Nimepoteza mimba 10 kwa tatizo hili

Nimepoteza mimba 10 kwa tatizo hili

Wakuu nimekuja kwenu kwa mara nyingine tena naombeni msaada wenu.Mwaka 2022 nilileta uzi kuhusu watoto wangu wanaozaliwa na kufa kabla au baada ya kuzaliwa. Sasa mwaka huu tena 2024 nimepoteza watoto wengine wawili kabla ya kuzaliwa wakiwa tumboni.

Baada ya tukio hilo ikabidi kutafuta wazee kuwaomba ushauri.Kuna sehemu huku mkoani nikapelekwa kwa mama mmoja akaniangalia akasema nina likango kwa jina maarufu.

Hii ni kama bawasiri ila sio bawasiri na kazi yake ni moja tu kumaliza watoto. Huota katikati ya tundu la haja kubwa. Nikaambiwa inatakiwa nipate tiba ili niweze kuitwa baba.

Na katika mimba hizo 10 zimepatikana kwa kipindi cha miaka hii miaka4 kwa wanawake tofautitofauti. Nimekuja kwenu kuomba ushauri kwa mwenye experience na hii kitu aweze kunisaidia jinsi gani nitaiondoa katika mwili wangu.Asanteni 🙏..

Hii picha nilipiga mwaka 2021 ilivyonianza hilo tatizo la likango.
Pole sana.Mimi siyo Docta.Ila nadhani kuna upungufu wa aina flan ya madini.Ungekuwa ni mnyama ningesema baba yako na mama yako walikuwa ni mtu na dada ake.au ndugu wa karibu sana kutoka kwenye uzao mmoja
 
huyo mama ni daktari?
aliionaje hiyo bawasiri huko nyuma?

na mbona kuna watu wengi tu wana bawasiri na wana watoto na wajukuu?

wewe pamoja na mwenza wako unekusudia kuzaa nae mtoto muende kwa pamoja kumuona daktari wa uzazi,
na kisha tuanzie hapo kufuatilia kitaalam, nini hasa sababu ya songombingo hiyo?

na kwa Neema na Baraka za Mungu atakujaalia watoto na wajukuu.
Kua muaminifu, hii kuchovya chovya kila mahali sio ustaarabu 🐒
 
Dkt Colman ndo suluhisho.
Anapatikana Hosp Muhimbili ama Private pale Sinitaz Kwa wahindi pale Mikocheni
Huyo sio daktari wa wanawake?? Jamaa ni mwanaume, anaamini mambo ya kishirikina kuwa mimba za wanawake wake zinatoka kwasababu yeye anahiyo ishu. Jambo ambalo hata bila utaalamu ni wazi kuwa halina ukweli.
 
Pole sana.Mimi siyo Docta.Ila nadhani kuna upungufu wa aina flan ya madini.Ungekuwa ni mnyama ningesema baba yako na mama yako walikuwa ni mtu na dada ake.au ndugu wa karibu sana kutoka kwenye uzao mmoja
Asante kwa ushauri mkuu.
 
Back
Top Bottom