DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
 
Hizo fixed match unajua vipi? Na kwanini waweke fixed match watu wabeti kama wao wanazijua?
Je kama ni janja yao kwamba Kila tukiliwa hela kubwa tuseme match ilikua fixed. Uthibitisho wa match kuwa fixed ni ngumu na haupo, pili huyu aliyebet hausikii na kufix watch yeye amebashiri matokeo atahusika tu endapo ni mchezaji au ana mahusiano ya karibu na hao waliofix match
Aende mahakamani. Atoe ushahidi. Apate haki yake.

Mimi wala sikuandika kuhusu mleta mada. Wala lingekuwa ni jambo langu nisingekuja JF na nisingedai 27M pekee. Ningedai na fidia ya usumbufu.
 
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
🤣🤣🤣🙌
 
Umeongea sahihi sana kwenye betting kuna utapeli mkubwa sana, ni vile watu wengi hawashindi wanaona kawaida tu.

Mimi nilishawahi kushinda 17m wakafungia Account yangu, hao Gaming board ni takataka tu hawana msaada wowote
Mkuu ilikuwa kampuni gani?
 
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
Mkuu unahisi tangu 2024 mpaka leo hajawahi pata hii idea. Kwamba ni ngeni hajawahi ambia mtu yeyote aliyekuwa anayo?

Au unahisi hajawahi sema kwingine ndio kwa mara ya kwanza kaomba ushauri JF?
 
Kwani mpaka betpawa Kuna verification au mpaka ushinde mabilioni ndiyi verification
Kuna verification ukishinda hela nyingi na mechi zenye ukakasi. Inaweza chukua siku mbili hivi, unapiga picha na vitambulisho.

Ukitazama akaunti ya mtu aliyewahi kula hela nyingi iko verified na kwa muda fulani inaweza kuwa limited kwenye stake.
 
Nimekuuliza ili ujibu nikuelewe. Anyway kama hakuna majibu ni sawa tukimaliza kwa style hii ya kuelekezana kwenda mahakamani.
Ndio maana nikasema suluhisho ni mahakamani. Mimi mwenyewe fixed games nimebashiri sometimes hela inarudishwa, sometimes nashinda, sometimes mimi nashinda mwenzangu aliyeweka vilevile anakataliwa anarudishiwa hela yake, sometimes stake kwangu inakataa juu ya 300,000 kwa mwingine inakataa juu ya 120,000. Ila ukibeti ambazo sio fixed unakuta stake ya 2,000,000 inakubali.

Kwahiyo criterias za fixed inajulikana vipi sijui zaidi ya maelezo niliyotoa.

Ila utakuwa unajiumiza kichwa kama unaamini mtu anajua ana haki since 2024 analalamika tu haijafika mahakamani. I can bet 95% hiyo kesi anashindwa na sio kwa kuonewa. Angekuwa wa kushinda angefika mahakamani hiyo 2024 na sio kutafuta sympathy. Suala la gharama na muda si kampuni ileile ingelipa na fidia yake.
 
Hapa tumeskiliza upande mmoja. Pigabet watu wanapiga hadi milion 600 hapo the grand casino na wanalipwa waje washinde kulipa milion 27? kwanza kwa sheria za kampuni za betting hawawezi kuruhusu wewe kuweka mkeka wa kiwango ambacho hawawezi kukilipa. Trust me ku sehem kuna shida jamaa aweke wazi
Hao walioshinda milioni 600 una uhakika walilipwa zote au wanapewa milioni 10 kisha wanawarekodi na kutuma tangazo kwenye TV kuwalaghai watu kuwa mshindi kapata milioni 600.
Sijawahi kuwaamini watu wa mchezo wowote wa kamari uhuni mwingi
 
Unaweza beti fixed odds. Ukafidiwa hela ya take it or leave it pale utakapolalamika kunyima ushindi. Ni hela ambayo unapewa kufungwa mdomo na msizungushane, endapo hutaki nenda mahakamani msomeane vifungu na ushindwe.

