Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Nakusifu dada ayngu Regia kwa kumpotezea huyu mlevi...

Hao waliomnunua waangalie vizuri wanakoelekeza fedha zao. This is not a right guy...
 
Hivi kwa nini wa tanzania ni wepesi wa kutumia offensive language iliyo wazi?!
 
Mjadala unakuwa mzuri sana unapojikita katika kukata issues kuliko kumjadili mtu binafsi. Huyu dada anahitaji kuungwa mkono na sio kumkatisha tamaa kwasababu udhaifu unauona wewe kwake katika mjadala huu, ndio kadhalika udhaifu huo huo tunaouona kwako pia katika mjadala huu.Ni sawa na kumkosoa mtu kuwa kaandika kiswahili kibovu wakati na wewe ukosoaji wako una makosa ya kiswahili(ila wewe huyaoni na huyakubali hata ukionyeshwa)

Kwa ujumla hakuna aliye mkamilifu, suala la msingi ni kupeana moyo maana hatuna shaka na uzalendo wa huyu dada katika kutaka kulitumikia taifa. Wakati fulani ni vema kuweka pembeni chuki, kinyongo au wivu juu ya mtu na kuangalia njia ya kusaidiana katika yale tunayoyaona ni udhaifu kwa kutoa ushauri jinsi ya kuondoa hayo mapungufu
 
"offensive language" "iliyo wazi" ndio ikoje hiyo?

kama hiyo 'mlevi' , 'gay', 'lesbian'............na maneno mengine yanayochukuliwa kuwa matusi kwenye jamii husika

offensive language isiyowazi..................ni ile isiyokuwa defined kama tusi katika jamii husika lakini mlengwa aka dhani/fahamu kuwa ametusiwa......mfano hapa labda kama shyrose alipoulizwa kama anatafuta mume


note: hii sijaitoa kwenye kamusi, ni mtazamo wangu tu wa aina ya offensive languages
 
offensive language isiyowazi..................ni ile isiyokuwa defined kama tusi katika jamii husika lakini mlengwa aka dhani/fahamu kuwa ametusiwa......mfano hapa labda kama shyrose alipoulizwa kama anatafuta mume

Hapa kama unakubali kuwa Shyrose alitusiwa. Sasa ule ubishi wako kwenye ile thread ulikuwa wa nini? Gaijin bana...you are all over the place.....:love:
 
muahahaha .................nisome uzuri 'Mlengwa atadhani katusiwa' :tongue:.................mimi sikudhani kuwa katusiwa labda lakini bi shy yeye alidhani hivyo ndo maana akarusha ngumi!
 
muahahaha .................nisome uzuri 'Mlengwa atadhani katusiwa' :tongue:.................mimi sikudhani kuwa katusiwa labda lakini bi shy yeye alidhani hivyo ndo maana akarusha ngumi!

Wewe umeshapata mume? Au bado unakazana na mavitabu?
 
mmmmh kiranga kama mashambulizi yako umeyaelekeza sipo hivi!?

Nafikiri huwezi kumtaka mtu abadilike 'uwezo' wake........tukichukulia kuwa ameweka juhudi zote lakini amefika kuwa na Uwezo huo unaouona( hana exposure, hajui kujieleza, akiingia kwenye debate analia lia, ...........- if indeed this is true) basi kosa ni la chama chake.

Nafikiri tunaweza kuilaumu chadema kwa
kutuwekea mtu below par (if she is) labda kwa kuwa hawakuwa na choice nyengine kwa sababu she is the best among waliojitokeza kuwania nafasi hiyo
(hapa pia linakuja suala la how big was their sample. best amoung two? the only contender? ............)

and if you want to stretch the point unaweza kutoa lawama kwa watu wote wa Kilombero, kwa kushindwa kutoa mgombea bora zaidi ya huyo aliyejitokeza sasa

in short ni kuwa you cant blame a machine for its low COP but the maker for not making a better machine


Be careful
Mix with yours
 
Ngabu kwani kupata mume lazima?

