Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Si afadhali hata huyu profesa anayemwomba mtu ambaye aliwahi kuishi hapa duniani? Ni yupi bora:- kati ya profesa wa kwetu anayemwomba mtu au professor wa India (tena bingwa kindakindaki wa compyuta) anayeabudu ng'ombe?
 
Imani ya mtu iache ilivyo. Kama wewe unaamini ukijilipua utakwenda kupewa mabikra 72 shauri yako !! Kama unaamini kwamba ukimwomba kakakuona, basi bei ya unga itashuka na kukatika umeme mara kwa mara, shauri yako !!

Kama unaamini (kama walivyo maprofesa wengi walio na elimu kubwa kwenye mambo ya teknolojia huko Marekani na Ulaya ), kwamba mwanaume mwenzio anaweza kukuweka kinyumba na akufanye "mke" shauri yako.

ACHANA NA IMANI ZA WATU !!
 
Twende taratibu, umesema Constantine ndio ameanzisha Ukatoliki lakini maelezo yako hayajaonesha alipoanzisha Kanisa jipya! Naomba tujikite hapo. Alafu umesema maaskofu wa Greece kujitenga, mbona hiyo ni baadae sana na sababu zao za huo mtifuano zipo wazi! Hayahusiani na mambo ya Rumi na dola ya kirumi ilishajifia.

Sisi ni Wakristo, hatuhitaji uongo kuinjilisha. Unajua huko Rumi dini ya kiyahudi ilipewa ruhusa pia kabla ya Ukristo? Unajua Ukristo kuwa dini rasmi ya Rumi ilikuwa lini? Usishanganye Wakristo kuruhusiwa na kutambuliwa kama dini na pale rumi ilipoamua kuifanya kuwa dini ya dola.

Alafu unajua faida za Rumi kuokoka? Unajua mchango wao kupitia mifumo na maendeleo yao yalivyosaidia Ukristo imara? Hata mitaguso ya mwanzo kukusanya maaskofu ili kujadili na kuweka misimamo ya kiimani kinyume na uzushi ikiwemo uzushi mkubwa kuwa Yesu si Mungu ulifadhiliwa na Rumi!

Hivi unajua nguvu ya ofisi ya Peter duniani hata leo? Unafikiri ni mapenzi ya shetani? Hata kiimani unafikiri pale kwenye msalaba wa Yesu " Yesu mfalme wa Wayahudi" kuandikwa kwa lugha tatu, Kiebrania, kilatini na kigiriki unafikiri ilikuwa bahati mbaya au kwavile zilikuwa tu lugha maarufu? Kachunguze uelewe ili uache tabia ya upinga Kristo bila kujua.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nimesema alianzisha roman catholic na sio mwanzilishi wa catholic (kanisa la dunia nzima) na huu ni ukweli. Yeye alianzisha dini ya roman catholic kwa kupitia mgongo wa kanisa lililokuwepo tayari na asilimia kubwa aliweza kulicorrupt kanisa lililokuwepo mpaka likapoteza nuru ya Kristo.

Nashukuru kwamba umeelewa kwamba kwa kuzingatia misingi roman catholic lilivyoanza na linavyoendelea sasa ni nje ya neno la Mungu LAKINI taasisi hiyo ya roman catholic ulimwenguni pote inazo faida nyingi hasa kwenye elimu na afya. Kuna maeneo hata injili imepelekwa na roman catholic maana mtume Paulo alisema iwe kwa hila au kwa dhati cha muhimu injili ifike mbali.

Mimi ninaamini Mungu anao watu wengi ndani ya roman catholic na anazidi kuwaokoa kwa neema yake. Movement kama ile ya charismatic ni njia mojawapo ya kupeleka wokovu ndani ya roman catholic. Kuna nchi kadhaa ambapo roman catholic inashirikiana na makanisa yanayoitwa ya kiprotestant na hii imesaidia wengi kukutana na Yesu Kristo.

Changamoto kubwa ni ileile aliyokutana nayo Bwana Yesu Kristo wakati alipokuwa anahubiri injili. Watu wa dini huwa wanakuwa dogmatic. Mungu anabadilisha methods za utendaji wake na kuleta mafunuo mapya kila kizazi bila kubadilisha principles zake. Neno lake halibadiliki.

Roman catholic ilitakiwa kutubu kipindi cha Luther na ilipokataa tukapata Lutheran. Lutheran ilitakiwa kutubu kipindi cha John Wesley na Charles Wesley na ilipokataa tukapata Methodist na baptist. Hawa nao walipokataa kupokea mafunuo mapya kipindi cha Seymour tukapata Assemblies na Charismatic. Hawa nao sasa hivi hawataki kukubali ufunuo wa kinabii na mitume hivyo mvutano unaendelea nyakati hizi.

Hapa duniani hakuna jipya, yanajirudia yaleyale. Hatari kubwa ni kumuwekea Mungu mipaka katika utendaji wake. Mimi niko open kujifunza katikati ya mafunuo mapya kwa kuhakikisha nayakubali yale yaliyopo kwenye neno la Mungu na kuyakataa yale yaliyo nje. Canonicity of the bible tuizingatie, tusipunguze au kuongeza lolote.
 
