Nimeshindwa kuelewa formula ya mahesabu ya mikopo ya benki hii

Nimeenda benki fulani kwa uhitaji wa mkopo wa 8.4m wakanimbia riba 18%....
Mkuu, kwenye calculation za mkopo kuna formula kuu mbili:

1. Straight method
2. Reducing method

Watu wa bank kuna mambo huwa hawayaweki wazi. Ili la mikopo likiwa ni moja wapo.

Lingine ni suala la fixed deposit. Always maelezo wanayotoa kwa wateja ni tofauti ni kile ambacho utapata siku ya mwisho. Mfano:

1. Suala la kodi-hili huwa hawalisemi kabisaa yaani.

Yapo mengi sana!
 
Kudadadeki
 
Mkuu kuna watu hawajui.

Bank zina Riba nafuu ukiliinganisha na taasisi nyingine za kifedha.

Ukiijulia mikopo, utaifaidi mnoo
 
Shida ndo zinafanya watu wakope...Ila hizi taasisi za kifedha dah...wengine Wana hadi 35% marejesho ya kiasi unachokopa.....!
 
itoshe tu kusema tayari umeshaingia mkenge utakatwa kwanzia mtt anaingia darasa la kwanza Hadi anamaliza darasa la 7. Umechukua 8 alaf unarudisha 14 nikama unarudisha mara mbili ya mkopo
 
Waislam haturuhusiwi kula riba wala kuliwa riba ...ndio maana dini imekataza kutona na unyonyaji uliopo
 
Waislam haturuhusiwi kula riba wala kuliwa riba ...ndio maana dini imekataza kutona na unyonyaji uliopo
Lakini unyonyaji unaofanywa na benki za kiislam ni mkubwa zaidi ya huu
 
Yaani hawa no NMB kabisa, wameninyang'anya duka kibaya Wanechukua na Fridge ya mjomba ang nililokuw nimemhifadhia, saivi mi nadaiwa fridge la watu,

mikopo mibaya wazee[emoji848][emoji848]
 
Kama humwambii mteja ukweli juu ya biaashara yako ni sawa na wizi tuu
 
Mkuu, ninaamini kuwa ingesaidia sana kwa kuliweka jina LA Benki hiyo hadharani ili kusaidia Wananchi wengine kuikwepa hiyo Dhahama.
Unawalaumu kwa kwa ribs za kisiri siri...halafu wewe unafanya siri siri kuwafichia jina lao??
Ninaamini kwamba hata ukiweka wazi jina lao hawawezi wakakujua kutokana na jina unalotumia humu JF.
Na hata wakijua, kwani ulichowaandika ni Uongo??
Funguka, Usaidie Wengine....
 
Hiyo riba ni kwa kila mwaka.Mikopo ya muda mrefu iko hivyo ni karibia unalipa mara mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…