kidadari
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 8,647
- 9,604
Nimeenda benki fulani kwa uhitaji wa mkopo wa 8.4m wakanimbia riba 18%.
Baada ya kupewa makato yakawa 195,820 kwa mwezi kwa miaka 6. Sasa nawauliza mbona kiuhalisia sio 18% kama wanavyotuambia kwenye matangazo yao? Wanajibu kwa mujibu wa calculator yao ipo sahihi, hapa ina maana mpaka marejesho itakua ni 14,099,040 ndani ya miaka 6.
Hawa jamaa wanatumia formula gani kufanya calculations zao, kuna dalili ya wengi kupigwa maana kuna usiri mwingi sana. Ni vizuri ikawekwa wazi ili kabla hujaenda kuchukua mkopo ujue na marejesho yake yatakuwa vipi.