DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
acha uhuni hizo sababu dhaigu wampe haki yake ningekuwa mimi isingepita hata wiki
 
wewe ndo ulikosea katika mashariti ya usajiri, tatizo la kufanya mambo kwa mazoea
naelewa sana tatizo nchi nilipo kamari sites wanaziblock imebaki parimatch na 1xbet nako siku nyingine unaamka hazifanyi kazi hata kwa vpn so usajili wake ulihitaji email na line ya simu na OTP Nikatumiwa ila sasa kumbuka hii line nilipewa tu na agent sasa hata sijajua ilisajiliwa vp lakini hatukufanya registration yoyote kwa details zangu
 
Hapana akiwapost mitandaoni kesi itamgeukia yeye kwa kusema amewachafua hapa njia sahihi anatakiwa awapeleke mahakamani tena atafute na msaada wa mawakili inaonekana wamemuona jamaa anaenda kinyonge ndio maana wanapata tamaa ya kumrubuni jamaa ili wampige pesa zake
 
Asipolipwa lazima dish liyumbe
 
Mi ndo sitaki kabisa kusikia mambo ya jackpot, maana hiyo pesa wanayotangazwa nayo washindi hupati yote.

Kuna jamaa naemjua alishinda jackpot ya sportpesa million 200+ walienda kumuweka hotel serena for 5 days wana bargain nae tu, mwisho wakafikia compromise jamaa hakusema exactly walimpa kiasi gani ila alikubali kufanya tangazo la hundi ya milion 200+, in return wakampa gari yenye thamani ya milion 30 na undisclosed amount of money..

Kiufupi hajafanya lolote la maana mpka sasa mana maisha yake ni yale yale tunayoyajua ila still gari anayo.
 
1x sio ya kijinga, hapa ni wewe tu ukosea utaanzaje kubeti kabla ya kuverify account, sasa ukila utatoahe hela

ila 1x ndo mimi naikubali haina mbambamba ukifuata utaratibu
 
Hahaha unatumika kusaidia wanaokufahamu waendelee kubeti wakiamini kuna ushindi kweli. Inshort unakuwa tapeli na wewe kwa malipo kidogo.
 
Hahaha, hizi Janja janja hizi.
 
Kuna jamaa ana lalamika kadhulumiwa betting Fanya hivi.

NENDA KWENYE GAZETI KIBWA INAWEZA KUWA MWANANCHI, AU MWANASPOTI, WAMBIE KUA NILI SHINDA KITITA CHA PESA PIGA BET LAKINI SIJALIPWA PESA ZANGU SASA BASI NATAKA HII HABARI ITOKE KWA UKUBWA MBELE YA GAZETI LA JUMA TATU.

PIGA BET, WALIWA WATAPELI WAINGIA MITINI BILA KUMLIPA MDAU HAKI YAKE, 27M.

mkuu alafu sikilizia
 
Uthibitisho huwa ni nini kuwa hii imekuwa fixed? Michezo husika ilifutwa matokeo? Acha kutetea utapeli. Janja janja hahaha
Mwenzako anajadili kwa mantiki wewe unajadili kihisia. Ungekuwa unasoma terms and conditions za hayo makampuni ya kubeti usingeuliza haya maswali.

Siku nyingine bashiri fixed match, shinda alafu kosa hela uende mahakamani uone kama utapewa.
Huwezi tumia mihemko kisha umzidi anayetumia logic, common sense na maarifa.
 
Tafuta mwanasheria sio viwanasheria uchwara washita hiyo betting, gaming board, waziri wa fedha na mwanasheria mkuu.
Kwa mwanasheria mkuu utatoa notisi ya siku 90 nakuhakikishoa watakulipa kabla ya kqenda mahakamani.
 
Mpe KIBATALA hizo 7 umalizane na hao wahuni.
Lkn mkuu,mbona ulichelewa sana kuwaanika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…