Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Mwenye kosa ndio alaumiwe. Makosa makubwa ya Prof. Mkenda; Waziri wa Kilimo hadi akaambiwa hoja zake (sio yeye binafsi) ni nonsense yanatokana na:

1. Kuishi kwa Kukariri na kutotambua majira:
Hizo sera anazozozitetea za ''Protectionism'' tuliziacha toka March 2021. Kila kiongozi ana falsafa zake na maono yake, na bahati nzuri Rais Samia amekuwa wazi sana kuhusu sera za kuifungua nchi. Huyu mwenzetu alikuwa bado yupo kwenye zama za awamu ya tano...
Inabidi umwambie na Majaliwa Kasim Majaliwa maana yeye PM na Mkenda waliongea lugha sawa
 
..Waziri hajazuia uagizaji wa sukari.

..hata mwaka huu kuna sukari ambayo imeingia nchini kutoka Uganda.

..Tatizo ni taarifa za uongo toka kwa Raisi Museveni.
 
Mwenye kosa ndio alaumiwe. Makosa makubwa ya Prof. Mkenda; Waziri wa Kilimo hadi akaambiwa hoja zake (sio yeye binafsi) ni nonsense yanatokana na:

1. Kuishi kwa Kukariri na kutotambua majira:
Hizo sera anazozozitetea za ''Protectionism'' tuliziacha toka March 2021. Kila kiongozi ana falsafa zake na maono yake, na bahati nzuri Rais Samia amekuwa wazi sana kuhusu sera za kuifungua nchi. Huyu mwenzetu alikuwa bado yupo kwenye zama za awamu ya tano...
Ukimaliza kutoa povu lako la kutokujielewa na uelewa finyu kwenye intra country trading issues kalale. Rubbish

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hapa tatizo ni Mkenda kuambiwa Hana SENCE? Ukweli Kati ya mawaziri si Mkenda peke yake ambaye Hana SENCE, wako wengi tu akiwemo wa Fedha, wa Biashara, wa Maliasili, wa Madini na kubwa Lao Afya.

Majority is zero including Head of state
 
Tunalinda viwanda vya ndani vyenye uwezo mdogo kwa gharama kubwa sana na kwa kubebesha mzigo wananchi. Sukari ikiingia kutoka Brazil bei yake haitazidi TSH. 1800, ukilinganisha na bei ya sasa ya TSH 2600 hii si kulinda viwanda vya ndani bali ni rushwa. Mambo ya monopoly yalishaisha zamani! Kwanini tunalinda viwanda vya sukari tu na vingine vinashindana na vya nje kama kawaida. Natamani kujua viwanda vya sukari vinamilikiwa na nani maana vilibinafsishwa.
TPC inamilikiwa na beberu, sukari yake 90% inatoka nje, kwa nini kusiwe na uhaba.
 
Hivi bado kuna uhaba wa sukari mpaka leo? Sijasikia zile kelele muda mrefu.

Rais wetu naona kama amekubali kutumiwa na Museveni nae akatumika, kama Museveni ana sukari nyingi kwake haina soko ameona aje kulitafuta huku na sisi badala ya kujiuliza kama tunaihitaji naona tumekimbilia kukubali ombi tu ili kukuza urafiki na majirani.

Suala la kuita msimamo wa waziri wake Nonsense tena public nalo nalipinga, kama alikerwa na huo msimamo ana kila nafasi ya kuonana na waziri wake na kumweleza aliyonayo, sio kumsubiri Museveni aje ndio anamnanga mbele za watu, hizi ni tabia typical za kike - umbea.

Huyu mama haijui management kbs yaani Mungu atuhurumie sana mtu wa calibre yake ndiyo anakuwa mkuu wa nchi kweli. Hiyo kauli aliyoitoa in broad sense amejinanga mwenyewe kwamba serikali yake ni 'nonsense'
 
Mwenye kosa ndio alaumiwe. Makosa makubwa ya Prof. Mkenda; Waziri wa Kilimo hadi akaambiwa hoja zake (sio yeye binafsi) ni nonsense yanatokana na:

1. Kuishi kwa Kukariri na kutotambua majira
Hizo sera anazozozitetea za ''Protectionism'' tuliziacha toka March 2021. Kila kiongozi ana falsafa zake na maono yake, na bahati nzuri Rais Samia amekuwa wazi sana kuhusu sera za kuifungua nchi. Huyu mwenzetu alikuwa bado yupo kwenye zama za awamu ya tano.

