Tangu mwaka uanze nahisi huu ni uzi wako wa maana kuliko zote.
Anyway binafsi jpm nillikuwa namkubali kawaida tu hasa nikiwa sehemu ya changanyikeni kama humu, nilikuwa simchukii kama wengine, kuna vitu alikuwa akifanya nasema huyu kweli rais hata kama sisem ila moyoni nasema hili jembe.
Siku niliposikia habari za kifo chake trh 9 nilisikia maumivu ambayo sikujua yametoka wapi.
Miliogopa hata kumwambia mtu yeyote maana alienihakikishia kafa alinitaka nifunge mdomo wangu.
Nilikuwa nikiingia humu nakuta watu wanachangia nyuzi kibao eti jpm yupo wapi na mimi najilazimisha kuchangia as if sijui kinachoendekea.
Pili moyo haukuamini nilichoambiwa nikawa akisemea ' huyu mbwa nae mwongo jpm atakufaje kizembe hivi?
Siku moja nikataka kumwambia mama yangu moyo ukasema hapana yupo hai yule fala mzushi.
Trh 17 usiku nikaota eti kafa nikastuka usingizini nikajisemea hapana ni nawazo yaliyo kichwani mwangu coz nishapewa hiyo habari wiki moja kabla.
Niliamka nikapiga magoti nikasali mikasema hii ndoto isiwe kweli, nikaingia jf nikakuta mtu kapost eti kwa nini wasitangaze tu rais kashakufa kha! Ndo niliamini yale maneno.
Baada ya kutangaza nilipata maumivu ambayo sikujua yametoka wapi, maana niliona Tanzania ambayo jpm alikuwa akiitengeneza ikiyeyuka.
Niliona ujinga ukirudi kwa kasi, wizi, miradi yake ikifa, nidham ya watumishi ikirudi 0, ufisadi nje nje , majambazi wakirudi kwa kazi, unyanyasaji wa wanyonge, viongozi kula mishahara ya bure,kupewa kazi kwa kujuana, vyeti feki,
Nikaona lile genge sugu la majambazi wanaotesa nchi wakifurahia kifo chake, nililia sana nikasema Mungu alitupa malaika ila wengi tulichukulia poa.
Huko ulipo jpm ulale salama, hakuna siku imepita bila kukukumbuka. Binafsi nimekumiss sana.
Rip jpm.