Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Status
Not open for further replies.
Hivi kuwa na wivu wa kike kwa mwanamke ni tusi? Nikimwambia Regia, ambaye ni mwanamke kuwa ana wivu wa kike ni tusi kwake? Ebo!!

Of course prejudice yako inakupofusha huwezi hata kuona wivu hauna uhusiano na jinsia.

"Wivu wa kike" hauna tofauti na "ujinga wa watu weusi" inawezekana kwako si tusi kuambiwa kwamba watu weusi wana ujinga wao maalum unaotokana na weusi wao, lakini wengine tunaona tusi.
 
Hivi kuwa na wivu wa kike kwa mwanamke ni tusi? Nikimwambia Regia, ambaye ni mwanamke kuwa ana wivu wa kike ni tusi kwake? Ebo!!

Kwa Muktadha huu, hilo linaweza kuwa tusi...muulize Kiranga hommie...
 
Sure...au kama atakuwa hajapewa 'thalatha-twalaka', maana yataka moyo wa JIWE kuishi kwenye ndoa hii!

Taratibu kiongozi. Hii sentensi yako yaweza geuzwa na kuitwa tusi...
 
Ningeweza kumuuliza lakini naogopa anaweza kunitusi lol

Kiranga mtu wa utani na mizaha kwa ratli nyingi tu, ila matusi anayaepuka, badili yake anashusha bashasha za kirafiki tu.

Watu hawamuelewi tu.

In the third person too, don't think I don't know.
 
karibu sana dada regia, na hongera kwa mapambano uliyoyafanya. Naamini umeonyesha unaweza ila kura hazikutosha, kwa hiyo bila shaka utajipanga upya na vizuri zaidi kwa mapambano yajayo. Keep it up.
hazikutosha?????angeamua kukata rufaa?
 
Kiranga mtu wa utani na mizaha kwa ratli nyingi tu, ila matusi anayaepuka, badili yake anashusha bashasha za kirafiki tu.

Watu hawamuelewi tu.

In the third person too, don't think I don't know.

Aha! Kumbe muda wote ulikuwa wamfanyia mzaha Da Regia? Haya propose basi tukutane wapi tumpe michakato ya nini cha kufanya hapo baadae. Ofkozi bia na ndugu zake vikiwa mezani.
 
Aliyewatusi binadamu wa kike wote duniani kwamba ni viumbe wenye wivu inherently.

Kisha anafuata anayemtusi mgombea ubunge (na mshindi asiyetangazwa na Tume) kwa kuona post zake ni "vipost" tu (inherently as well).

Next....
 
Karibu sana Regia pole sana na mihangaiko katika harakati za kuisaidia jamii tulikumiss pia tunafurahi kukuona umerudi salama kabisa .
Pia pongezi kwa juhudi zako zote katika kulipigania taifa letu.
Na imani nitakuwa wa kwanza kama si wa Mwisho kuonana na wewe
Wish best of luck in your life:tea::A S-heart-2:
 
Ndivyo alivyosema hivyo?

Kiranga una kiranga kweli msome hapa...........Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.
 
Sawa sawa,

Lakini kina Simon Mbilinyi walivyoenda kupumzika Bahamas wakati constituencies zao zinaishi maisha ya dola moja kwa siku huko tuliwaita mafisadi, Regia leo anapata pass kwa sababu gani? Kwa sababu CHADEMA ?

Regia hajaenda Bahamas na Regia si fisadi. Mafisadi ni wabadhirifu wa fedha na mali na rasilimali za umma. Regia hayuko kwenye hiyo nafasi ya kuweza kuwa fisadi.

Kama unajua kwamba kulitumikia taifa ni zaidi ya siasa ungeshangaa Regia kuwakacha wananchi wa Kilombero wiki moja tu baada ya uchaguzi.

Regia kawakacha wana Kilombero? Ndivyo walivyokwambia hivyo au tena unasadiki?

Siwezi kujua mipango ya Regia, kwa sababu so far anaonekana hana mipango. Mtu mwenye mipango anaweza kutoa vipost kama vya Regia ?

Umejawa namadharau kupita kiasi!!!! Hujui mipango yake lakini unatoa hukumu kulingana na post zake za hapa. Au umemwuliza ukaongea naye kwa mapana na marefu kuhusu hiyo mipango yake na ukaona kuwa hana mipango?