2. Kuvuka mpaka wa majukumu yake
Waziri wa Kilimo ni nafasi ya ndani ya nchi, hata Zanzabar hapo hana mamlaka. Amepata wapi audacity ya kuzungumzia sera za nchi dhidi ya nchi nyingine. Je yeye ndiye mhimili wa diplomasia ya nchi. Mwenye dhamana ya kwanza linapokuja suala la mahusiano iwe ya kibiashara au vyovyote katika ya nchi na nchi ni RAIS mwenyewe au msaidizi wake Waziri wa Mambo ya nje. Ambaye naye huzungumza kwa niaba ya Rais; hata Waziri Mkuu au Makamu wa Rais hawezi kuzungumza suala la nchi na nchi bila idhini ya Rais wa nchi. Sasa huyu mwenzetu huo ujasiri aliotoa wapi? kama sio kudhani mambo ni kama juzi.

Rais wetu hapati hata muda wa kupumzika kila siku anafanya diplomasia ndani na nje ya nchi. Akirudi Ikulu hakuna kupumzika ni mlolongo wa mikutano kila siku ya kidiplomasia na uchumi ili kuifungua nchi ambayo ki ukweli mahusiano na nchi na taasisi nyingi hayakuwa mazuri. Mama halali usingizi, kutia uzito anaona aende mwenyewe maana ni ngumu mtu mwingine kuaminika maana mambo ya nyuma yaliamuliwa na sitting president. Hivyo, lazima Rais mwenyewe aende ili kujenga imani. Chuma hutolewa na chuma.

Rais anafanya jitihada hizi halafu anatokea mtu anasema '' MIMI SITAFANYA'' wewe ni nani useme hivyo? ni utashi wako au utashi wa nchi?

Tuwe makini sana, nchi sasa hivi iko kwenye paradigm shift mambo makubwa ya kisera ni vyema kufanya consultations na wakuu kabla ya kutoa matamko.
Crap!
Protectioism ni sera ya kuzuia kabisa bidhaa toka nje zisiingie nchini.
But it does not make sense kuingiza sukari yenye bei chee wakati wazalishaji wa ndani wapo na wanafanya kazi.
Serikali ile matapishi yake yenyewe na wanajua kuwa bei ya sukari inayozalishwa nchini imechangiwa na kodi lukuki inazoziandama sekta binafsi na viwanda.
Tusiruke majivu na kuishia kwenye moto.
 
Rudia tena kusoma ulichoandika.............if it doesn't make sense kwako kuingiza sukari ya bei chee, kwa sisi wananchi tusio na na kipato kikubwa it makes a helluva lot of sense. Why wazalishaji wa ndani wapewe preferential treatment...........kwanini sukari tu? Mbona haihusu viwanda vingine vinavyozalisha hapa nchini? Nadhani umesikia video hapo juu ( courtesy of Joka Kuu), kwamba wengi waliobinafsishiwa hivyo viwanda walikuwa ni watumishi waandamizi serikalini. Kwa hiyo walitengeneza mazingira ya viwanda vyao kulindwa , na uagiza wa sukari vibali wanakuwa wanapewa wao.............kwanini?
 
Nimeshangazwa na kauli hii ya Mh Rais, kuita msimamo wa mteule wake Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje, kuwa NONSENSE, tena hadharani.

Nimesikitishwa na kauli hiyo kwa sababu mbili.

Moja, public reprimand kwa kiongozi mwandamizi, sidhani kama ni utawala bora.

Na hii naanza kuhisi ile power is getting to the head, and power corrupts.

Pili, nimesikiliza arguments za Mkenda, though pompous, kuna relevance pale.

Argument ni kuagiza sukari kama kuna shortage, si kwa matakwa ya wafanyabiashara.

Sasa wale wawekezaji wanaovipanua viwanda ili ku boost uzalishaji wa sukari, wale ni nonsense?

