Umasikini ni mbaya sana maana hata watu wengi wenye roho mbaya ni wale masikini japo hata wenye uwezo wapo wenye roho mbaya,
Nimegundua kulikuwa na watu waliokuwa wakifurahia dhuluma kwa wengine kama kuuawa,kutekwa,kuteswa,kuporwa fedha na mali zao kwa sababu tu waliona umasikini wao umesababishwa na hao wachache waliofanikiwa hivyo walifurahi sana kuteswa kwa hao watu. Walifurahia pia hata baadhi ya watumishi kudhalilishwa na viongozi wachache waliokuwa wakimtumikia shetani.
Hayo yote yalisababishwa na roho mbaya ya umasikini lakini sasa baada ya mambo kubadilika kuna watu wanaumia kwanini sasa viongozi hawafanyi dhuluma na kudhalilisha watu.
Hawa ndio wale wanaolaumu na kuubeza utawala wa sasa kila kukicha.