Hivi kuwa na wivu wa kike kwa mwanamke ni tusi? Nikimwambia Regia, ambaye ni mwanamke kuwa ana wivu wa kike ni tusi kwake? Ebo!!
Hivi kuwa na wivu wa kike kwa mwanamke ni tusi? Nikimwambia Regia, ambaye ni mwanamke kuwa ana wivu wa kike ni tusi kwake? Ebo!!
Sure...au kama atakuwa hajapewa 'thalatha-twalaka', maana yataka moyo wa JIWE kuishi kwenye ndoa hii!...si ndio eeh?Kama atakuwa ameoa. Si ndio?
Mkuu nadhani anamaanisha kurudi hapa jamvini na si kukimbia kutoka Kilombero....TUMSIMHUKUMU BALI TUMSAIDIE na kumpa moyo ajipange upya
Kwa Muktadha huu, hilo linaweza kuwa tusi...muulize Kiranga hommie...
NN amevuka lengo...Hata Diana anamjua achilia mbali Viki.
Sure...au kama atakuwa hajapewa 'thalatha-twalaka', maana yataka moyo wa JIWE kuishi kwenye ndoa hii!
Ningeweza kumuuliza lakini naogopa anaweza kunitusi lol
jamani eeh mnadhani ni baa gani itafaa kumkaribisha dada regia....?
mi nadhani tungelijadili hili....
hazikutosha?????angeamua kukata rufaa?karibu sana dada regia, na hongera kwa mapambano uliyoyafanya. Naamini umeonyesha unaweza ila kura hazikutosha, kwa hiyo bila shaka utajipanga upya na vizuri zaidi kwa mapambano yajayo. Keep it up.
Kiranga mtu wa utani na mizaha kwa ratli nyingi tu, ila matusi anayaepuka, badili yake anashusha bashasha za kirafiki tu.
Watu hawamuelewi tu.
In the third person too, don't think I don't know.
Aliyewatusi binadamu wa kike wote duniani kwamba ni viumbe wenye wivu inherently.
Ndivyo alivyosema hivyo?
Sawa sawa,
Lakini kina Simon Mbilinyi walivyoenda kupumzika Bahamas wakati constituencies zao zinaishi maisha ya dola moja kwa siku huko tuliwaita mafisadi, Regia leo anapata pass kwa sababu gani? Kwa sababu CHADEMA ?
Kama unajua kwamba kulitumikia taifa ni zaidi ya siasa ungeshangaa Regia kuwakacha wananchi wa Kilombero wiki moja tu baada ya uchaguzi.
Siwezi kujua mipango ya Regia, kwa sababu so far anaonekana hana mipango. Mtu mwenye mipango anaweza kutoa vipost kama vya Regia ?
Anasubiri huruma za party bigwigs wampe kiti maalum tu bungeni, we unafikiri kurudi haraka mjini kuna sababu ndogo ?
Jamani on a serious note, naomba na mi niungane na waungwana wengine kukmaribisha tena hapa jamvini Mh Regia Mtema, nimpe pole na pongezi kwa kupambana vilivyo lakini zaidi kwa kuonyesha kuwa anaweza kuchallenge the status quo......
Karibu sana
By the way NN FYI calabash pale yupo FLORA, muulize big braza ODM akupe 'habari yake'
NN amevuka lengo...Hata Diana anamjua achilia mbali Viki.
Regia hajasema kaja kutafuta mawakili, kasema karudi kutoka Kilombero. Unafahamu maana ya "kurudi" ? Mtu anarudi kwenye base yake, mtu anarudi nyumbani kwake. Inaonekana Regia anaona Kilombero si base wala makazi yake, ndiyo maana "anarudi kutoka Kilombero". Ama sivyo angetuambia "nimekuja mjini" kama kweli angekuwa amefanya Kilombero base yake.
Hili ni tatizo kubwa tunalo, wabunge wetu na wadau wengine wanaotaka kuwakilisha wananchi wanataka kulundikana mijini, watakuwa vipi karibu na wananchi wanaotaka kuwaomba kura? Hawa kweli wanataka kuwakilisha matakwa ya wananchi au wanataka ukubwa tu ?
Regia hajaenda Bahamas na Regia si fisadi. Mafisadi ni wabadhirifu wa fedha na mali na rasilimali za umma. Regia hayuko kwenye hiyo nafasi ya kuweza kuwa fisadi.
Regia kawakacha wana Kilombero? Ndivyo walivyokwambia hivyo au tena unasadiki?
Umejawa namadharau kupita kiasi!!!! Hujui mipango yake lakini unatoa hukumu kulingana na post zake za hapa. Au umemwuliza ukaongea naye kwa mapana na marefu kuhusu hiyo mipango yake na ukaona kuwa hana mipango?
Ingekuwa hivyo wala hata asingethubutu kuweka jina lake na familia yake kwenye mstari wa mbele ambako kuna kila aina ya visanga vikiwemo kejeli na dharau toka kwa watu kama wewe. Kajitosa, kagombea na haikwenda kama ilivyotarajiriwa kutokana na sababu mbalimbali za dhuluma halafu wewe unadiriki kusema anasubiri huruma za grand poobahs wa CHADEMA. Hapa mwombe radhi.