Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Accusations zisizo na vithibitisho zipo tokea enzi za kambarage, unfortunately hazijawahi kufuta kumbukumbu nzuri walonazo watu kwa viongozi majemedari.
So, itabidi mvumilie sifa watakazomwagiwa mpaka mtakapokufa.
Sifa za kulea Majangili akina Sabaya ?
Kwa hili atakumbukwa sana
 
punguza chuki mkuu, yesu pia alikua na wanafunzi wao je, uovu wao ulifuta credibility yake?
Unataka Kumfananisha Magufuli na Yesu ?
Acha Kumfananisha Mwokozi wa Ulimwengu na Binadamu
 
Umasikini ni mbaya sana maana hata watu wengi wenye roho mbaya ni wale masikini japo hata wenye uwezo wapo wenye roho mbaya,
Nimegundua kulikuwa na watu waliokuwa wakifurahia dhuluma kwa wengine kama kuuawa,kutekwa,kuteswa,kuporwa fedha na mali zao kwa sababu tu waliona umasikini wao umesababishwa na hao wachache waliofanikiwa hivyo walifurahi sana kuteswa kwa hao watu. Walifurahia pia hata baadhi ya watumishi kudhalilishwa na viongozi wachache waliokuwa wakimtumikia shetani.
Hayo yote yalisababishwa na roho mbaya ya umasikini lakini sasa baada ya mambo kubadilika kuna watu wanaumia kwanini sasa viongozi hawafanyi dhuluma na kudhalilisha watu.
Hawa ndio wale wanaolaumu na kuubeza utawala wa sasa kila kukicha.
 
Ulishuhudia Kupotezwa Ben Saanane, Kutekwa Kwa Roma Mkatoliki, Kupigwa risasi Akwilina, uchaguzi Mkuu kuharibiwa kabisa, Kuibuka Kwa Magenge ya wahuni Kama vile Sabaya, Musiba, Bashite, Mashimo n.k
kumchukia mtu ni mtizamo binafsi hilo sikuingilii bt nataka tu unambie ni rais gani tanzania katika utawala wake watu hawakutekwa, kupigwa risasi, uchaguzi kuharibiwa na nk... ?
 
Sahihi kabisa, Ma Sadist bado tunao wengi sana
 
Kwangu mimi JPM JPM alikuwa rais muuaji, mwenye chuki kali sana kwa wanamkosoa na kumpinga, mbinafsi aliyepitiliza kiwango cha kawaida na mungu mtu aliyependa kusujudiwa mpaka na nzi. MUNGU AMEWATENDEA HAKI WATANZANIA.
haya nitajie rais wa tanzania ambae hajaua katika utawala wake, ambae hajawatesa wanaomkosoa ili nijue kama husumbuliwi na chuki binafsi
 
kumchukia mtu ni mtizamo binafsi hilo sikuingilii bt nataka tu unambie ni rais gani tanzania katika utawala wake watu hawakutekwa, kupigwa risasi, uchaguzi kuharibiwa na nk... ?
Huyu Ibilisi wenu alizidi
 
Ulishuhudia Kupotezwa Ben Saanane, Kutekwa Kwa Roma Mkatoliki, Kupigwa risasi Akwilina, uchaguzi Mkuu kuharibiwa kabisa, Kuibuka Kwa Magenge ya wahuni Kama vile Sabaya, Musiba, Bashite, Mashimo n.k
Naam ulishuudia yote ayo ata kuuwawa kwa Chacha Wangwe nilishuhudia pia.
 
Mliwahi kumuuliza Mbowe kuhusu kifo cha Chacha Wangwe. Je ulishawahi kungalia upande wa pili wa shilling? Siku mkija kuujua ukweli mtashangaa
Kama kweli Mbowe alimuua Chacha Wangwe basi lazima alikuwa na ushirika na serikali na CCM. Hakuna namna angeachwa hivi hivi mpaka leo wanahangaika naye kwa kesi ya ugaidi. Sio Tanzania hii tunayoijua.

Halafu, kwa mshangao zaidi, dereva aliyehusika kwenye ajali yenyewe akaachiwa kwa msamaha wa Rais baada ya muda mfupi wa kuwa jela! WTH!
 
Back
Top Bottom