Kwa mlinganisho huu nilitegemea nyani ndo wawe na hizi imani kwa hali ya juu ila sijawahi kuona popote nyani anasali
Mkuu, Almost viumbe wote wenye frontal lobe wana exhibit hizi imani.
Sema kadri kiumbe anavyozidi kuwa na frontal lobe kubwa ndio hizi imani zinakuwa complicated zaidi.
Lakini essence ya hizi imani ni moja...Essense ya kuwa nikifanya kitu A kitaniletea kitu B...ambapo unakuta A na B havina uhusiano wowote kabisa(causal relationship).
Mfano in the wild, nyani huko senegal wameshaonekana wakifanya rituals kama kuponda mawe mti, kila nyani ana mti wake wa kuponda nk. So kuna association wanaamini kuponda miti na imani fulan kma kupata chakula etc... Ukisoma Kazi za Jane Goodal ameelezea deeply tabia ritualistic za nyani.
Ukija maabara kuna experiments nyingi zimeshafanywa kwa Kunguru, Panya, dolphins nk.
Mfano, 1948 famous psychologist B.F Skinner alifanya experiment na njiwa waliokuwa half-starved..Aliwaweka bandani halafu akawa anawapa chakula kila baada ya sekunde kadhaa at a constant interval..As long as ile interval ni fupi, wale njiwa wakaanza kutengeneza behaviours kama kugeuza geuza vichwa, kuzunguka clockwise, kujigeuza geuza chini, kupiga mabawa nk. wakiamini hizo tabia ndo zitaleta chakula.
Baada ya hizo tabia kujengeka hata wakiongeza interval ya kuleta chakula wale njiwa wataendelea kufanya hizo behaviours. Ambapo skinner akiacha kuleta chakula njiwa wanaonekana kama wajinga fulan.
Hii experiment Michael wa Vsauce aliifanya mwaka juzi kwa BINADAMU..mtu anawekwa katika chumba chenye tundu.. halafu kila baada ya sekunde 30 hilo tundu linatoa hela..Sasa wale watu walikuwa wakikaa mule kwenye chumba wanaanza kutengeneza behaviours ambazo waliamini wakifanya ndo zinaleta hela, Kuna wengine waliruka ruka, wengine walizunguka zunguka chumba, wengine walicheza na wengine walichuchumaa. Cheki hapa
So wanyama wengi huwa hatupendi kuwa confused au kukosa control ya matokeo katika mazingira yetu..So instead ya kukubali hatuna control ni bora tutengeneze kitabia/matendo fulani ambayo yatatuaminisha tunayo control hata kama hatuna.
Mfano.
-Kucheza ngoma au kusafisha makaburi li mvua inyeshe
-Kuvaa nguo fulan unapoenda interview
-mchezaji kuchimba chini kabla ya mechi
-Kuvaa nguo/viatu fulani ili timu yako unayoshabikia ishinde (Mimi nilishawahi kudevelop ka tabia kuwa nikienda banda fulani barcelona lazima ishinde)
-Kuweka kakifaa upande fulan dukani ili wateja waongezeke
-Kupiga magoti na kuomba kwa invisible man/woman(Maria)in the sky ili akusaidie jambo fulani nk. Nk.
Sasa hii inashangaza kuwa pamoja na kuwa sisi homo sapiens tumedevelop sana sehemu ya ubongo inayodeal na logic na reasoning, bado we fall prey to these archaic beleif systems.