All in all, Mkenda anapaswa kujiuzulu ku-save face.
Bidhaa yoyote duniani inaagizwa na kuingizwa sokoni kama kuna DEMAND. Wanaojua hali ya demand na supply ni washiriki wa soko, yaani wauzaji na wanunuzi, nje ya hapo ni siasa tupu.
Mfanyabiashara anaagiza bidhaa at his own risk, akiamini ataiuza apate faida, huku pia akijua uwezekano wa kushindwa kuiuza (na kupata hasara), lakini anaingia kwa kuwa ameshapima na kuona uwezekano wa faida ni mkubwa zaidi.
Sasa wewe serikali unapokataza mfanyabiashara kuzungusha pesa yake halali, unafanya hivyo kwa faida ya nani?
Ukizuia mfanyabiashara kuagiza sukari kutoka nje, na matokeo yake wananchi wa kawaida wakauziwa sukari ya ndani ya nchi kwa bei kubwa kuliko ile ya nje, umemsaidia nani? Kama serikali inataka nafuu ya maisha kwa wananchi wake, ingeboresha mazingira ya gharama za uzalishaji ili wananchi wapate sukari ya ndani kwa gharama nafuu kuliko sukari ya nje, tofauti na hapo ni kuumiza wananchi.
Na hata sukari ya ndani ikishakuwa bei rahisi, bado wanaotaka sukari ya nje wana haki ya kuinunua hata kama wanalipa ghali kwa sababu pesa wanazotumia kununua hiyo ya bei ghali ni za kwao; ni utashi wao na choice yao kununua kitu wanachotaka. Hizo ndizo dynamics za soko.
Mchele pale sokoni Tandale unauzwa sh 1,700 kwa kilo, lakini bado kuna watu wanaununua katika supermarkets kwa sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo. Ni chaguo lao, kwanini tuwaingilie? Bidhaa ziletwe sokoni wateja wachague wanachotaka.
 
Nimeshangazwa na kauli hii ya Mh Rais, kuita msimamo wa mteule wake Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje, kuwa NONSENSE, tena hadharani.

Nimesikitishwa na kauli hiyo kwa sababu mbili.

Moja, public reprimand kwa kiongozi mwandamizi, sidhani kama ni utawala bora.

Na hii naanza kuhisi ile power is getting to the head, and power corrupts.

Pili, nimesikiliza arguments za Mkenda, though pompous, kuna relevance pale.

Argument ni kuagiza sukari kama kuna shortage, si kwa matakwa ya wafanyabiashara.

Sasa wale wawekezaji wanaovipanua viwanda ili ku boost uzalishaji wa sukari, wale ni nonsense?

All in all, Mkenda anapaswa kujiuzulu ku-save face.
Ukishangaa ya sukari na kutaka kupewa mlungula airport sijui huko kwenye umeme ndio tusemeje, watu wa sampuli ya akina Prof ndio wanasiasa wetu hawaitaki, naona fursa kwa wapiga dili zinazirudi kurudi, wale wanaojifanya wazalendo na wana uchungu na nchi hii huo ndio mwanzo wa kupuuzwa, kuhusu suala la sukari kuna janja nyingi nyuma ya pazia na M7 kaamua makusudi kudanganya, nimemsoma balozi Ami Mpungwe ambaye ni mwenyekiti wa KSC kuwa si kweli kuwa sukari kutoka Uganda haiagizwi na ametoa mfano sukari ambayo viwanda vimenunua kutoka Uganda hivi karibuni, tulidhani tunapokea shule kumbe kuna jambo .
 
Kwanza inatakiwa uelewe Tanzania Ina shortage ya sukari kwa miaka mitano mfululizo, na hii yote imesababishwa na jiwe, Hivyo basi sukari inatakiwa iagizwe Mana viwanda vyetu having uwezo wa kuzalisha sukari mpaka wananchi wote tutosheke,
Nazani unaelewa kuwa bei ya sukari imeongezeka kwa asilimia mia moja. Wacha tufungue mipaka ili mwananchi apate nafuu
Tatizo ni uwezo wa viwanda kuzalisha sukari au malighafi(miwa) ndiyo hatuna/tunazalisha kwa kiwango kidogo?
 
Uko sahihi kwa kiwango kikubwa
Lakini naye mama haeleweki kama ni mamalia au ndege.Leo anafukia sera za mwendazake kesho anatetemeka yupo Chato kuzindua shule ya msingi...
Anataka kufuta maujinga ya jiwe huku akiliogopa genge la Chato..
Asimame sehemu moja aache kutuchanganya
Mwenye kosa ndio alaumiwe. Makosa makubwa ya Prof. Mkenda; Waziri wa Kilimo hadi akaambiwa hoja zake (sio yeye binafsi) ni nonsense yanatokana na:

1. Kuishi kwa Kukariri na kutotambua majira
Hizo sera anazozozitetea za ''Protectionism'' tuliziacha toka March 2021. Kila kiongozi ana falsafa zake na maono yake, na bahati nzuri Rais Samia amekuwa wazi sana kuhusu sera za kuifungua nchi. Huyu mwenzetu alikuwa bado yupo kwenye zama za awamu ya tano.

