Twende taratibu, umesema Constantine ndio ameanzisha Ukatoliki lakini maelezo yako hayajaonesha alipoanzisha Kanisa jipya! Naomba tujikite hapo. Alafu umesema maaskofu wa Greece kujitenga, mbona hiyo ni baadae sana na sababu zao za huo mtifuano zipo wazi! Hayahusiani na mambo ya Rumi na dola ya kirumi ilishajifia.
Sisi ni Wakristo, hatuhitaji uongo kuinjilisha. Unajua huko Rumi dini ya kiyahudi ilipewa ruhusa pia kabla ya Ukristo? Unajua Ukristo kuwa dini rasmi ya Rumi ilikuwa lini? Usishanganye Wakristo kuruhusiwa na kutambuliwa kama dini na pale rumi ilipoamua kuifanya kuwa dini ya dola.
Alafu unajua faida za Rumi kuokoka? Unajua mchango wao kupitia mifumo na maendeleo yao yalivyosaidia Ukristo imara? Hata mitaguso ya mwanzo kukusanya maaskofu ili kujadili na kuweka misimamo ya kiimani kinyume na uzushi ikiwemo uzushi mkubwa kuwa Yesu si Mungu ulifadhiliwa na Rumi!
Hivi unajua nguvu ya ofisi ya Peter duniani hata leo? Unafikiri ni mapenzi ya shetani? Hata kiimani unafikiri pale kwenye msalaba wa Yesu " Yesu mfalme wa Wayahudi" kuandikwa kwa lugha tatu, Kiebrania, kilatini na kigiriki unafikiri ilikuwa bahati mbaya au kwavile zilikuwa tu lugha maarufu? Kachunguze uelewe ili uache tabia ya upinga Kristo bila kujua.
Sent from my SM-A315F using
JamiiForums mobile app