DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hilo suala la kuombwa analijua yeye na waliyekubaliana naye kwasababu kama ni rushwa nikinyume na utaratibu na serikali itakosa mapato yanayozidi milion 3 labda waseme sababu ni kuwa either kuna fraud ambayo ipo nje ya mleta mada hivyo hiyo milion 3 ni kifuta jasho ambapo kimsingi hapaswi kuepewa maana mkeka wake haujapewa ushindi. Lakini hoja yakuwa kampuni imeona hiyo milion 27.7 kuwa ni nyingi na kuwa wamlipe milion 3 sio sababu sahihi wanatakiwa kumlipa kwa lazima
Na kwa nini yote hayo yatokee kama mhusika ana haki ya ushindi 😂?
Kwamba TGB na Pigabet wajinga sana mpaka wapoteze muda wao kukaa na mtu asiyestahili kulipwa?
 
Una uhakika gani? Je kama aliscreenhot mapema kama ushahidi wa lolote linaloweza kutokea? Halafu kumbe hujaelewa mtoa mada anazungumzia kufutwa kwa mkeka baada ya kushinda na sio wakati game zikiendelea
Wewe ndio hujaelewa pengine umeangalia juu juu. Kabla ya mkeka kuwini kunanaesha screenshot na kiwango atakachoshinda. 2. Kuna screenshot imepigwa baada ya mkeka kukamlika na kuwa haujashinda na dau limerejeshwa sasa hapo mkeka umefutwa katika hatua gani katika hizo mbili ikiwa mkeka kabla ya kushinda anazo taarifa. Na mkeka baada ya kikamlika anazo taarifa? Fungua ubongo kijana ,, mkeka kufutwa nilabda baada ya matokeo asingeuona mkeka huo kwamba umefutwa ilihali umeshinda
 
Sio sahihi kivipi? ,, mtoto mada kasema wameshindwa kumlipa. Mimi nikasema huo sio utetezi huwezi toa hoja kuwa kampuni imeshindwa kukulipa ukaeleweka. Mikeka yote wanayoruhusu maana yake wanaweza kukulipa , Hata ikitokea maximum win umeshinda bilion nilazima ulipwe. Kwahiyo hiyo sio sababu ya msingi. Nikasema kuna sababu zinazoweza kuzuia usilipwe. 1. Fixmatches, error kwenye mfumo au ikatokea wamehitaji kyc ukashindwa kutuma ,, sasa kama sababu ni hizi huwezi kulipwa. Lakini kama sababu nikuwa wameshindwa kukulipa hiyo sio sababu ya msingi wanatakiwa wakulipw hata kwa kushurutishwa. Sasa wewe hujaona msingi wa hoja yangu vipi
Kampuni za michezo ya kubahatisha hua zina maximum amount watakayokulipa hua wanaiweka kwenye terms and conditions. Mfano maximum amount ni 15M ukishinda 16M wanarudi kwenye terms and conditions na kukulipa waliyoisema.

Ubaya ni kwamba, hawatokataa betslip uliyoweka ambayo inavuka maximum amount ila ukishashinda ndiyo unapitishwa kwenye terms and conditions.
 
Msingi wa hoja yako sio sahihi kwa mtoa mada kwa sababu wewe ulikimbilia kumuattack badala ya kuangalia muktadha upande wake upoje

Muktadha kwake ashasema walikubali kumlipa lakini kwa kiwango pungufu bila sababu za msingi ambacho kwake bado anaona sio sahihi, huoni kama mpaka tayari hoja zako zinakosa nguvu?

Akasema " Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo,"
Kanuni gani ,imetumika hapo?
Huoni kuna viashiria vya wizi?
Point ya pili hoja yako kukosa mashiko

Tunakuja tena akasema
"Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi "
Kwa nini walikubali kumlipa means hoja zake zilionekana ziko sahihi mbele ya board ,lakini je kwa nini haikuandikwa kwenye maandishi? Unapata viashiria kuwa bado na kampuni shtakiwa kuna kitu walikubaliana behind the door.
Na kwa nini wakubali kumlipa miliion 3?

Kwa nini point yako dhaifu ,point ya 4
Akasema
" kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, "
Kwa nini wambembeleza kushusha kiwango cha ushindi kwenye ushindi unaoutilia mashaka?

Point ya 5
Akasema
"Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano."
Mpaka bodi (TGB) wanafikia stage hii wao kwamba muda wote huo hawakuona viashiria unavyodai wewe vya upangaji wa matokeo na kufuta shauri?

Inshort HOJA ZAKO ZINA MADHAIFU MENGI SANA em tubishane kwa hoja
Huyo member anaongea logic na taratibu zilivyo lakini kwenye hii ishu hakuna logic wala taratibu.

Kama ushindi ungekua una shida ilibidi watoe ushahidi na kugomea kumlipa.

Kama terms and conditions zinasema maximum amount ni 3M ilibidi watoe hiyo hoja kwa gaming board.

Kisha gaming board ingetoa maamuzi ya kwamba mleta uzi alipwe 3M kwakua ndiyo maximum amount.

Mleta uzi angefika mahakamani na kumbukumbu zingeonyesha kwamba gaming board ilifanya maamuzi.

Mahakama ingejaribu kuona kama maamuzi yalikua sahihi ama la.

Lakini kwa scenario aliyoeleza jamaa hapa kuna upuuzi upande wa gaming board na upande wa kampuni.
 