2. Kuvuka mpaka wa majukumu yake
Waziri wa Kilimo ni nafasi ya ndani ya nchi, hata Zanzabar hapo hana mamlaka. Amepata wapi audacity ya kuzungumzia sera za nchi dhidi ya nchi nyingine. Je yeye ndiye mhimili wa diplomasia ya nchi. Mwenye dhamana ya kwanza linapokuja suala la mahusiano iwe ya kibiashara au vyovyote katika ya nchi na nchi ni RAIS mwenyewe au msaidizi wake Waziri wa Mambo ya nje. Ambaye naye huzungumza kwa niaba ya Rais; hata Waziri Mkuu au Makamu wa Rais hawezi kuzungumza suala la nchi na nchi bila idhini ya Rais wa nchi. Sasa huyu mwenzetu huo ujasiri aliotoa wapi? kama sio kudhani mambo ni kama juzi.

Rais wetu hapati hata muda wa kupumzika kila siku anafanya diplomasia ndani na nje ya nchi. Akirudi Ikulu hakuna kupumzika ni mlolongo wa mikutano kila siku ya kidiplomasia na uchumi ili kuifungua nchi ambayo ki ukweli mahusiano na nchi na taasisi nyingi hayakuwa mazuri. Mama halali usingizi, kutia uzito anaona aende mwenyewe maana ni ngumu mtu mwingine kuaminika maana mambo ya nyuma yaliamuliwa na sitting president. Hivyo, lazima Rais mwenyewe aende ili kujenga imani. Chuma hutolewa na chuma.

Rais anafanya jitihada hizi halafu anatokea mtu anasema '' MIMI SITAFANYA'' wewe ni nani useme hivyo? ni utashi wako au utashi wa nchi?

Tuwe makini sana, nchi sasa hivi iko kwenye paradigm shift mambo makubwa ya kisera ni vyema kufanya consultations na wakuu kabla ya kutoa matamko.
 
Si tunaagiza sukari kwa ajili ya shortage, shortage ipo haipo, kama ipo why isiagizwe?
Hao wanaotanua, watanue tu, ikitosheleza tutaacha kuagiza

Acheni bidhaa zifurike mtaani bei ishuke.

Hii tabia ya kupendelea, matokeo yake ndio haya.
 
Very sad,

Hivi hawa communicate ndani kwa ndani mpaka wadhalilishane kwenye media ??....kuna udhaifu kwenye mawasiliano yao
 
Bro ni vizuri pia ujue kuwa Uganda nao wamesucrifice sana kwa kuleta bomba Tanzania, hilo bomba kiuhalisia lilitakiwa lipite Kenya but wao wakalileta kwetu na pia kuna benefits kubwa tunazipata kwa waganda kutumia bandari za Tanzania badala ya za Kenya hivyo na sisi ni lazima tuoneshe mkono wa shukrani
Ndo umuabishe waziri wako?
 
Nimeshangazwa na kauli hii ya Mh Rais, kuita msimamo wa mteule wake Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje, kuwa NONSENSE, tena hadharani.

Nimesikitishwa na kauli hiyo kwa sababu mbili.

Moja, public reprimand kwa kiongozi mwandamizi, sidhani kama ni utawala bora.

Na hii naanza kuhisi ile power is getting to the head, and power corrupts.

Pili, nimesikiliza arguments za Mkenda, though pompous, kuna relevance pale.

Argument ni kuagiza sukari kama kuna shortage, si kwa matakwa ya wafanyabiashara.

Sasa wale wawekezaji wanaovipanua viwanda ili ku boost uzalishaji wa sukari, wale ni nonsense?

All in all, Mkenda anapaswa kujiuzulu ku-save face.
Unaweza kuta kikao cha pamoja,mkubwa na wasaidizi kina siku kadhaa hakijakaa.
Mambo muhimu hayajajadiliwa,unaweza kuta kauli na matamko mengine sio msimamo wa Serikali.!!
 
The buck stops with Madame President, and it has rolled the wrong way.
 
Back
Top Bottom