DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ndio maana nikasema suluhisho ni mahakamani. Mimi mwenyewe fixed games nimebashiri sometimes hela inarudishwa, sometimes nashinda, sometimes mimi nashinda mwenzangu aliyeweka vilevile anakataliwa anarudishiwa hela yake, sometimes stake kwangu inakataa juu ya 300,000 kwa mwingine inakataa juu ya 120,000. Ila ukibeti ambazo sio fixed unakuta stake ya 2,000,000 inakubali.

Kwahiyo criterias za fixed inajulikana vipi sijui zaidi ya maelezo niliyotoa.

Ila utakuwa unajiumiza kichwa kama unaamini mtu anajua ana haki since 2024 analalamika tu haijafika mahakamani. I can bet 95% hiyo kesi anashindwa na sio kwa kuonewa. Angekuwa wa kushinda angefika mahakamani hiyo 2024 na sio kutafuta sympathy. Suala la gharama na muda si kampuni ileile ingelipa na fidia yake.
Okey mkuu
 
Kila slip yako ikiangaliwa inaonyesha ulimuamini maniuuuu na liverkukuu
 

Attachments

  • downloadfile-27.jpg
    downloadfile-27.jpg
    86.9 KB · Views: 6
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
Msaidie
Duh hawa jamaa ni wajanja wamejiwekea kinga kuwashinda mahakamani ni shughuli pevu
Kampuni zote ndio hivyo vigezo na masharti vipo kuwalinda wao
 
Ukijiwekea kinga ama vigezo vinavyokubeba wewe tu bila consideration ya upande mwingine ukienda mahakamani itatengua maana mkataba hauwezi kuegemea upande mmoja tu.

Mikataba ina mwongozo wake hata kama mnaingia mkataba watu binafsi bado kuna terms and conditions huwezi kuzikiuka.
Sio kweli mkuu. Wanakwambia kabisa kwa kujisajili account umekubaliana na vigezo na masharti accept sasa umekubali na tiki umeweka mahakama itatenguaje😁
 
Sio kweli mkuu. Wanakwambia kabisa kwa kujisajili account umekubaliana na vigezo na masharti accept sasa umekubali na tiki umeweka mahakama itatenguaje😁
Mkuu jamaa anachomaanisha ni hivi sawa japo jamaa alitiki na kukubali vigezo na masharti lakini kama hivyo vigezo vimekaa kihuni wanaweza kuvipitia virekebishwe ili kuwe na usawa isiwe vigezo vimeegemea upande mmoja
 
Acha uzembe! Tafuta mwanasheria serious mpige hela ndefu kuliko hiyo. Shtaki wote kampuni na board! Nakuhakikishia watalipa bila kujiuliza! Wamekuona boya ndio maana hawajali
 
Mkuu jamaa anachomaanisha ni hivi sawa japo jamaa alitiki na kukubali vigezo na masharti lakini kama hivyo vigezo vimekaa kihuni wanaweza kuvipitia virekebishwe ili kuwe na usawa isiwe vigezo vimeegemea upande mmoja
Haviwezi kurekebishwa kampuni zote za betting vigezo ni hivyo hivyo. Vigezo vipo upande wao kwasabbau wao ndio wanaweka mtaji mkubwa kuliko wewe. So lazima kuwa na vigezo vya kuwalinda wewe utaweka jero lakini wao unawashinda hadi zaidi ya bilion zo huyo wa bilion nilazima ajilinde dhidi yako kwa mbinu zozote utakazotumia kumshinda
 
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Umejaribu kufuatilia mwenye hiyo kampuni ni nani...?
 
Mkuu unahisi tangu 2024 mpaka leo hajawahi pata hii idea. Kwamba ni ngeni hajawahi ambia mtu yeyote aliyekuwa anayo?

Au unahisi hajawahi sema kwingine ndio kwa mara ya kwanza kaomba ushauri JF?
Amesema alienda mahakaman kufungua kesi akawekewa pingamizi, kaelezea mengi sana ila sijaona aliposema amekaa chini na vibatara,
Unaweza beti fixed odds. Ukafidiwa hela ya take it or leave it pale utakapolalamika kunyima ushindi. Ni hela ambayo unapewa kufungwa mdomo na msizungushane, endapo hutaki nenda mahakamani msomeane vifungu na ushindwe.

Ambacho hujui makampuni hayataki usumbufu. Mfano unaweza kuilalamikia Vodacom kwenye jambo fulani ambalo linaichafua na kwa sababu wabongo wengi ni vilaza hawana logic na wanachukia matajiri wakihisi wao ndio wamewafanya wawe maskini, basi wana-side na mnyonge. Sasa Voda inaweza piga hesabu ya gharama za mwanasheria, usumbufu na bad publicity ikauita ikupe labda 5M muachane. Hiyo haimaanishi ukikataa kupokea hela utawashinda ukienda mahakamani. Wala haimaanishi wamekosea ndio maana wametaka kukulipa.


Ni match za kupanga matokeo mfano Simba inacheza na timu ambayo tiyari imeishashuka daraja hata ingefunga. Na bado Simba inataka pointi 3 ili iikimbize Yanga kileleni, na wakubwa wa timu inayoshuka daraja wanajua hawana future nzuri. Kwahiyo wanapanga na Simba ili wafungwe mfano 4-1. Sasa odds za matokeo exact ya 4-1 unazijua zinakuwa nyingi kuanzia 5 au 6 uko.

Au kwenye kesi hiyo, Yanga wanaitafuta timu inayoshuka daraja wanaiambia kaza muifunge Simba au mpate sare, tutawapa 40M. Wanakaza vibaya mno.

Kwahiyo kampuni za kubeti zinasoma trend zinashangaa mbona kuna watu kama 50 ndani ya lisaa wameweka beti ya Simba 4 - Timu XXX 1 full time. Hapo wanafungia mechi au wanafungia option au wanaweka limit ya stake.

Alternatively, kampuni mojawapo ya kubeti inapiga hesabu total stake ya watu wote waliopata hizo fununu ni ngapi labda total ni zaidi ya 300M kwenye ile fixed, inamtafuta refa na kiongozi wa timu ile dakika za mwisho kabisa kabisa inawapa pesa na kuwapangia matokeo labda Simba wakaze ifunge 3 ile timu nyingine isifunge goli kabisa (sababu haina uwezo wa draw au kuifunga Simba). Striker wa timu XXX akionyesha dalili za kushambulia sana anatolewa anaingia boya boya.

Mara nyingi wanaambiwa kipa, refa, manager wa timu. Wachezaji wengine nao wanaweza kuwa walisanuka wakaweka 4-1 ila dakika za mwisho kabisa deal limesukwa hawajui. Kwa kawaida huwa hawashiki simu dakika kadhaa kabla ya mechi.
Corporate companies zinakulq sana mieleka mahakaman tena sometimes wakiona wanadalili yakutokutoboa hizo kesi huwa wanaomba kumalizana nje ya mahakama maana maana italeta damage kwa brand zao, tatizo letu wabongo ni inferiority complex kuhis hawawez kushindana na makampuni wakat wenzetu hizo legal blunders kwao ni fursa, kama ATCL wanavyofanyaga double boooking na watu wananyamaza tu wakihis hawana chakuwafanya ila akitokea opportunist atalifilisi shirika letu
 
Back
Top Bottom