Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Hakuna kitu kama hicho na siku ukijua hizo trick utacheka sana
 
Pole sana,

Yes,
ukibainika kupiga chabo mambo ya watu wengine, kwanza ni kosa, lakini pia inaumiza sana.

Na kwahivyo,
Jambo hilo linagharama yake.
Na linahitaji kuchukua tahadhari kubwa na zaidi sana linahitaji ulinzi mkali sana wa kimwili na kiroho.

Omba sana kujawa na roho Mtakatifu wakati wote, vinginevyo pepo wabaya wanaweza kutumwa dhidi yako as a long missile of revenge.

Kawannini unipige chapo inaweza kuambatana na kushikishana adabu kimwili kishirikiana.

Na siku zote mchawi na mshirikina anapendelea akuone ukitaabika tu, hapo anaenjoy vizur sana.Hahitaji kingine kutoka kwako.

Mary Christmas πŸŽ„
 
Bora nisingechungulia
 
Nitafanya hivyo mkuu
Nikupe siri ya hayo madubwasha.
  1. Unapokutana na jini au pepo au kiumbe cha ajabu, usiogope kwa sababu mpaka kinajionesha kwako ni alama kubwa kuwa umeshinda. Shetani ama nguvu za giza zipo kila mahala duniani na zinafanyakazi. Wanaposhindwa kutimiza lengo baya kwako maana yake una ulinzi wa Mungu na hawawezi kukudhuru. Silaha yao ya mwisho ni HOFU YAKO. Wataitafuta hofu ama.uoga wako kwa kujionesha kwako dhahiri. Ukiingia uoga ama hofu unakuwa umefungua mlango waingie kwako. Kumbuka Petro alipoanza kutembea juu ya maji alifanikiwa lakini alipoona upepo (mawimbi) akaona hofu ndipo akaanza kuzama. Usiogope bali pambana kwa maombi ya ushindi
  2. Wachawi wapo, nao hawana tofauti na celestial beings. Kikubwa hilo tukio uliloliona usiku ni Mungu amekuonesha. Kabla ya kulala hakikisha unasali kuombea familia, ulizi wa mali zako, ulinzi wa miradi yako na kunyunyiza damu ya Yesu kwa maombi. Utaona mengi kama utasisitiza Mungu akupe Hekima ya Roho Mtakatifu wake
  3. Chonde chonde, achana na maji ya baraka, mafuta ya upako, chumvi na chochote kutoka kwa watumishi maana agizo la YESU ni kutumia neno la kinywa chako. Mungu hana masharti kama wafanyavyo waaguzi wa shetani. Kutumia hizo zana ni kufungua milango ili shetani aingie

Pole mkuu, wewe ni mshindi
 
Ikitokea kaonekana inakuwaje?
Ninavojua Mimi Hawa watu wakiingia eneo lolote chakwanza kbla ya kufanya chchte watafanya mambo Yao wanayoyajua kuhakikisha wanafanya shughuli zao na kuondoka eneo latukio bila kuonekana..
Mwiko mkubwa sana kwenye shughuli za uchawi ni kuonekana mkuu.
Sijui ilikuwaje uyo jamaa akaonekana.
Hapo lazma wmfanyie gwaride la utambuzi huyo jamaa kuona kama kweli jamaa alivomchungulia alimtambua kama hakumtambua hakuna shida.
Huyo mchawi atarudi rudi t kwenye mazingira ya kawaida kukusoma kama ulimtambua kwenye tukio.
 
Nimekuelewa vyema kabisa mkuu vita niliyonayo kwa sasa ni HOFU ila nitaishinda na naamini sitodhurika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…