Nimeshindwa kuelewa formula ya mahesabu ya mikopo ya benki hii

Nimeshindwa kuelewa formula ya mahesabu ya mikopo ya benki hii

Ningetegemea ungemsaidia hata kuweka screen shot ya hiyo Excell calculator but umeishia maneno matupu tuu, kiufupi hatuwezi kukuamini ukisemacho, tena yawezekana wewe ni mmoja wao huko bank.
Screenshot_20201215-152156.png

Nimeweka screen shot , hao kwenye $ sign isomeke Tsh
 
Hiyo siyo formula inayotumika kwenye mikopo , sababu interest sio kila mwezi itapigiwa hesabu kwenye hela iliyochokuliwa mwanzoni mwa mkopo
Em wewe weka formula yako maana mimi hiyo sijaweka kwa mwezi niliweka kwa mwaka ndomana T niliweka 6 nikimaanisha miaka sita sio miezi 72
 
Nimeenda benki fulani kwa uhitaji wa mkopo wa 8.4m wakanimbia riba 18%.

Baada ya kupewa makato yakawa 195,820 kwa mwezi kwa miaka 6. Sasa nawauliza mbona kiuhalisia sio 18% kama wanavyotuambia kwenye matangazo yao? Wanajibu kwa mujibu wa calculator yao ipo sahihi, hapa ina maana mpaka marejesho itakua ni 14,099,040 ndani ya miaka 6.

Hawa jamaa wanatumia formula gani kufanya calculations zao, kuna dalili ya wengi kupigwa maana kuna usiri mwingi sana. Ni vizuri ikawekwa wazi ili kabla hujaenda kuchukua mkopo ujue na marejesho yake yatakuwa vipi.
Huo mchanganuo uko sawa probably hayo makato ya mwezi wame-include na gharama nyingine za mkopo.

Formula waliyotumia ni REDUCING BALANCE METHOD.

Mikopo ya benki ukitaka ikupe tija uwe na uwezo wa kuurejesha kwa kipindi kifupi let's say 6 months to 12 months or 18 months. Kadri unavoongeza muda wa marejesho ndivyo utakavyokamukiwa na kutokupata tija.

Pia uwe mdadasi wa kujua kuhusiana na INCLUSIVE COSTS na taarifa nyinginezo zinazoendana na mkopo iliuweze kufanya uamuzi sahihi. Usipokuwa mdadadisi theye won't give you all details.
 
Nimeenda benki fulani kwa uhitaji wa mkopo wa 8.4m wakanimbia riba 18%....

Hayo marejesho mbona hamna wizi hapo!?

Ujue hiyo million 8 kwenye biashara inaweza ikazalisha faida ya hadi 6M au hata zaidi ndani ya mwaka mmoja!

Tatizo ni kwamba watu wanakopa wanaenda kufanya harusi na kula bata au kutatua matatizo ya kifamiliaa, hapo ni lazima uone bank ni wezi tu!
 
Wana aina flani ya uyapeli ndo maana hawaweki wazi mahesabu yao
Basically waomba mikopo wengi huwa wapo too excited hata hawaombi kuprintiwa ile payment plan ili waidadavue kabla mtu hajaingia king mazima

Bank hawana kosa kimsingi. Wao wapo pale kibiashara zaidi
 
Hayo marejesho mbona hamna wizi hapo!?
Ujue hiyo million 8 kwenye biashara inaweza ikazalisha faida ya hadi 6M au hata zaidi!
Tatizo ni kwamba watu wanakopa wanaenda kufanya harusi na kula bata au kutatua matatizo ya kifamiliaa, hapo ni lazima uone bank ni wezi tu!
Au kununua vitz
 
Tatizo nyie watumwa wa umma mnakuwa kama vipofu pindi mkihitaji mikopo sijui shuleni mlifundishwa nini kima nyie mnaishi maisha ya hovyo kwa sababu mna makato mengi ya mikopo amambayo hatuoni uwekezaji wake
 
Mkopo wa bank ni faida kwa bank siku zote wanakwambia 18% ukija kupiga hesabu inakuwa umelipa 75 -80%, ila ndo hivyo ukiwa na shida utaenda mwenyewe
 
Tatizo nyie watumwa wa umma mnakuwa kama vipofu pindi mkihitaji mikopo sijui shuleni mlifundishwa nini kima nyie mnaishi maisha ya hovyo kwa sababu mna makato mengi ya mikopo amambayo hatuoni uwekezaji wake
Matusi hayo
 
Nimefoward


Kuna mzee mmoja kakopa crdb 30m kwa mshahara wake. Amekatwa kwenye mshahara wake wee mpaka kufika mwisho kajikuta amelipa 68m

[emoji2298] Tulishaambiwa riba ni haraam hatukomi....... Wangapi wamechkua overdraft (mikopo ya biashara) wameishia kuumbuka kwa kuuziwa nyumba zao walizoweka kama security!!!!!! Mungu Hadhihakiwi
 
[emoji2298] Tulishaambiwa riba ni haraam hatukomi....... Wangapi wamechkua overdraft (mikopo ya biashara) wameishia kuumbuka kwa kuuziwa nyumba zao walizoweka kama security!!!!!! Mungu Hadhihakiwi
Wapi wanatoa bila riba au faida tuende fasta
 
18% ni kwa mwaka.

Ukikopa miaka 6 inakuwa 18%x6.

Binafsi sielewi inakuwaje mtu unakopa mkopo kwa muda mrefu hivyo ?

Key Points.

1. Kadri unavyokaa na pesa ya mkopo muda mrefu ndivyo Riba na pesa ya jumla ya marejesho itajavyokuwa kubwa.
( Umirudisha pesa yao mapema maana yake atakopeshwa mtu mwingine ).

2. Watu wengi wanapenda mikopo ya muda mrefu kwa kufurahia tu kiasi cha pesa watakachobaki nacho kwenye mshahara baada ya makato, bila kuangalia Total amount na muda wa malipo ).

Note: Kopa mkopo, lipa kwa maumivu ndani ya muda mfupi kadri uwezavyo, utalipa pesa kidogo.

Sure!!! Mie naona kuna watu wanafanya vizuri kwa kukopa kwa zile taasisi za kukopesha like BRAC kuliko hata wanaokopa bank
 
Ndio maana pia nliamua kutochukua loan Baada y miaka kadhaa y mahangaiko n bayport
 
Back
Top Bottom