Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Herini ya sikukuu ya Noeli, kwangu naona ilishakuwa mbaya kwa mfululizo wa yanayoendelea na hili lililonifanya niandike hapa muda huu.

Kwanza nianze kwa kusema sina utulivu kabisa usingizi umekata na hauwezi kuja kwahiyo kama ntakosea kwenye kuandika mnivumilie.

Ipo hivi nilikuwa ndotoni ghafla nikashtuka muda ilikuwa saa 04:24 , nilivyoshtuka naona reflections za mwanga wa moto, nikajua labda n mwanga wa taa za gari lakini moyo ukasita kuliamini hilo kwa kuwa mwanga wa gari huwa ni mkali zaidi, nikiwa bado kitandani nashangaa zile reflections ghafla zikaanza kumove na kupotea, nikasogeza kapazia kidogo nione nje kinachoendelea. Nimeona moshi unafoka na nikapigia mstari majibu yangu kuwa ule ni moto.

Moyo ukapiga paa!! Nikazungusha macho upande wa pili wa dirisha nikaangalia kwa kunata bila kupepesa macho kama sekunde 40 na kushuhudia mtu kwa mbali kama kapigwa na butwaa akitazama uelekeo wangu kama vile ameniona (ni kama mita 10-15 kutoka nyumba ilipo) ila sikumtambua ni nani kutokana na giza. Baada ya kuona vile nikarudishia pazia nimefanya maombi na ninaamini nipo salama ila hili limenishtua kwa kiasi fulani.
Wakuu nifanye nini zaidi?
Kuna madhara yeyote kushuhudia hilo?
Mshana Jr muongozo wako ni muhimu mkuu nna taharuki kwa lililotokea.

Upuuzi, Nenda kalale
 
Sawa mkuu kila lakheli...nakuombea ili siku moja uje hapa utoe shuhuda na ujithibitishie kwa macho na u regret hizi kauli zako na sio mbali toka Sasa.....
Tokea 2008 huko natoa ofa kwa wachawi wote popote pale walipo, waniroge hata kidogo tu ili wanishikishe adabu na kunifunga mdomo, lakini wapi. Hakuna lolote. Bado nadunda na ngebe zangu.

Uchawi haupo.
 
Kufunga pazia na kuanza kusali ni ishara ya kuwa umejawa na hofu kubwa.

Pale pale mkiwa mnakodoleana, ungemkemea kwa imani. Unammaliza nguvu na mngemaliza biashara.

Sasa zidisha maombi. Maana atakurejea.

Achukue hii,

Witches never leave their projects.

Huyo lazima amrudie tu kuhakiki amejua au hajajua yanayoendelea.
Hapo kwa kila mtu atakae mjia kwa story tata ni kujitoa ufahamu tu kama mwehu hajui chochote huku nafsini akinuia na kufanya dua mabaya yasimpate.

Hapo afanye ujasusi wa kiroho.
 
Achukue hii,

Witches never leave their projects.

Huyo lazima amrudie tu kuhakiki amejua au hajajua yanayoendelea.
Hapo kwa kila mtu atakae mjia kwa story tata ni kujitoa ufahamu tu kama mwehu hajui chochote huku nafsini akinuia na kufanya dua mabaya yasimpate.

Hapo afanye ujasusi wa kiroho.
Nizidishe tu maombi sina namna
 
Back
Top Bottom