Mantiki ya hii paragraph ni kuwa umemfanya Kristu awe muongo kwani alisema milango ya kuzimu haitalishinda kanisa lakini wewe unasema kanisa lilishindwa vibaya na Rumi mpaka likapoteza nuru
 
Kanisa Katoliki liligawanyika karne ya 10 na ukabakia upande wa Constantinople ugiriki na Roma kwa Papa. Constantinople na Rome walikuwa na tofauti muda mrefu sababu wote walikuwa na nguvu hivyo kufanya hata mambo ya imani kupingana kabla mgogoro huo kukolezwa na kulipasua Kanisa mwaka 1054. Pamoja na tofauti zilizopo ila makanisa haya yanafanana mambo mengi kimafundisho.

Kanisa Katoliki la Roma ni Kanisa la magharibi ikijumuisha na Waprotestanti ambao chanzo chao ni Kanisa Katoliki. Hivyo Constantine hakuanzisha Roman Catholic maana Petro na Paul ndio walioanzisha huduma huko hadi mauti yao walipouawa na warumi. Baada ya kuuawa Jimbo la Roma alilohudumu Petro na Paulo liliendelea kuwa na Maaskofu warithi wa Petro na ndio waliokomaa hadi Rumi ikawatambua rasmi baadae sana.

Kanisa Katoliki halifichi historia yake na hata Askofu Kilaini ameeleza mara nyingi crisis iliyopitia Kanisa hasa nyakati Maaskofu walipokuwa pia viongozi wa serikali huko rumi. Hadi kuja kutenga Kanisa na dola mengi yalitokea na sio kificho.

Pamoja na changamoto zote Kanisa lakini mafundisho ya Kanisa yametunzwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu hata leo. Kanisa hata leo linapitia crisis za kutisha ambazo wewe ukijua unaweza kusema Lucifer amekaa Vatican lakini kitu kimoja alichoahidi Yesu kinachoishi ni hata malango ya kuzimu haitalishinda ndio maana tutabakia na matatizo ya viongozi wa Kanisa n.k lakini sio mafundisho ambayo msingi wake hakuna wa kutikisa.

Kanisa Katoliki ni Kanisa lililoinjilisha kuliko Kanisa lolote duniani na lenye ushahidi wa uwepo wake toka mitume ( including Orthodox). Zaidi ya watu bilioni moja duniani wamebatizwa na kumkiri Yesu ( hapa najua mnapinga kwamba hawajaokoka).

Kuhusu Karistimatiki ni mkondo tu ambao ni vitu vya kawaida Kanisa Katoliki! Ndio maana ya kuwa Katoliki hukatazwi kufanya yasiyo kinyume na mafundisho ya Kanisa kwa kadri kila mmoja roho anavyomtuma. Ndio kukubalika haikuwa rahisi sababu imebeba mapokeo ya kiprotestanti au kilokole tunavyosema siku hizi. Ukienda kwenye semina za malezi na makuzi ya kiroho kule ndio utafindishwa kwa kina na kuelewa mengi.

Kwahiyo Constantine anamchango mzuri kwa uhuru wa Kanisa lakini hakuanzisha Kanisa. Martin Luther alianzisha tunajua na walutheri hawapingi, ufufuo na uzima tunajua ameanzisha Gwajima na hatupingi.

Hata ukienda Google ukiandika Founder wa kila Kanisa itakupa majibu alafu search founder wa Roman Catholic utapata jibu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Mantiki ya hii paragraph ni kuwa umemfanya Kristu awe muongo kwani alisema milango ya kuzimu haitalishinda kanisa lakini wewe unasema kanisa lilishindwa vibaya na Rumi mpaka likapoteza nuru
Yes, Kwamba Kanisa lilishindwa na Rumi hadi padre mmoja Martin Luther na wenzake "reformers" ndio wakaleta Ukristo wa kweli!

Hao reformers waliunda makanisa yao yenye mafundisho yao, wakanyofoa vitabu 7 vya agano la kale! Waliunda dini mpya ndani ya Ukristo ambao haukuwepo tangu mwanzo na hata wao walivyoupokea!

Reformers maana yake ilipaswa kuwa kwenye kile kilichopo lakini wao waliunda mapya na sasa tuna madhehebu zaidi ya 40,000 ya Kikristo yenye mambo mengi tofauti! Hii sio reformation ni deformation!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu huyo amekaza ubongo tu

Anasema Constantino alipoanzisha Roman Catholic, Kanisa la Greek likajitenga na wakakataa mafundisho Yao...
Na baadae baada ya martin Luther kuhoji.... Roman Catholic wakaongeza vitabu

Amesahau kwamba hao orthodox hivyo vitabu nao wanatumia.

Pia hata wao wanasali Kwa Bikira Maria atuombee kama sisi.

