Nimeshangaa Mufti kuongea maneno ya kujipendekeza kuwa Rais awasamehe kina Mbowe

Hivi kumbe gaidi ni rahisi kusamehewa kiivyo kweli tanzania ina mambo ya ajabu.ko osama bi laden alikuwa gaidi nini kilitokea ivi mnacheza na ugaisi.ninacho jua mbowe siyo gaidi mambo ya katiba mpya ndoo chanzo cha yote.
Mkwani mkuu alichokifanya Osama ndio kinabeba tafsiri ya neno ugaidi? neno ugaidi lina maana yake sidhani hadi ufanye kama alivyofanya Osama ndio uitwe ugaidi.

Sijasema kuwa Mbowe ni gaidi naamini ni mambo ya kisiasa ila hoja yangu ni huo mfano wako wa Osama.
 
Kama ni kero,kwa Nini mlimchagua!?
 
Huo ni msimamo wa mbowe na nimsimamo wa familia kama hujui.
Lakin Mbowe hawezi kutoka kwa gharama ya kuomba msamaha au kuombewa msamaha
kwa kosa ambalo sio lake.
Hao wangeomba haki itendeke.
Jela si kuzuri na familia yake inamuhitaji, sidhani kama kuendelea kukomaa kwenye hii kesi kutapanda mbegu yeyote kwa nchi kama Tanzania.
 
Wewe jamaa Sesten Zakazaka ,umeandika busara kama zimetoka kwa Mfalme Suleiman.
Ubarikiwe sana.
 
Jela si kuzuri na familia yake inamuhitaji, sidhani kama kuendelea kukomaa kwenye hii kesi kutapanda mbegu yeyote kwa nchi kama Tanzania.
Familia yake inamhitaji ndio lakini sio kwa gharama ya kuomba msamaha kwa kosa asilotenda.
Huo ndio msimamo wa familia.
 
Familia yake inamhitaji ndio lakini sio kwa gharama ya kuomba msamaha kwa kosa asilotenda.
Huo ndio msimamo wa familia.
Ndio nasema huko kukomaa kwamba hawataki kuomba msamaha ( ili awe huru) kwa sababu hana kosa ni jambo ambalo halipandi mbegu yeyote kwa nchi kama Tanzania, ni yeye au pamoja na familia yake ndio wanaoumia hapo na hakuna wanachokijenga.

Ila kama wenyewe wameona kuomba msamaha ni sawa kukubali kuwa ni kweli alifanya hilo kosa na hivyo ataharibu heshima yake na hilo ni jambo muhimu kwao kuliko chochote basi sawa waendelee kukomaa.
 
Muft alipoomba waachiliwe mashehe wa uamsho ndani ya wiki wakaachiliwa.
Nilipposikia na kwa Mbowe nikajua kapangwa pia wamedharirika.
Yaani haingii akilini,miezi yote hiyo wako ndani!Ila siku Moja kabla ya kuanza kujitetea shekhe anazungumza vile,halafu siku ya kuanza kujitetea wanafuta kesi!
Mbowe afungue kesi kudai fidia!
 
Yaani haingii akilini,miezi yote hiyo wako ndani!Ila siku Moja kabla ya kuanza kujitetea shekhe anazungumza vile,halafu siku ya kuanza kujitetea wanafuta kesi!
Mbowe afungue kesi kudai fidia!
Mbowe aendelee kukiwasha tu mtaani itaeleweka.
 
Msamaha aliomuombea umezaa matunda na leo amesamehewa yule bwana! Mufti oyeeeee!!!
 
Nna uhakika, umewashuka, shuuuu. Mmeona kauli ya Mufti ilivyo na nguvu?



Mmnh!

Wengine wanafikiri huenda ni mingo tu ilitegwa kiana ya mtindo wa propaganda!

Tuzidi kuomba amani, Umoja, haki, Umoja na mshikamano wa Kuanzia mtu mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.
 
Plan planned man
 
Nna uhakika, umewashuka, shuuuu. Mmeona kauli ya Mufti ilivyo na nguvu?
Umemaliza mjadala.Mufti Mungu ambariki,amemuombea msamaha,mtu asiye wa imani yake.Huu ndio uislamu,hata Mtume Muhammad(S.A.W),wengi waliompiga mawe,kumtukana ,kumdhihaki,wakati yupo Maka,na akakimbia Madina,siku aliyorudi akiwa na nguvu,na wafuasi wengi na jeshi lenye nguvu,wale waliomfanyia Ubaya,ambao sio waislamu,walifikiria,atawaadhibu,lakini aliwaambia endeleni na shughuli zenu,sikuja kuwaadhibu.Hongera Rais,mama yetu,Kipenzi cha watanzania,Mungu akubariki,kwa kukubali,ombi la viongozi wa dini,akiwemo Mufti Sheikh,Doktour Wa Tanzania.
 
Msamaha aliomuombea umezaa matunda na leo amesamehewa yule bwana! Mufti oyeeeee!!!
Yule Mufti Sheikh Doktour,ni msomi wa Hali ya juu.Mtu aliyeweza kuwaunganisha waislamu wa Tanzania,na kuwa kitu kimoja,katika masuala ya uislamu,ni.msomi wa hali ya juu.
 
Hivi kumbe bado upo na vitusi vyako vya reja reja?
 
Elimu ndugu yangu... elimu ya madrassa haitoshi
 
Eti huna elimu ya kushindana na wa mwaka wa kwanza wa madrasa 😄😄 kweli akili yako ni ya kimadrassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…