DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Lakini nimuhimu kusoma vigezo na masharti
Ukiangalia mkeka wa jamaa ni basketball na option ni both teams to score 25 points first half
Hili si suala la match fixing kabisa hio labda walikosea odds wenyewe kwa kuweka odds kubwa.
Vipi na waliobet under 25 first half kwao result zilisomeka vipi? Si walipoteza hela.
Hela bet, Piga bet haya yote ni makampuni ya wezi
 
Tukiacha hii issue ya jamaa , haijalishi unajua au haujui ukiangukia kwenye mchezo uliokuwa fixed kwenye option hiyo hiyo hauwezi kulipwa,, mara nyingi hii michezo inafungwa odds, au kufutwa kabisa kama ulikuwa ushabeti ina<
 

Kama wamekosa odds, au ni match fixing haya mawili wana haki ya kubatilisha ushindi hata mahakama inalijua hilo na hata kwenye terms and condition wanaweka. Sehemu atakaposhinda ni endapo jamaa mkeka uliwin kihalali halafu wao hawataki kumlipa bila hizo sababu mbili.
 
Hao matapeli waliosajiriwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha hukuwajua mapema? Kampuni ambazo hazina longolongo ni mbili tu BETPAWA na SPORTPESA ongezea SPORTYBET wengine kuanzia 1Xbet na kuendelea utasimulia magoli
Sema nikampuni zako unazozbetia lakini kuna watu hata hawazijui na hawajawahi kushinda na kutolipwa
 
Kwenye kamari na muziki kuna ushenzi wa kutisha. Dhuluma ndo nyumbani kwake. Kwa sababu uliamua kushiriki jambo haramu mimi naona bora udhulumiwe ili uwe uchukie betting maisha yako yote.
Umeongea sahihi sana kwenye betting kuna utapeli mkubwa sana, ni vile watu wengi hawashindi wanaona kawaida tu.

Mimi nilishawahi kushinda 17m wakafungia Account yangu, hao Gaming board ni takataka tu hawana msaada wowote
 
Inaonekana mambo sio straight.
 
Kila mtu anamuona aliyeshinda hana akili, hajafanya jitihada za kutosha kufuatilia 27m yake

Nasema sawa, subiría ushinde wewe utamuelewa...Kampuni zote zinakula na Game Boarding kukuzulumu wewe unayebet. Utazungushwa hutoamini.

Subiría ushinde utaona.
 
Hahaha.
 
Wao wanataka wakupune tu ukiwapuna wao ugomvi
 
Hakika Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…