Na mambo mengi wanafanana kama sisi isipokuwa tofauti ndogo ndogo tu
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]!
 
Uje utueleze baada ya Constantine kuwa mkatoliki, na mambo ya ajabu kutokea ..... Kanisa la Greek na Alexandria walijitenga .....

Baadae baada ya miaka 1500s Roman Catholic ikaongeza vitabu !

Swali
Je mbona hayo makanisa uliyoyasema kuwa yalijitenga mbona nawao wanatumia hivyo vitabu, ambavyo wewe unadai Roman Catholic waliviongeza kweny 1500s, ikiwa makanisa hayo yalijitenga kabla 1500s ?

Hayo mambo ya ajabu yaliyoingizwa Roman Catholic ni yapi ??

Unajuwa kuwa sehemu kubwa baina ya orhodox na Roman tunafanana ?

Hata wao wanamuomba Bikira Maria awaombee
 
Vitu vingine ni logic kidogo tu,bila kujali aina ya dini,binadamu wote tunaomba kwa "superior being"aliyesababisha sisi na Dunia na ulimwengu uwepo!!huyo aliyevitengeneza,awe Allah,God,Jah,Jesus,
Bottom line vitu havitokei tu,huwezi kusema,uende dukani uikute Samsung Galaxy,au apple,harsfu useme imetokea tu!!lazima Kuna brain behind iliyoitrngrneza.

Sasa kama wandsmu wapo,na Dunia,na sayari!!The could not have just happened by accident!some one some super being designed all of these.
Huyo ndio Profesa akifumba macho anamuona!!
 
paruraneni sana ila masdini haya yooote tumeletewa kila mmoja aishi kwa jinsi anavyoona inafaa tuache kukasirikiana
 
Iliwekwa na Nani?
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe. Hayo unayosema wenzio walishayajua zamani. Wewe ni heretic. Kanisa lenye miaka 2000 limepitia mengi na hakika Roho Mtakatifu walioahidiwa atawasaidia anawasaidia na kuwafundisha.

Ungejaribu kuwauliza ni kwa nini, mimi ninafahamu ni kwa nini anamuomba Maria na watakatifu. Na imeandikwa, isitoshe sio kinyume na maandiko wala amri za Mungu.
 
Haya maswala ya imani ni bora kuheshimu imani ya mtu pasipo kuidhihaki.
 
Uzuri ni kuwa wewe mwenyeww huna uwakika na ulichokiandika na wala hauna ushahidi wowote wa kisayansi na kiimani pia, hivyo sioni sababu ya wewe kumshangaa le professor.
 
Nilitegemea uweke maandiko yanayosema uombe kwa hao akina maria na watakatifu badala ya kuweka empty statements.
 
Hapa unaonesha wewe ni mshabiki wa katoliki na upo tayari hata kudanganya ili ujifurahishe. Naomba unijibu hili swali, vitabu vile sita viliongezwa mwaka gani kwenye biblia ya wakatoliki?
 
Mantiki ya hii paragraph ni kuwa umemfanya Kristu awe muongo kwani alisema milango ya kuzimu haitalishinda kanisa lakini wewe unasema kanisa lilishindwa vibaya na Rumi mpaka likapoteza nuru
Hii argument yako ni dhaifu sana. Hujaielewa kauli ya Bwana Yesu Kristo. Rudi kusoma historia halafu utumie argument yako kutueleza ilikuwaje nchi za kikristo kama uturuki, misri, tunisia, algeria, syria na indonesia zimekuwa za kiislamu sasa hivi.

Hapo ina maana Yesu Kristo alidanganya kwamba kanisa halitashindwa? Kipindi cha mitume kanisa la antiokia iliyopo syria ndio lilikuwa kanisa kuu na baadae kanisa la alexandria la pale misri. Makanisa saba yenye ujumbe wa kitabu cha ufunuo yalikuwa asia minor kwenye nchi ya uturuki ya sasa, yameenda wapi?

Roman catholic ilipoteza nuru na haikuweza tena kurudi kwa Kristo, imebaki kuwa taasisi ya kipagani inayojiita kanisa na Mungu wala hajazuiliwa. Kanisa lake halisi halijashindwa, bado linasonga mbele duniani kote. Hata Yerusalemu kanisa lilipokataliwa watu waliendelea kuhubiri dunia nzima hivyo roman catholic kumuacha Mungu haimaanishi kanisa lilishindwa.
 
Poa, thibitisha basi sio kunilisha maneno matupu.
Kwanza kati ya Allah, Yesu, Krishna, Budha, Zeus, Zumaridi, Yahweh, Nk. Nk. Na wengine 5000+ Ni yupi aliyeumba dunia? Maana hao wote wanatofautiana sifa na sio mmoja.

Ukidhajibu hilo, inabidi kwanza uthibitishe huyo Mungu kama yupo
Halafu sasa ndio uthibitishe ni kwa ushahidi upi huyo Allah/Yesu,/Yehova/Krishna/Zeus/Budha aliumba dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…