Wenzio wakija tunapindisha mjadala hapa waweza tumeza .............hebu mie!:love:
 
kapwani ................maelezo yako hayajajitosheleza. Hebu toa ufafanuzi ikiwezekana
 
Kiranga nimejaribu kufuatilia hoja zako kuhusu Regia, nasikitika kuwa zina harufu ya wivu. Ukiacha hivi vimaneno vya kiingereza ulivyoweka hapa, basi huna hoja kabisa. Kwanza naamini nivi vimaneno umevikariri, sidhani kama unaelewa maana yake...

Labda ututhibitishie kuwa unamfahamu Regia zaidi ya huku kwenye internet, lakini huwez sema mtu hana initiative kwa sababu amekubali ushauri aliyopewa, au hana exposure (husemi kwa nini).

Lakini nahisi pia kwamba inaweza kuwa unatumiwa na baadhi ya wapinzania wa Regia. Kama ndivyo, wasiliana na Malaria sugu, na Tumain wakuambie wao wanalipwa kiasi gani isijekuwa unadhulumiwa ndugu yangu...

Haya ndiyo yale yale ya mtu yeyote anayekupinga ni fisadi.

Halafu inachekesha una mention Kiingereza kama issue wakati Kiingereza ni lugha tu, na ukianza habari za "ukiacha kiingereza..." nakuona wewe ni mmoja wa wale limbukeni wanaofikiri kujua Kiingereza ni kuelimika, maana umeona Kiingereza ni issue tayari. Tayari ushajionyesha limbukeni asiyejua kuchambua mchele na chuya.

Kwa sababu CCM inafanya vibaya, basi mpinzani yeyote akija poa tu, hata kama gendaeka lisilopungwa wala kupigwa ubani.

Mimi siwezi kuwa na wivu kwa sababu sina mpango wa kuingia bongo politics kwenye elected office, in fact kwa mwendo huu kuwa elected official ni certificate kwamba umetoa rushwa na kufanya fyongo fulani somewhere, I don't want that on my resume, kama kujenga nchi kuna namna nyingi tu.Sasa wivu utoke wapi ndugu yangu?

Mara nyingine mtu anapokaa na computer yuko mtandaoni, no speechwriter, no proofreader, no election committee, ndipo
unapoona rangi zake za kweli kuliko hata kukaa naye uso kwa uso. Computer inatupa a false sense of privacy, unaandika
mawazo yako kwa mamilioni ya watu wenye mtandao wayasome, lakini huwaoni, wewe unaona kama unaandika katika computer yako tu. Kwa hiyo mtu anayemfuatilia Regia hapa anaweza kujua her innermost thoughts pengine vizuri kuliko hata peers wake ambao hawamfuatilii mtandaoni.

Nimesema hana tact kwa sababu mtu kama hutaki kujitangaza hujitangazi, kama unataka kujitangaza unajitangaza, anything in between is controversial. Ukitaka kujitangaza nusu nusu kama alivyoanza huyu dada watu makini watataka habari zote, usipowapa utaonekana unaficha kitu au hujiamini.Ndiyo mana ikabidi akubali forces of reason. Huwezi kutaka kuuzia wtu mbuzi kwenye gunia usawa huu.

Kwa kutoanzisha mambo, kwa kutojitaja, na vibaya zaidi kwa kutotupa sababu za kutojitaja amejionyesha hana initiative. Anakuwa reactive, anaacha kina Kiranga wa dictate mambo anayotakiwa kuyafanya, anakosa control ya campaign yake mwenyewe katika uwanja ambao alitakiwa awe na control kubwa sana kwa sababu ni member kitambo hapa, sasa kama hii
part ndogo tu ya online anashindwa kufanya mambo kwa initiative, kuandika tu hapa, akipelekwa jimboni kuhangaika na
logistics huko ataweza ?

Hana exposure kwa sababu anafanya mistakes za kitoto.Haelewi ukiwa unataka kuingia katika public service, hususan kama
uko upinzani, huwezi kuwa prima donna,huwezi kuwa msiri msiri, utakuwa unawapa watu image ambayo ni mbaya pengine kuliko hali halisi, unatakiwa uwasikilize watu, unatakiwa uheshimiane na watu.Sio mtu anakupa tough love na constructive
criticism wewe unamwambia "nenda kabebe box huko". Inaonekana hajui kwamba kusema hivyo ana alienate watu wengi tu ambao hata hawakuwa kwenye mjadala naye, na anajionyesha kwamba hafikirii sana, anasema kinachomjia kichwani. Anajionyesha hana tofauti sana na kina Sophia Simba wanaopata vyeo kwa networking lakini si kwa merit.Anajionyesha hana tofauti na kina Kikwete wanaosema wafanyakazi wasiotaka kumpigia kura hazihitaji kura zao. Kiongozi mzuri hawezi kufanya mistakes hizi.

Halafu hata haelewi kwamba ubunge unataka talent, anasema mtu yeyote tu anaweza kuwa mbunge. No wonder yeye kajaribu, kwa sababu angejua qualities za mbunge asingethubutu kujaribu, angetafuta exposure zaidi.Mtu anachangiwa na watu, anashangaa eti kwa sababu watu hawajui personally, anajionyesha kashazoea mumo wa "nipe nikupe" na kuchangiana kwa kujuana, akija mtu kumchangia kwa kuamini katika ideals za chama, huyu dada anashangaa, sijui hajawahi kuona hili? Exposure ndogo, communication skills ndogo, stretegy hamna, tact zero.No wonder kakimbia hapa.

Uzuri wangu mimi najaribu kuwa objective na mkweli kwa mambo ninavyoona mimi as much as posible.Ndiyo maana sina chama wala ushabiki kwa mtu, mimi naangalia uwezo, kwa hiyo CHADEMA wakichemka nawa blast, CCM wakichemka nawablast, CHADEMA wakifanya vizuri nawasifu, vile vile CCM ingawa napata tabu kupata cha kuwasifu.

Tatizo watu wanatumia emotions na irrational thinking katika kutetea mambo.Hawatumii rational thinking. Mjadala wa siasa
unageuka kama unazi wa mpira, it is us against them and you better say only nice things about us, because if you don't we
will lump you with them and we don't care about your rational arguments, all we care about is the sport of politics, we
are charged and you better not cross us, even if you have sound arguments which we can use to self correct our conduct

Mambo ya imani za siasa yanageuka dini, wagombea wanageuka mitume wasiokosea.

As many of you know, mimi siamini hata dini, kwa hiyo itabidi muelewe tu kwamba siasa na vyama vyake haviwezi kuni
impress mimi kiasi cha kutupa objectivity yangu isiyofungamana na upande wowote. Huwezi kusema natumiwa na wapinzani wake Regia wakati hata wao nawaandama, tena wengine nimewafuta kama unworthy of discussion, bora hata huyu Regia yupo katika radar zangu namzungumzia katika matumaini kwamba anaweza kujifunza machache na kuongeza exposure yake ndogo.
 
..........Hongera my sista kwa kuwa muwazi na kuamua kutoa jina lako kamili .Kila la heri......hakika utafanikiwa tu kuingia mjengoni.

Samahani sikutaka kukukoti wewe imetokea faulo
Regia..to what extent unaijua KILOMBERO unayotaka kuiwakilisha?
mix with yours
 
Hapa kama unakubali kuwa Shyrose alitusiwa. Sasa ule ubishi wako kwenye ile thread ulikuwa wa nini? Gaijin bana...you are all over the place.....:love:

Ha ha ha ha umemshtukia>

The guy yuko double standard(ized) kuliko maflip floper wote uliowahi kusikia (dont mention John Kerry please).
 
Mimi naanzisha petition kwa kiranga kuingia kwenye siasa ili aweke mfano wa nini wanasiasa wanatakiwa kufanya.
 
Ha ha ha ha umemshtukia>

The guy yuko double standard(ized) kuliko maflip floper wote uliowahi kusikia (dont mention John Kerry please).

sikutegemea kama atatokea mtu akashindwa kufahamu maana ya neno KUDHANI!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom