Nimeshangazwa na maboresho makubwa yaliyofanyika uwanja wa ndege wa KIA, unavutia sana

Requal

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2020
Posts
1,025
Reaction score
1,923
Sijatua hapa KIA tangu 2016. Jana nimetua hapa kwa mara nyingine. Kama ningezibwa macho nikasafirishwa mpaka hapa then nikaachiwa nione bila matangazo na mabango yaliyoko hapa kwa haraka haraka nisingeweza kutambua kama pale nilipokuwa ni KIA, asimilia kubwa
ya miundombinu imeboreshwa na imebadilika kutoka uhalisia wake wa awali kwa kiwango cha juu sana.

Pongezi kwa wote mliohusika kuleta mabadiliko haya, Japo sikukuta ndege kubwa pale uwanjani lakini nina uhakika madege makubwa kama yale ya Qatar yanaweza kutua pale kwa sasa.

Vyumba vya kupumzika wageni vimeongezwa na vinapendeza kwa ujumla wake vyote kwa upande wa wageni wa nje na ndani.

Ombi langu kwa serikali ruhusuni makampuni mengine ya ndege mfanye nayo ushindani hasa kwa safari za ndani, ATCL wana bei kubwa sana na timetable zao hazieleweki, ratiba inaweza kuonesha mnaondoka saa 4 asubuhi, mkaondoka saa 4 unusu au saa 5 na dakika zake.

Hongereni kampuni ya KADCO mnaoendesha uwanja wa ndege wa KIA.
 
Mkuu Kuna kitu gani kipya hapo KIA,labda Mimi ninapopita hapo macho yangu yanakuwa yanaumwa
Kuna mabadiliko mengi sana mkuu tangu nitue hapa mara ya mwisho 2016 na kama wewe unasafiri mara kadhaa naamini utakuwa umeyaona.
 
Macho yako tu mkuu, Ila hapo papo kawaida sana.
 
Naunga mkonohoja, serikaliiruhusu makampuni mengine ya ndege yafanye kazi hapa nchini kwenye hizi route za ndani
 
kabisa mkuu,ATCL wana bei za juu sana
 
Tuwekee hata kapicha mkuu na sisi tufaidi mandhari nzuri kabisa ya Kiwanja chetu cha ndege cha watalii
 
Naunga mkonohoja, serikaliiruhusu makampuni mengine ya ndege yafanye kazi hapa nchini kwenye hizi route za ndani
Kukosekana kwa ushindani wa ndege za abiria za ndani zinafanya bei iwe kubwa kwa air tanzania
 
Pongezi kwa wote mliohusika kuleta mabadiliko haya, Japo sikukuta ndege kubwa pale uwanjani lakini nina uhakika madege makubwa kama yale ya Qatar yanaweza kutua pale kwa sasa.

Dah...….aisee…..basi huna habari za KIA muda sana……...
Pale panatua…..Ethiopian….Qatar......Turkish.....KLM.....Condor....FlyDubai(ndugu yake Emirates)……..na jamaa yetu tuliyempiga pini…...
Private jets ndio acha kabisa…...za kumwaga…..

Preta…...safarini Namanga kuchunga KQ isikatize…...…..
 
mkuu nadhani utakuwa hujanisoma vizuri

ndicho nilichomaanisha
 
Kia panatia aibu Sana ule uwanja unahitaji maboresho makubwa sana
 
Dah...….aisee…..basi huna habari za KIA muda sana……...
Pale panatua…..Ethiopian….Qatar......Turkish.....KLM.....Condor....FlyDubai(ndugu yake Emirates)……..na jamaa yetu tuliyempiga pini…...
Private jets ndio acha kabisa…...za kumwaga…..

Preta…...safarini Namanga kuchunga KQ isikatize…...…..
Unaelekea Namanga dah! Tumepishana mkuu mi ndo naelekea Arusha mjini
 
Back
Top Bottom