Nimerudisha imani kwa CHADEMA, nimerudisha imani kwa Mbowe, watanzania tuamke hii sasa inatosha

Nimerudisha imani kwa CHADEMA, nimerudisha imani kwa Mbowe, watanzania tuamke hii sasa inatosha

Nasikia mkataba.....

Hauna KIKOMO
Hairuhusiwi kuvunjwa Kwa sababu yoyote ile (kumbuka hauna kikomo)
Serikali yetu kupitia TRA hairuhusiwi kukusanya kodi bali itakuwa inagawiwa nyama choma kidogo baada ya wakubwa kishiba

Mengine yanatia kinyama...
 
Aliye karibu na viongozi wa CHADEMA awasanue fasta. Badala ya kupiga tu kelele tafuteni wataalamu wa lugha fasta wautafsiri huo mkataba kwa lugha rahisi ya kiswahili halafu sambazeni kwa wananchi wa kawaida na wabunge waelewe wanajadili nini. Inawezekena tunawalaumu wabunge kwa kwa kuupigia debe huo mkataba pengine lugha ndio inawachenga. Labda tu wamehaditihiwa tu kuwa huo mkataba ni mzuri lakini hawajui nini kimeandikwa ndani yake.
 
Nimemsikiliza Mh mbowe kwa umakini sana, awali ya yote nisamehewe kwani kuna wakati nilihoji na kuponda maamuzi ya mbowe nikidhani ni 'mlamba asali'

Yameongelewa mengi kuhusiana na mkataba wa Bandari na kampuni ya DP world, lakini maswali matatu ambayo mpaka sasa yamekosa majibu yamenifikirisha sana. Maswali hayo ni

1. Ni muda gani mkataba utadumu (duration)
2. Kwanini bandari za zanzibar hazijaguswa?
3. Hyo kampuni itawekeza kiasi gani? Na nini nchi itapata?

Ndugu zangu, kumbe mkataba huu umevujishwa kwa siri na wazalendo, lakini pia umepelekwa bungeni kujadiliwa tu na kupitishwa. Hakuna kitu kingine wabunge wanaweza kufanya.

Ndani ya nchi yetu kumewahi kushuhudiwa mikataba ya hovyo kama ile ya
A) Kagoda
B) Escrow
C) Buzwagi nk. Lakini mkataba huu ndio wa hovyo na hatari zaidi, kwani hauna kikomo!

Ndugu zangu, ni kweli watanzania wengi tuna njaa, lakini kuna wakati njaa zikae pembeni tuokoe vizazi vijavyo.

Wengi hawajui kua kampuni hii inamilikiwa na nchi za UAE (state owned) sasa sie Tanzania tunashindwa nini kuunda kampuni itakayosimamia bandari zetu.? Keanini tusiunde kampuni ambayo itatoka nje ya Tz kufanya biashara kama zilivyo kampuni za Dp word, au ile ya Arabs contractors? Ni kipi ambacho Tanzania tunakosa?

Sina lengo baya, ila inawezekana kwa sasa tuna uongozi wa hovyo kuwahi kutokea.
Yule Mafia Rostam bado yuko nyuma ya ujambazi mkubwa trust me!
 
Huyu hata sijamuelewa.

Mamlaka ya bandari ni kitu gani kwa serikali?

Kilichpolekwa bungeni na kujadiliwa ambapo inaonekana wabunge wameshajipanga au wamepangwa kukitetea ni Mkataba mama.

Itakatoyofuata ni mikitaba ambayo ikiwa na shida reference itakuwa mkataba mama.

Ni kama vile sheria zote zinavyotokana na sheria mama yaani, Katiba.

Mkataba wenyewe ulishasainiwa takribani miezi 6 iliyopita, kimya kimya. Haraka hii ya nini?
IMG-20230608-WA0045.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe na genge lake ni wapuuzi wamehusika sana kuharibu nchi miaka 5 iliyopita
Wewe unatuondoa kwenye ustaarabu maana utatufanya tukuite kuwa huna tofauti na mbwa! Mbowe kahusikaje na uendeshaji wa nchi miaka 5 iliyopita?
Unamchukia Mbowe utadhani alimrubuni mzazi wako wa kike akamkimbia baba yako ili amtafune?
We kama unamchukia nenda chumbani kwako kamtukane hadi uchoke usituletee humu
 
Yule Mafia Rostam bado yuko nyuma ya ujambazi mkubwa trust me!
Tuna uzembe mkubwa sana katika kulinda nchi yetu. Hata wananchi wenyewe wanapaswa kuwanyoosha wezi na vibaka bila kutegemea polisi au jeshi.
Mwizi au kibaka sio wale wa kuku au simu pekee, bali hata hao kina Rostam nao ni hatari tena zaidi.
Kwa nini tunawashindwa?
 
Ndani ya nchi yetu kumewahi kushuhudiwa mikataba ya hovyo kama ile ya
A) Kagoda
B) Escrow
C) Buzwagi nk. Lakini mkataba huu ndio wa hovyo na hatari zaidi, kwani hauna kikomo!
Rada ya Mzee wa Nyoka mwenye makengeza
Netgroup SA (wale wahuni waliokuja kutuuza umeme ambao ni wa kwetu wenyewe)
IPTL ya singasinga
 
Back
Top Bottom