Ambacho hujui makampuni hayataki usumbufu. Mfano unaweza kuilalamikia Vodacom kwenye jambo fulani ambalo linaichafua na kwa sababu wabongo wengi ni vilaza hawana logic na wanachukia matajiri wakihisi wao ndio wamewafanya wawe maskini, basi wana-side na mnyonge. Sasa Voda inaweza piga hesabu ya gharama za mwanasheria, usumbufu na bad publicity ikauita ikupe labda 5M muachane. Hiyo haimaanishi ukikataa kupokea hela utawashinda ukienda mahakamani. Wala haimaanishi wamekosea ndio maana wametaka kukulipa.


Ni match za kupanga matokeo mfano Simba inacheza na timu ambayo tiyari imeishashuka daraja hata ingefunga. Na bado Simba inataka pointi 3 ili iikimbize Yanga kileleni, na wakubwa wa timu inayoshuka daraja wanajua hawana future nzuri. Kwahiyo wanapanga na Simba ili wafungwe mfano 4-1. Sasa odds za matokeo exact ya 4-1 unazijua zinakuwa nyingi kuanzia 5 au 6 uko.

Au kwenye kesi hiyo, Yanga wanaitafuta timu inayoshuka daraja wanaiambia kaza muifunge Simba au mpate sare, tutawapa 40M. Wanakaza vibaya mno.

Kwahiyo kampuni za kubeti zinasoma trend zinashangaa mbona kuna watu kama 50 ndani ya lisaa wameweka beti ya Simba 4 - Timu XXX 1 full time. Hapo wanafungia mechi au wanafungia option au wanaweka limit ya stake.

Alternatively, kampuni mojawapo ya kubeti inapiga hesabu total stake ya watu wote waliopata hizo fununu ni ngapi labda total ni zaidi ya 300M kwenye ile fixed, inamtafuta refa na kiongozi wa timu ile dakika za mwisho kabisa kabisa inawapa pesa na kuwapangia matokeo labda Simba wakaze ifunge 3 ile timu nyingine isifunge goli kabisa (sababu haina uwezo wa draw au kuifunga Simba). Striker wa timu XXX akionyesha dalili za kushambulia sana anatolewa anaingia boya boya.

Mara nyingi wanaambiwa kipa, refa, manager wa timu. Wachezaji wengine nao wanaweza kuwa walisanuka wakaweka 4-1 ila dakika za mwisho kabisa deal limesukwa hawajui. Kwa kawaida huwa hawashiki simu dakika kadhaa kabla ya mechi.
Duh kumbe kazi yao inahusisha hadi kufanya fitina uwanjani?
Na hii inafanyika hadi kwenye timu za ulaya au ni bongo tu?
 
Hao walioshinda milioni 600 una uhakika walilipwa zote au wanapewa milioni 10 kisha wanawarekodi na kutuma tangazo kwenye TV kuwalaghai watu kuwa mshindi kapata milioni 600.
Sijawahi kuwaamini watu wa mchezo wowote wa kamari uhuni mwingi
Mimi nimewahi kumuona mwalimu mmoja alipiga milion 28 na alilipwa yote hao walikuwa ni sportpesa
 
Tafuta mwanasheria akusimamie jambo lako ndani ya muda mfupi tu utaweka kibunda chako kibindoni.

Tena hapo ukiwa na mwanasheria anajua namna ya kudai hadi fidia za namna mbalimbali ili hata zisipotiki zote lakini zipo zitakazotiki baada ya hoja kukubaliwa na mahakama.
 
Duh hawa jamaa ni wajanja wamejiwekea kinga kuwashinda mahakamani ni shughuli pevu
Ukijiwekea kinga ama vigezo vinavyokubeba wewe tu bila consideration ya upande mwingine ukienda mahakamani itatengua maana mkataba hauwezi kuegemea upande mmoja tu.

Mikataba ina mwongozo wake hata kama mnaingia mkataba watu binafsi bado kuna terms and conditions huwezi kuzikiuka.
 
Back
Top Bottom