza kumtekenya mwamba kidogo mwisho akaingia laini,kwahiyo mwamba amejikuta yupo chini ya mwanamke,,,kwahiyo tokea awali stand kwa mwanaume maadam unasimamia jambo sahihi

Ntawapa mfano mmoja,,,nilioa single maza mwenye binti wa kike,kwakawaida katika meza ya chakula nilizoea kukaa kile kiti kama cha mwenyekiti nadhan mnakijua kipo kona halafu peke yake

Sasa binti alivyokuja rasmi kuishi nasi smtm akawa anakaa katika kiti nilichokizoea,nikawa namwambia mwanangu hama hapa kaa pale,,kumbe wife alikuwa anaona namnyanyasa mwanae,,ndo akaniambia kuwa anaona kama namnyanyasa mwanae,,nikwambia kama kwa ishu hii unaona namnyanyasa basi mpeleke kwa baba yake,,pale pale akaomba yaishe na kuomba radhi,so kama nisingekaza kesho lingezuka lingine

Ajabu nyingine ikatokea binafsi napenda watoto sana,basi nikawa smtm kama siko bize namfuata mtoto huyu shule wkt tunarudi home tunaenda beach nakaa nae kidogo afurahi kisha tunarudi,,ukaja ujinga wa wanaume ambao wanatembea na binti zao wa kambo,sasa inaelekea kupitia magroup yao ya whats up wakatiana uwoga nahisi akaanza kuwa na hofu kwa kitendo changu cha smtm kupita nae bichi,,nikaona isiwe tabu nikaona niache tu

Sasa awali aliona namnyanyasa binti yake hlf baadae kumwonyesha mapenzi mtoto anaona nina langu jambo

Kikubwa mwanaume kuwa na msimamo daima, nyumba ipo chini ya maamuzi ya mwanaume
 
Daaah yani nyumbani kwako wanaokuja ni marafiki zake na ndugu zake yy TU. Kuna MZEE mmoja aliwahi kusema ukienda kwa ndugu yako ukikuta ndugu w mke ni wengi ujue mume ndondocha.




KAZI ni kipimo cha UTU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…