Nimeshawasilisha barua ya mashtaka dhidi ya Rais Samia kwenye mahakama ya The Hague ICC

Mkuu hongera, lakini hii mahakama imewahi kumfunga Rais gani?
Bado mpaka sasa isipokuwa viongozi wa vita yaani warlords kama Charles Taylor, na raisi wa Serbia na ilokuwa Yugoslavia Slobodan Milosevic. Pia aliekuwa raisi wa Philippines bwana Duterte.

Hata hivyo utaratibu wao ICC ni kwamba kwanza huanza na uchunguzi wa awali yaani "preliminary examination".

Malengo halisi ya hatua hii ni kushinikiza serikali ya nchi husika ifanye uchunguzi wa madai yalotolewa yenyewe kwa watu wote walohusika kufanya uhalifu huo ndani ya mipaka ya nchi husika.

Baada ya hapo ifisi ya mwendesha mashtaka (Office of The Prosecutor) itaamua kuanza uchuguzi (investigation) kulingana na kiwango cha ushahidi na vielelezo vyote ambavyo vyakidhi matakwa ya mkataba wa Rome.
 
Kama tukio la tarehe 29 linahitaji uchunguzi gani na kila kitu kipo wazi? ile mahakama huwa siielewi hata kidogo
 
Nimekupata mkuu, ila huo ndo utaratibu.

Ofisi ya mwendesha mashtaka huanza kazi hiyo ya "preliminary examination" baada ya kukusanya taarifa kutoka kwa watu binafsi, makundiya watu,nchi fulanifulani, taasisi mbalimbali na zile taasisi zisizo za kiserikali (NGOs).
 
JF ipo thread Moja yenye collection ya video zote za mauaji jukwaa la siasa.
 
Why don’t you form your own NGO accurate information and build a case.

Kuangalia hizi ‘gruesome’ images inatosha especially out of the blue. Kama ni salamu tumepata huyu ajuza na genge lake la wahuni ni katili.

Lakini hizo images tumechoka with nightmares, tayari tumeamini hili janamke ni lishetani.

Hizo picha kwa JF ziwe na mada yake na kwengine kuwe na utaratibu wa kuzikusanya kwa ushahidi wa mahakama yeyote duniani (she deserves to get there) hila images za kustukia kwa wengine tumeshaumia vya kutosha.

Source moja itawaruhusu wenye vifua vya kuangalia distributing images na wenyewe kupata haki ya kuona kinaga ubaga ushenzi wa Samia.
 
Ushahidi umo humu JF Kwa mpangolio ulionyooka…wauchukue tu na kuupeleka…GE2025 - Compilation: Picha na Video za Mauaji na mashambulizi yaliyofanywa kwa Raia nchini Tanzania wakati wa Maandamano Oktoba 29, 2025
 
Hao ndio ma BICHWA KOMWE - yenyewe sasa
 
Mkuu hongera, lakini hii mahakama imewahi kumfunga Rais gani?


Mnamo Machi 11, 2025, rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte alikamatwa na Polisi wa Kitaifa wa Ufilipino na Interpol katika Operesheni chini ya hati ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) akishtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusiana na vita vya dawa za kulevya Ufilipino.

Anaodaiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinadamu wa mauaji na jaribio la mauaji, unaodaiwa kufanywa katika eneo la Jamhuri ya Ufilipino kati ya 1 Novemba 2011 na 16 Machi 2019 katika muktadha wa kampeni ya 'vita dhidi ya dawa za kulevya'




Majaji wa ICC wanakataa kumwachilia Rais wa zamani wa Ufilipino Duterte, kwa sababu ya hatari yakutokomea ulimwenguni (Flight risk)

Oktoba 10, 2025 7:54 PM EST

HAGUE, Uholanzi (AP) - Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu siku ya Ijumaa walikataa ombi la Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte la kuachiliwa kutoka kizuizini, wakiona kuwa kuna uwezekano wa kukataa kurejea mahakamani na anaweza kutumia uhuru wake kuwatisha mashahidi.

Source: BPS News.

Source: Amnesty.org.uk [Amnesty international Press release]

Source: https://www.icc-cpi.int/news/situation-philippines-rodrigo-roa-duterte-icc-custody
 
Mkuu naona umetembea na Chat Gtp na Ai ,nakushauri achana na ayo mambo tujenge nchi kwa sasa..!!
Wakati nasoma miaka hiyo ambayo hata weye ulikuwa hujazaliwa bado na hizo Apps hazikuwepo.

Usipende kutumia sana hizo zitakutoa akili.

Halafu wasema tujenga nchi kwa sasa, nchi itajengwa vipi ikiwa vijana ambao ni nguvukazi na taifa la kesho ndo wauawa kama kuku?

Nchi hujengwa kwa misingi ya kuheshimu haki za binadamu haki za raia na kuheshimu katiba ambayo nayo imesiginwa.
 
Mkuu, nipo kwenye hatua za kati za kuweka "News Feeder" au Aggregator ambayo itakuwa "dedicated" kwa ajili ya mambo kama haya. Nipo kwenye mazungumzo na host ambayo itakuwa katika moja ya nchi rafiki.Watu wataweza kutuma taarifa humo na zitapangwa kulingana na siku ya tukio na tarehe.

Naangalia uwezekano wa kutumia RSS (Really Simpe Syndication) pekee kutoka kwenye vyanzo vilivyopo tiyari kama JF au pia kuwa na feeder ya pili ambayo itakuwa na habari nyingi za uchambuzi "from scratch" hii yaitwa RSS feed generator lakini ni lazima utumie mafaili yenye XML code.

Hata hivyo zipo good news kwenye suala la kutuma picha na video za matukio kama yalotokea tarehe 29 na 30 Octoba kwamba ipo App iitwayo Eye Witness App ambayo yapatikana hapa: New Resource: Practical guide on when to use the eyeWitness to Atrocities app

App hii ipo katika Google Store hivyo kuwa rahisi kupatikana kwa watumiaji wengi wa simu za Android.

Maelekezo yote ya namna ya kutumia App hii yapatikana hapa : https://www.eyewitness.global/documents/2023-eyeWitness-new-resource-launch.pdf

Hivyo hili suala si la kulifumbia macho ni lazima serikali zetu za kiafrika zijifunze kwa lazima kuheshimu haki za binadamu na kufuata sheria zote za ndani na sheria za kimataifa.
 
Ulikuwa wapi siku hyo shoga? Dudu ilipanda kweli??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…