Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Inabidi umwambie na Majaliwa Kasim Majaliwa maana yeye PM na Mkenda waliongea lugha sawa
 
..Waziri hajazuia uagizaji wa sukari.

..hata mwaka huu kuna sukari ambayo imeingia nchini kutoka Uganda.

..Tatizo ni taarifa za uongo toka kwa Raisi Museveni.
 
Ukimaliza kutoa povu lako la kutokujielewa na uelewa finyu kwenye intra country trading issues kalale. Rubbish

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hapa tatizo ni Mkenda kuambiwa Hana SENCE? Ukweli Kati ya mawaziri si Mkenda peke yake ambaye Hana SENCE, wako wengi tu akiwemo wa Fedha, wa Biashara, wa Maliasili, wa Madini na kubwa Lao Afya.

Majority is zero including Head of state
 
TPC inamilikiwa na beberu, sukari yake 90% inatoka nje, kwa nini kusiwe na uhaba.
 

Huyu mama haijui management kbs yaani Mungu atuhurumie sana mtu wa calibre yake ndiyo anakuwa mkuu wa nchi kweli. Hiyo kauli aliyoitoa in broad sense amejinanga mwenyewe kwamba serikali yake ni 'nonsense'
 
Crap!
Protectioism ni sera ya kuzuia kabisa bidhaa toka nje zisiingie nchini.
But it does not make sense kuingiza sukari yenye bei chee wakati wazalishaji wa ndani wapo na wanafanya kazi.
Serikali ile matapishi yake yenyewe na wanajua kuwa bei ya sukari inayozalishwa nchini imechangiwa na kodi lukuki inazoziandama sekta binafsi na viwanda.
Tusiruke majivu na kuishia kwenye moto.
 
Rudia tena kusoma ulichoandika.............if it doesn't make sense kwako kuingiza sukari ya bei chee, kwa sisi wananchi tusio na na kipato kikubwa it makes a helluva lot of sense. Why wazalishaji wa ndani wapewe preferential treatment...........kwanini sukari tu? Mbona haihusu viwanda vingine vinavyozalisha hapa nchini? Nadhani umesikia video hapo juu ( courtesy of Joka Kuu), kwamba wengi waliobinafsishiwa hivyo viwanda walikuwa ni watumishi waandamizi serikalini. Kwa hiyo walitengeneza mazingira ya viwanda vyao kulindwa , na uagiza wa sukari vibali wanakuwa wanapewa wao.............kwanini?
 
Bidhaa yoyote duniani inaagizwa na kuingizwa sokoni kama kuna DEMAND. Wanaojua hali ya demand na supply ni washiriki wa soko, yaani wauzaji na wanunuzi, nje ya hapo ni siasa tupu.
Mfanyabiashara anaagiza bidhaa at his own risk, akiamini ataiuza apate faida, huku pia akijua uwezekano wa kushindwa kuiuza (na kupata hasara), lakini anaingia kwa kuwa ameshapima na kuona uwezekano wa faida ni mkubwa zaidi.
Sasa wewe serikali unapokataza mfanyabiashara kuzungusha pesa yake halali, unafanya hivyo kwa faida ya nani?
Ukizuia mfanyabiashara kuagiza sukari kutoka nje, na matokeo yake wananchi wa kawaida wakauziwa sukari ya ndani ya nchi kwa bei kubwa kuliko ile ya nje, umemsaidia nani? Kama serikali inataka nafuu ya maisha kwa wananchi wake, ingeboresha mazingira ya gharama za uzalishaji ili wananchi wapate sukari ya ndani kwa gharama nafuu kuliko sukari ya nje, tofauti na hapo ni kuumiza wananchi.
Na hata sukari ya ndani ikishakuwa bei rahisi, bado wanaotaka sukari ya nje wana haki ya kuinunua hata kama wanalipa ghali kwa sababu pesa wanazotumia kununua hiyo ya bei ghali ni za kwao; ni utashi wao na choice yao kununua kitu wanachotaka. Hizo ndizo dynamics za soko.
Mchele pale sokoni Tandale unauzwa sh 1,700 kwa kilo, lakini bado kuna watu wanaununua katika supermarkets kwa sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo. Ni chaguo lao, kwanini tuwaingilie? Bidhaa ziletwe sokoni wateja wachague wanachotaka.
 
Ukishangaa ya sukari na kutaka kupewa mlungula airport sijui huko kwenye umeme ndio tusemeje, watu wa sampuli ya akina Prof ndio wanasiasa wetu hawaitaki, naona fursa kwa wapiga dili zinazirudi kurudi, wale wanaojifanya wazalendo na wana uchungu na nchi hii huo ndio mwanzo wa kupuuzwa, kuhusu suala la sukari kuna janja nyingi nyuma ya pazia na M7 kaamua makusudi kudanganya, nimemsoma balozi Ami Mpungwe ambaye ni mwenyekiti wa KSC kuwa si kweli kuwa sukari kutoka Uganda haiagizwi na ametoa mfano sukari ambayo viwanda vimenunua kutoka Uganda hivi karibuni, tulidhani tunapokea shule kumbe kuna jambo .
 
Tatizo ni uwezo wa viwanda kuzalisha sukari au malighafi(miwa) ndiyo hatuna/tunazalisha kwa kiwango kidogo?
 
Uko sahihi kwa kiwango kikubwa
Lakini naye mama haeleweki kama ni mamalia au ndege.Leo anafukia sera za mwendazake kesho anatetemeka yupo Chato kuzindua shule ya msingi...
Anataka kufuta maujinga ya jiwe huku akiliogopa genge la Chato..
Asimame sehemu moja aache kutuchanganya
 
Si tunaagiza sukari kwa ajili ya shortage, shortage ipo haipo, kama ipo why isiagizwe?
Hao wanaotanua, watanue tu, ikitosheleza tutaacha kuagiza

Acheni bidhaa zifurike mtaani bei ishuke.

Hii tabia ya kupendelea, matokeo yake ndio haya.
 
Very sad,

Hivi hawa communicate ndani kwa ndani mpaka wadhalilishane kwenye media ??....kuna udhaifu kwenye mawasiliano yao
 
Ndo umuabishe waziri wako?
 
Unaweza kuta kikao cha pamoja,mkubwa na wasaidizi kina siku kadhaa hakijakaa.
Mambo muhimu hayajajadiliwa,unaweza kuta kauli na matamko mengine sio msimamo wa Serikali.!!
 
Unaweza kuta kikao cha pamoja,mkubwa na wasaidizi kina siku kadhaa hakijakaa.
Mambo muhimu hayajajadiliwa,unaweza kuta kauli na matamko mengine sio msimamo wa Serikali.!!
The buck stops with Madame President, and it has rolled the wrong way.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…