Nimeshangaa sana, Timu za Ujerumani badala ya kuungana kumaliza utawala wa Bayern, zinakamiana

Nimeshangaa sana, Timu za Ujerumani badala ya kuungana kumaliza utawala wa Bayern, zinakamiana

Kwa hiyo Haaland na Sancho waliibwa na Bayern ili kuidhoofisha Dortmund?
 
Hakuna ligi zenye matokeo ya kushangaza km ligi za ujerumani na Italy🤣🤣


Sa dortmund jana alihitaji sure tu na yupo nyumbani ila hakupata hata io sare
We jamaa ni muongo hatari😂😂😂
 
Unataka wapange matokeo? Yaani Mainz wakubali kufungwa kwa sababu tu FC BAYERN amechukua ubingwa mara nyingi?

Ukishapanga matokeo mkapata bingwa asiyestahili nini kitaenda tokea tokea kwenye UCL?
 
We huna akili kabisa, unadhani ni bongo pale, kwamba Singida ukicheza naye unajiokotea kwa sababu ni tawi la utopolo lile
 
Dortmund wapuuzi sana. Yan wachezaji mentality yao sijui ilikuaje unapata penalty unakosa, mechi ya kutafuta unatanguliwa kwa goli mbili? Kabla ta mechi ya jana huko nyuma walifanikiwa kuongoza ligi ila wakawa wanajishaua mara wasare, wapoteze yan watakavyo jisikia wao wenyewe. Kwa kilichotokea jana mi siwashangai kabisa walikitafuta wenyewe
 
Kocha Amna mule wachezaji awakutakiwa wapewe matokeo ya mechi nyingne inavyoendelea alivyoona bayern wamechomolewa goli wakawa wanashangilia na kuwaambia wachezaji wake kuwa bayern tayari amechomolewa wachezaji wakaanza kupunguza munkari ya kushambulia wakitegemea bayern akidraw ata wao wakifungwa tayari wanachukua kombe..
 
Ligi imekosa mvuto, timu moja inachukua kombe kwa miaka 11 mfululizo kwa kutumia mbinu za kupora wachezaji wazuri kutoka timu pinzani

Kwa mbinu hii pengine inaweza kuchukua ubingwa hata mara 20 mfululizo, maana msimu huu ndio walikuwa dhaifu kuliko misimu mingine

Badala ya timu kuungana ili kuua hii monopoly inayoua mpira, ndiyo kwanza zinakamiana

View attachment 2637694
Unataka kuleta mambo ya Singida Big Stars na Yanga katika soka la Ulaya??
 
Zamani enzi hizo twacheza mpira wa makaratasi, ulikuwa ukisikia neno bundes liga maana yake ni rafu mwanzo mwisho.
Ila bundesliga ya Dortmund hapana
Ilikua ni ligi ya mpira kazi
Kipa jamii ya Oliver Khan
Mabeki kina olive beharf na Samuel kufor
Viungo jamii ya David odonko
Halafu washambuliaji watu chuma kina Michael Ballack ,anatandika shuti kati kati ya uwanja ambalo kipa akipangua anateguka mkono,famasihala Nini
Hii bundesliga ya Sasa wamejaa utelembwe na lonyolonyo kina Jude Bellingham na musiala hamna kitu kabisa
 
Back
Top Bottom