kissa anyigulile
JF-Expert Member
- Apr 21, 2017
- 1,550
- 1,742
Baada ya kuona mwaka 2021 umemalizika, na muda mrefu sana sijajihusisha na mambo ya dini, nikatahayari sana.
Asubuhi mapema nikatafuta boksi langu ninalotunzia vitabu vyangu vya dini.
Nikapekuapekua, paap!, nikakutana na Biblia kubwa kabisa nyeusi nilipewaga na mama yangu.
Nikafumba macho. Nikafunua paap! katikati. Macho yangu yakaangukia maneno yafuatayo:
"Siku za miaka yetu ni miaka sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Na kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana chapita upesi tukatokomea Mara."
Daa! Nika- Google, nikatambua kitabu hicho kiliandikwa 460 B. C. E (miaka 2,480 hivi iliyopita)
Sasa nimebaki najiuliza, kama mambo yako wazi hivi kwa muda mrefu hivyo, kwa nini binadamu tunahangaikia sana maisha kiasi cha kutoana uhai? (kitabu ni Zaburi ya 90, 10 Union version)