Nimeshakatwa 120,000/= gharama za kutuma na ya kutolea ndani ya saa 20, tunakomoa wananchi?

Nimeshakatwa 120,000/= gharama za kutuma na ya kutolea ndani ya saa 20, tunakomoa wananchi?

Na angekuwepo Mwendazake basi lawama zote angeshushiwa yeye tofauti na sasa lawama anapata Mwigulu na Mama anaonekana wanamuharibia tu.
CCM ni ileile, Kama wanavyoimba wao!

Ova
 
Kweli lengo ni kukusanya kodi ama kuna mtu anahujumiwa?
Kweli wanaaminini wananchi tutaikubali hali hii kikondoo?
hivi niwaulize swali ina maana kabla ya hizi njia za kutumiana pesa kuptia simu mlikuwa mkiishije?

hizi mpesa sijui tigo pesa juzi tu mwaka 2008 hazikuwepo, maisha hayakwenda?

na si lazima utumie mobile fund transfer, zipo njia nyingne hebu acheni deko za kike.

Nakumbuka miaka ya 2004/5/6 ukitaka kumtumia mtu pesa locally labda 10,000/= unanunua vocha ya 12 elf unakwangua unatuma yeye kule mangi anamtoa ten

Lakini huwezi jua huenda wanataka ku-empower sekta ya kibenki ambayo kwakweli imejeruhiwa mno na hiyo miamala yenu.
wanadai mazingira ya uwekezaji ktk sekta hyo ni magumu sana tanzania
 
Kweli lengo ni kukusanya kodi ama kuna mtu anahujumiwa?
Kweli wanaaminini wananchi tutaikubali hali hii kikondoo?
Umetuma Tsh55000 na Tsh4700.0 ada ya kutolea .Makato Tsh 2,650.00( Ada Tsh 600.00 + Kodi Tsh 2,050.00).Salio Jipya Tsh 12,282.30,Muamala No😛P210716.2316.D08105.
Nimwmtumia mtu makato ni hatari tupu
 
hivi niwaulize swali ina maana kabla ya hizi njia za kutumiana pesa kuptia simu mlikuwa mkiishije?

hizi mpesa sijui tigo pesa juzi tu mwaka 2008 hazikuwepo, maisha hayakwenda?

na si lazima utumie mobile fund transfer, zipo njia nyingne hebu acheni deko za kike.

Nakumbuka miaka ya 2004/5/6 ukitaka kumtumia mtu pesa locally labda 10,000/= unanunua vocha ya 12 elf unakwangua unatuma yeye kule mangi anamtoa ten

Lakini huwezi jua huenda wanataka ku-empower sekta ya kibenki ambayo kwakweli imejeruhiwa mno na hiyo miamala yenu.
wanadai mazingira ya uwekezaji ktk sekta hyo ni magumu sana tanzania
Kwahiyo unataka maendeleo tuliyonayo turudi nyuma, si ndio?
 
Ndiyo lengo. KODI halali ambayo hutoi rushwa ka TRA wakukadirie kidogo wala hawawezi kukubandikia kodi isiyokuwepo. Hii ni afadhali kuliko kupata kodi kwa nguvu na kufunga biashara za watu.Hao matajiri ndio watumiao simu kwa wingi hivyo watatoa kodi kubwa. wewe wa vocha ya 500 watakukata shs 10 siku ukiweka mara moja kwa mwezi ili line isifutwe. Maoni yangu tu. Nataka pesa hizo zikakamilishe mradi wa umeme rufiji na reli ya SGR TU. ULE WA BAGAMOYO WATOE HAO WAWEKEZAJI PESA YOTE KAMA WANAITAKA BANDARI SASA HIVI. ISUBIRI TUKAMILISHE RELINA BWAWA.
Bogus point!
 
Umetuma Tsh55000 na Tsh4700.0 ada ya kutolea .Makato Tsh 2,650.00( Ada Tsh 600.00 + Kodi Tsh 2,050.00).Salio Jipya Tsh 12,282.30,Muamala No😛P210716.2316.D08105.
Nimwmtumia mtu makato ni hatari tupu
Mkuu nadhani Bank kuna nafuu kidogo tutumiee huko watoto wangu nimewafungulia accounts naona ni sehemu sahihi kwa kipindi hichi
 
"Hizi gharama mpya za mitandao ni dalili kuwa hatujuani hali zetu. Hayo makato sio mzigo kwa wenye uwezo bali kwa "wanyonge" ni mzigo mzito. Hakika matajiri na mali zao na maskini na watoto wao."- Dr. Stephen Munga

Wewe mpaka umelipa 120.000 ndani ya saa 20 basi upo vizuri.
JPM aliwakamua matajiri, nyie na michadema mkapiga kelele. Sasa mama kawaachia matajiri mnakatwa nyie mnaanza kulalama. Mnataka lipi maana kwa vyovyote vile serikali lazima iwe na hela na inatakiwa itokane na kodi. Na bado
 
Haya yote yana mwisho wake. Huu ujinga unaoendelea hivi sasa huku Tanzania utakoma.

Watanzania sio wajinga kama wanavyotufikiria.
 
Ni makato ya kijambazi kwa mgongo wa sheria hakuna kodi za namna hiyo...
 
Tulikubaliana tusitumie hiz M/Tigo,halo pesa lakn mazoea yanatabu sana nikijaribu kutuma pesa kwa mama kule shamba nakosa n njia gan nitumie zaid ya hzo
 
Back
Top Bottom