Anasubiri huruma za party bigwigs wampe kiti maalum tu bungeni, we unafikiri kurudi haraka mjini kuna sababu ndogo ?

Ingekuwa hivyo wala hata asingethubutu kuweka jina lake na familia yake kwenye mstari wa mbele ambako kuna kila aina ya visanga vikiwemo kejeli na dharau toka kwa watu kama wewe. Kajitosa, kagombea na haikwenda kama ilivyotarajiriwa kutokana na sababu mbalimbali za dhuluma halafu wewe unadiriki kusema anasubiri huruma za grand poobahs wa CHADEMA. Hapa mwombe radhi.
 
Dada Regia ..................Hongera sana mpambanaji! Sikupi pole kwani ulijua unachokiiingia na hatari zake ! Nakupa hongera kwani wewe na wengine wote kama wewe mmeshinda! mmeshinda kwa maana ya kuwa sasa Tanzania siyo ile ya majuzi na juzi! Hongereni sana wapiganaji wote!

Pili niungane na Kiranga na rai yake kuhusu wewe "kurudi" mjini! dada Regia na wenzio wote................kazi ndo kwaanza imeanza na huko mbele kuna kazi kubwa zaidi..................... kuwa mmejitolea na kweli mmefika hapo mlipo si busara kuishia hapo na kubaki hapo..............songeni mbele! Mungu awape nguvu na awabariki!
 
Jamani on a serious note, naomba na mi niungane na waungwana wengine kukmaribisha tena hapa jamvini Mh Regia Mtema, nimpe pole na pongezi kwa kupambana vilivyo lakini zaidi kwa kuonyesha kuwa anaweza kuchallenge the status quo......

Karibu sana

By the way NN FYI calabash pale yupo FLORA, muulize big braza ODM akupe 'habari yake'

NN amevuka lengo...Hata Diana anamjua achilia mbali Viki.

Imebidi niwatoroke hawa vya mdoli maana hii mada imenipandisha mzuka kiaina.....karibuni supu
 
Regia hajasema kaja kutafuta mawakili, kasema karudi kutoka Kilombero. Unafahamu maana ya "kurudi" ? Mtu anarudi kwenye base yake, mtu anarudi nyumbani kwake. Inaonekana Regia anaona Kilombero si base wala makazi yake, ndiyo maana "anarudi kutoka Kilombero". Ama sivyo angetuambia "nimekuja mjini" kama kweli angekuwa amefanya Kilombero base yake.

Hili ni tatizo kubwa tunalo, wabunge wetu na wadau wengine wanaotaka kuwakilisha wananchi wanataka kulundikana mijini, watakuwa vipi karibu na wananchi wanaotaka kuwaomba kura? Hawa kweli wanataka kuwakilisha matakwa ya wananchi au wanataka ukubwa tu ?

Kiranga mimi nimeelewa tofauti kabisa na wewe! Regia alikuwa amehama jamvini hapa, sasa amerudi jamvini. Hajasema yuko Dar au wapi, pengine yupo huko huko Kilombero na sasa amepata nafasi ya kurudi hapa JF! Kwa nini unafikiri hayupo Kilombero! You are prejudiced my friend about what goes on in the constituencies. Actually wale wa CCM ndio watalii katika majimbo yao!
 
Regia hajaenda Bahamas na Regia si fisadi. Mafisadi ni wabadhirifu wa fedha na mali na rasilimali za umma. Regia hayuko kwenye hiyo nafasi ya kuweza kuwa fisadi.

Regia kawakacha wana Kilombero? Ndivyo walivyokwambia hivyo au tena unasadiki?

Umejawa namadharau kupita kiasi!!!! Hujui mipango yake lakini unatoa hukumu kulingana na post zake za hapa. Au umemwuliza ukaongea naye kwa mapana na marefu kuhusu hiyo mipango yake na ukaona kuwa hana mipango?

Ingekuwa hivyo wala hata asingethubutu kuweka jina lake na familia yake kwenye mstari wa mbele ambako kuna kila aina ya visanga vikiwemo kejeli na dharau toka kwa watu kama wewe. Kajitosa, kagombea na haikwenda kama ilivyotarajiriwa kutokana na sababu mbalimbali za dhuluma halafu wewe unadiriki kusema anasubiri huruma za grand poobahs wa CHADEMA. Hapa mwombe radhi.

Yatosha kamanda. Kiranga kashakuelewa na kashaingia mitini......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom