DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu ni umeacha hela kizembe, mimi ilishawahi kunikuta na nilifanikiwa kwanza document zinazotakiwa siyo passport tu kama una kitambulisho cha mpigakura na nida utapata hela yako muhimu taharifa za kitambulisho ziendane na taarifa zilizopo 1xbet, namba ya simu siyo lazima iwe na majina sawa yaliyopo 1xbet, kama unahitaji maelezo zaidi uliza mkuu hawa watu nina uzoefu sana nao.
 
Mkuu waone bodi ya michezo ya kubahatisha wakusaidie kuclaim fedha zako. Akishindwa, waburute mahakamani hao wapuuzi.
 
Mama Samia Suluhu Hassan Rais wetu kipenzi cha watanzania na vijana wote Tanzania tunakuamini na kukupenda sana mama yetu tunaomba msaidie huyu kijana kwenye hii changamoto yake apewe pesa yake ikibidi muongezee na nyingine apate mtaji wa kufungua genge la kuuza mboga mboga na nyanya ntoreπŸ™πŸ™
 
Hapo mtafute wakili mmoja anaitwa kibatala then atakupa vijana wake wakusimamie hapo unaweza vuna hata 50m+ ila kama kuna ukweli ndani yake kupitia mkwamo huo na maelezo yako kuna kosa la utapeli,kosa la zuruma,kupotezewa muda kwaiyo huwezi kosa fidia maana kamari ni biashara kwaiyo wamenufaika na pesa zako zaidi ya 2yrs+
 
huyu mleta mada tuko nae tunabishana lakini hatumjui
leta mada na id yako ili uweze kujitetea
 
Nilisha withdraw
 
Kwa slip zangu zinavyochanika ningekuwa mimi nisingepunguza hata hiyo 7

Mkeka wangu ungelipwa kama nilivyo shinda.

Kwenye hili tungefika mbali, ningesimamisha mitikasi yangu kushughulika na hawa matapeli.
 
Kumbuka account Nina zaidi ya mwaka nachezea
Hakuna makampuni yan rules ngumu kama kampuni la 1xbet la kirus na makampuni yaliyo copy hilo kampuni mfano paripesa yale yana masharti kibao sana.

Ukicheza kidogo huna akaunti..yani wale wakivurugwa huna akaunti nenda nao taratibu tu.
 
Pole sana mkuu. Tafuta wakili anayejitambua akusaidie kupata chekeli zako. Makampuni mengine ni matutusa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…