Kampuni za michezo ya kubahatisha hua zina maximum amount watakayokulipa hua wanaiweka kwenye terms and conditions. Mfano maximum amount ni 15M ukishinda 16M wanarudi kwenye terms and conditions na kukulipa waliyoisema.

Ubaya ni kwamba, hawatokataa betslip uliyoweka ambayo inavuka maximum amount ila ukishashinda ndiyo unapitishwa kwenye terms and conditions.
Kwa kampuni ninazo zijua zenye maximum payment kiwango kitakachoonekana kwenye mkeka ndicho utakachoshinda na kulipwa,, ukizidisha timu utalipwa kiwango hicho hicho kama utashinda na kuongeza timu hakutapandisha maximum payment. Kampuni nyingine hawakuruhusu kuzidi hicho kiwango walichoweka kama umeweka odds nyingi watakulimit kwenye stake unaweka. Kampuni nyingine wana limit kwenye Stake pesa unayoweka kwa mkeka husika au timu zisizidi 50 ,, kampuni nyingine unaweza kuweka kiwango chochote mradi huvuki timu hamsini na hawakulimit kwenye kiwango utakachoshinda isipokuwa wanakulimiti kwenye option utakazo chagua . Lakini kwenye mada mkeka wake haujapewa hata huko kushinda kwenyewe na bado 27 M haiwezi kuwa limit hata kama kampuni ni ndogo kiasi gani ( Japo miaka ya nyuma mbet waliwahi kuwa na kiwango cha chini)

kwasababu kwenye betting huwa kuna mtaji unatakiwa uufikie ndipo upewe leseni ndio maana unaona sio rahisi kukuta watanzania wanamiliki kampuni za betting kwasababu inahitaji mtaji mkubwa na operation zinazohitaji fedha nyingi tena At risk
 
Huyo member anaongea logic na taratibu zilivyo lakini kwenye hii ishu hakuna logic wala taratibu.

Kama ushindi ungekua una shida ilibidi watoe ushahidi na kugomea kumlipa.

Kama terms and conditions zinasema maximum amount ni 3M ilibidi watoe hiyo hoja kwa gaming board.

Kisha gaming board ingetoa maamuzi ya kwamba mleta uzi alipwe 3M kwakua ndiyo maximum amount.

Mleta uzi angefika mahakamani na kumbukumbu zingeonyesha kwamba gaming board ilifanya maamuzi.

Mahakama ingejaribu kuona kama maamuzi yalikua sahihi ama la.

Lakini kwa scenario aliyoeleza jamaa hapa kuna upuuzi upande wa gaming board na upande wa kampuni.
Kama ni mambo ya maximum payment kwanza hapo walitakiwa wampe win kwenye mkeka na wachukue dau lao na alipwe na malalamko yangekuwa kwanini amelipwa kiwango kidogo na jibu liwe alivuka maximum payment.

Tatizo hapo mkeka timu zimeshinda lakini hajapewa ushindi kwenye mkeka na hapa lazima wampe majibu yanayoeleweka
 
Kampuni ina omba mungu 😄
Ila kamari mambo yake yana endeshwa kikamari kamari
Kwenye T&C zao unakuta wanasema wana uwezo wa kufunga AC wanapo ona inafaa au kukulipa kile wanacho ona kinawafaa wao sasa si balaa hilo
Hizo T&C ndo wanaztumia kampuni uchwara uchwara kama hao piga Nini sjui kupiga watu ..
Kampuni inakuibia mpaka stake ya buku3 unategemea wakulipe millions ..
 
Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo,"

Kampuni ikisimamisha mkeka huwa haitoi taarifa na hilo limeelezwa kwenye vigezo,na masharti
Kwahiyo mpaka hapo umeandika nonsense!
Pili kuhusu mkeka kufutwa hiyo sio kweli kwasababu aliweza kupiga hadi screenshot mkeka.

Kama kampuni imeshindwa kumlipa isingerudisha dau lake la 900 badala yake ingeonesha ameshinda kiwango husika lakini hajalipwa , Kwahiyo hiyo ni nonsense nyingine uliyoandika ,, kinachofanya urudishiwe dau lako ni mambo matatu 1. Ume cashout mwenyewe. 2. Fixed game, 3. System error hapa unarejeshewa kiasi ulichoweka ( na ndipo msingi wa hoja yangu unapoanzia) kwahiyo hata akienda mahakamani hawezi kusema nilishinda kiasi fulani halafu sikulipwa mana hakuna ushahidi wa ushindi na akilipwa haya serikali itapata kodi yake. Hoja yake ni mkeka sahihi kutopewa ushindi nasio kushinda kiasi fulani na kutolipwa ,, jambo jingine nivigumu kuwa na makubaliano kati ya wewe na kampuni bila maandishi labda iwe hayo makubaliano huyo mwakilishi wa kampuni aliyafanya kibinafsi na sio kwa niaba ya kampuni. Kwa bahati mbaya mleta mada hajaweka kiambatanisho hata kimpja kutoka Gaminh board hata email hajaweka kwahiyo siwezi kulisemea sana kuwa ni kweli ama la
Unazurula zurula tu kifupi kampuni lenu ni la kitapeli na haliaminiki
 
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Oya mzee Kaza wakupe pesa zote, hao gaming boards n kama vile wamepewa pesa wakukatae, ukishindwa kabisa fanya namna utegeshe bomu kwenye ofisi zao ili wote mle hasara kmmk
 
Back
Top Bottom