DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Haya ni ya kweli Mkuu? Maana zile jackpot za Sportpesa hua zinafika adi 1.2B kwamba mtu ashinde 1B afu wamnyime tena kwanini sasa walianzisha hiyo michezo kama kweli picha liko ivyo?🤔
 
Waburuzee mahakamani tu wakulipe fidia million 270 kabisa..
 
Nimekuelewa, lakini fixed match si mpaka idhibitishwe na mamlaka inayosimamia soka ya nchi husika, mfano hapa ligi ya bongo mpaka TFF au caf, wadhibitishe kuwa mechi fulani imepangwa, au hayo makampuni ya kubeti yanadhibitisha yenyewe?
Ndio maana unatakiwa usome terms and conditions za kampuni husika.

Vilevile ndio maana kwenye solutions za fixed matches mojawapo nimeandika kampuni mojawapo inawazunguka walioweka fixed. Watu kama 25 wa timu X wanakubaliana wafungwe over 2 kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili wafungwe over 3.

Hao hao 25 wana ndugu, marafiki, classmates, wadau mtaani. Wanatoa siri. Baada ya masaa kama manne placements zote ni over 1.5 first half, au over 4.5 full time, au matokeo yanayoashiria yamepangwa.

Betting company ina mengi ya kufanya. Inafungia mechi, inarudisha muamala, inapunguza odds, inazuia options, inafanya mechi iwe "void". Au inanunua mechi.

Inaitafuta ile timu Y ambayo X walitaka waiachie kizembe ifunge, betting company inawaambia kuna shilingi kadhaa hakikisha mnafunga goli 1 first half tu. Second half kama hawarudishi msifunge, wakirudisha funga la pili tu. Kwa sababu wale X wanacheza kufungwa hawawezi kuifunga Y. Mwishowe kila aliyejilipua anachana mkeka.

Haya mambo yapo. Ndio maana nimeandika page za mwisho huku maana wasomaji wanaishia page 1 or 2.
 
Unadhani habari kuandikwa front page kwenye gazeti ni rahisi kihivyo Ndugu?
Gharama ya kukaa front page je? Lazima iwe habari ya kuwaingizia fedha..
 
Betway hawana longo longo.
Unamaliza kila kitu online.
Una deposite, withdraw pesa yako kwa njia ya simu bila verification Kibao au mauzauza ya pigabet na 1xbet au galsports au betpawa.
Siku utakapo shinda pesa mingi ndio utajua kwanini hizi kampuni hua zina hitaji ufanye Full Registration kwa ku verify acc kama hukuweka/attach necessary document wakat una fungua akaunt yako
 
huwa naogopa sana hizi kamuni ndogo
Udogo wa kampuni unapima na nini kwamba kuna kampuni inaanza biashara bila kuwa na mtaji hitajika ? Kuna vigezo kwanz nilazima uwe na mtaji kiasi kadhaa ndio usajiliwe pili . Kila kampuni ina kiwango maximum chakulipa na hawataruhusu ushinde zaidi ya hicho kiwango ,, hivyo kama wamwkubali wewe kustake maana yake wana uwezo wa kukulipa kama utashinda
 
Kuna kitu mtoa mada haja kiweka wazi ila kwa mtazamo wangu nime jaribu kufikiria hizo Odds na aina ya option yawezekana ndipo shida ilipo

Aina ya mchezo ni basketball option ni kua kipindi cha kwanza team zote zifunge point kuanzia 25 ndio ushinde (kampuni imeweka odds 8 mpaka 9) kwa option hiyo ambapo kiuhalisia hizo odds ni nyingi na huu ndio mushkeli kampuni ilifanya makosa yenyewe yawezekana ndio sababu ya kugoma kulipa hiyo amount.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…