Kiranga nimejaribu kufuatilia hoja zako kuhusu Regia, nasikitika kuwa zina harufu ya wivu. Ukiacha hivi vimaneno vya kiingereza ulivyoweka hapa, basi huna hoja kabisa. Kwanza naamini nivi vimaneno umevikariri, sidhani kama unaelewa maana yake...
Labda ututhibitishie kuwa unamfahamu Regia zaidi ya huku kwenye internet, lakini huwez sema mtu hana initiative kwa sababu amekubali ushauri aliyopewa, au hana exposure (husemi kwa nini).
Lakini nahisi pia kwamba inaweza kuwa unatumiwa na baadhi ya wapinzania wa Regia. Kama ndivyo, wasiliana na Malaria sugu, na Tumain wakuambie wao wanalipwa kiasi gani isijekuwa unadhulumiwa ndugu yangu...
Haya ndiyo yale yale ya mtu yeyote anayekupinga ni fisadi.
Halafu inachekesha una mention Kiingereza kama issue wakati Kiingereza ni lugha tu, na ukianza habari za "ukiacha kiingereza..." nakuona wewe ni mmoja wa wale limbukeni wanaofikiri kujua Kiingereza ni kuelimika, maana umeona Kiingereza ni issue tayari. Tayari ushajionyesha limbukeni asiyejua kuchambua mchele na chuya.
Kwa sababu CCM inafanya vibaya, basi mpinzani yeyote akija poa tu, hata kama gendaeka lisilopungwa wala kupigwa ubani.
Mimi siwezi kuwa na wivu kwa sababu sina mpango wa kuingia bongo politics kwenye elected office, in fact kwa mwendo huu kuwa elected official ni certificate kwamba umetoa rushwa na kufanya fyongo fulani somewhere, I don't want that on my resume, kama kujenga nchi kuna namna nyingi tu.Sasa wivu utoke wapi ndugu yangu?
Mara nyingine mtu anapokaa na computer yuko mtandaoni, no speechwriter, no proofreader, no election committee, ndipo
unapoona rangi zake za kweli kuliko hata kukaa naye uso kwa uso. Computer inatupa a false sense of privacy, unaandika
mawazo yako kwa mamilioni ya watu wenye mtandao wayasome, lakini huwaoni, wewe unaona kama unaandika katika computer yako tu. Kwa hiyo mtu anayemfuatilia Regia hapa anaweza kujua her innermost thoughts pengine vizuri kuliko hata peers wake ambao hawamfuatilii mtandaoni.
Nimesema hana tact kwa sababu mtu kama hutaki kujitangaza hujitangazi, kama unataka kujitangaza unajitangaza, anything in between is controversial. Ukitaka kujitangaza nusu nusu kama alivyoanza huyu dada watu makini watataka habari zote, usipowapa utaonekana unaficha kitu au hujiamini.Ndiyo mana ikabidi akubali forces of reason. Huwezi kutaka kuuzia wtu mbuzi kwenye gunia usawa huu.
Kwa kutoanzisha mambo, kwa kutojitaja, na vibaya zaidi kwa kutotupa sababu za kutojitaja amejionyesha hana initiative. Anakuwa reactive, anaacha kina Kiranga wa dictate mambo anayotakiwa kuyafanya, anakosa control ya campaign yake mwenyewe katika uwanja ambao alitakiwa awe na control kubwa sana kwa sababu ni member kitambo hapa, sasa kama hii
part ndogo tu ya online anashindwa kufanya mambo kwa initiative, kuandika tu hapa, akipelekwa jimboni kuhangaika na
logistics huko ataweza ?
Hana exposure kwa sababu anafanya mistakes za kitoto.Haelewi ukiwa unataka kuingia katika public service, hususan kama
uko upinzani, huwezi kuwa prima donna,huwezi kuwa msiri msiri, utakuwa unawapa watu image ambayo ni mbaya pengine kuliko hali halisi, unatakiwa uwasikilize watu, unatakiwa uheshimiane na watu.Sio mtu anakupa tough love na constructive
criticism wewe unamwambia "nenda kabebe box huko". Inaonekana hajui kwamba kusema hivyo ana alienate watu wengi tu ambao hata hawakuwa kwenye mjadala naye, na anajionyesha kwamba hafikirii sana, anasema kinachomjia kichwani. Anajionyesha hana tofauti sana na kina Sophia Simba wanaopata vyeo kwa networking lakini si kwa merit.Anajionyesha hana tofauti na kina Kikwete wanaosema wafanyakazi wasiotaka kumpigia kura hazihitaji kura zao. Kiongozi mzuri hawezi kufanya mistakes hizi.
Halafu hata haelewi kwamba ubunge unataka talent, anasema mtu yeyote tu anaweza kuwa mbunge. No wonder yeye kajaribu, kwa sababu angejua qualities za mbunge asingethubutu kujaribu, angetafuta exposure zaidi.Mtu anachangiwa na watu, anashangaa eti kwa sababu watu hawajui personally, anajionyesha kashazoea mumo wa "nipe nikupe" na kuchangiana kwa kujuana, akija mtu kumchangia kwa kuamini katika ideals za chama, huyu dada anashangaa, sijui hajawahi kuona hili? Exposure ndogo, communication skills ndogo, stretegy hamna, tact zero.No wonder kakimbia hapa.
Uzuri wangu mimi najaribu kuwa objective na mkweli kwa mambo ninavyoona mimi as much as posible.Ndiyo maana sina chama wala ushabiki kwa mtu, mimi naangalia uwezo, kwa hiyo CHADEMA wakichemka nawa blast, CCM wakichemka nawablast, CHADEMA wakifanya vizuri nawasifu, vile vile CCM ingawa napata tabu kupata cha kuwasifu.
Tatizo watu wanatumia emotions na irrational thinking katika kutetea mambo.Hawatumii rational thinking. Mjadala wa siasa
unageuka kama unazi wa mpira, it is us against them and you better say only nice things about us, because if you don't we
will lump you with them and we don't care about your rational arguments, all we care about is the sport of politics, we
are charged and you better not cross us, even if you have sound arguments which we can use to self correct our conduct
Mambo ya imani za siasa yanageuka dini, wagombea wanageuka mitume wasiokosea.
As many of you know, mimi siamini hata dini, kwa hiyo itabidi muelewe tu kwamba siasa na vyama vyake haviwezi kuni
impress mimi kiasi cha kutupa objectivity yangu isiyofungamana na upande wowote. Huwezi kusema natumiwa na wapinzani wake Regia wakati hata wao nawaandama, tena wengine nimewafuta kama unworthy of discussion, bora hata huyu Regia yupo katika radar zangu namzungumzia katika matumaini kwamba anaweza kujifunza machache na kuongeza exposure yake ndogo.