Nimeshindwa kwenda kumzika Mama haya maisha hayako fair naombeni msaada😭

Well Said Tonny Kapola Gas Station

Pole Kwa Msiba ... Mboju


Mungu Akutangulie Kwa Kila Jambo 🙏
 
Pia bado hajazikwa

Mkuu bado hajazikwa mazishi ni kesho kama unavyojua vijijini wanathamini sana ndugu na watoto wakubwa kuwepo
Kama ni kesho sidhani kama utawahi mazishi labda utoke muda huu kwa magari ya kuunga ambayo nayo ni ngumu.

Najua unavyojihisi kukutwa na msiba na hauna pesa, Ilinitokea pia lakini marafiki walinisave chap (faida ya kusaidia watu). Ni hali ngumu sana

Kwa hiyo nakuelewa ila nachokushauri ujitahidi kutulia wakati ukitafuta alternatives. Akitokea wa kukupa ticket chap alhamdulillah ila ukikosa, subiri ya kufunga mwezi au kumaliza msiba maana mtoto mkubwa kufika msibani na hauna kitu. Dharau utakayoipata Itakuumiza mara mbili zaidi mkuu
 
Ushauri mzuri,
Kutoka dar mpka kyerwa ni mbali mnoo mbali sana, hata kama wanazika jioni hawezi kuwahi akiondoka sasa hivi. Asome mara mbili mbili huu Ushauri wako. Kama lengo ni kuwahi mazishi
 
Nitakutumia 50,000 nimategemeo yangu wengine pia watakusaidia,miaka mitatu iliopita nilifiwa na babayangu mkumbuke kwenye duwa brother.

Nitakutumia 50,000 nimategemeo yangu wengine pia watakusaidia,miaka mitatu iliopita nilifiwa na babayangu mkumbuke kwenye duwa brother.
Shukrani kaka Na Allah atie baraka pale utakapo toa pia baba Allah ampe pumziko la Amani🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
JAmani tumsaidie mwenzetu kwa chochote kitu, hata ukiwa na buku Mungu atakubariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…