Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 38,283
- 97,793
- Thread starter
-
- #101
asante sana mkuu uwe na sikukuu njema.Inaonekana mkuu hujapitia misukosuko ya hii dunia, sasa katukio kadogo tu hako, kanakutia hofu, ungemuona hapo chumbani si ungeamkia hospital jamani, kuwa na AMANI hilo tukio halikua linakuhusu wewe, ila wakuu wako waliokabidhiwa usalama wako ndio walikuamsha kukuonyesha hali ya mazingira yanayokuzunguka, ili ikiwezekana uchukue tahadhari, na yeye aligundua kama kuna mtu kamuona, but kajithibitishia kwamba hujamtambua, so hawezi kuja kukusumbua kwa sababu hujaharibu mission yake, Kula pilau lako kwa furaha mkuu. Nawatikia SIKU KUU NJEMA.
Dah hatari sana kaka inaogopesha ila sitaogopa nashukuru mmenipa ujasiri.Hakika. Wala usiogope na kuwakimbilia waaguzi wa giza.
Nilianza kuona majini na cellestial beings tangu nikiwa darasa la nne. Niliambiwa NISIOGOPE, nami niliishi na neno hilo hadi leo. Hapa ninapoishi mauzauza kinoma. Kuna wakati unakuta bomba la maji limefunguliwa bafuni huku home nikiwa peke yangu. Unasikia watu wapo nje ukichungulia hakuna kitu.....
Yote yameisha maana nilisali na kukemea. Ninayaona mengi lakini Mungu ananishindia
Sina uo ugonjwa mkuuHii ni dalili ya ugonjwq wa akili inaanza, wahi kutibu, usije chelewa, pia umaskini unazidi pia anza kujikita kufuta umaskini wako kwa haraka, kwani umaskini ni mojawapo ya chanzo cha ugonjwa wa akili
Hili nimejifunza mkuu sirudii tena.Usipende kuchungulia dirishani kila usikiapo mambo ya nje nyakati za usiku unaweza pigwa upofu.
π kumbe ni wewe basi nisharudi kwenye default modeKumbe muoga hivyo ni mimi nilijua kukusabahiπ
Nimeshaomba na nitaendelea kuomba mkuuHuyo aliyekujia huu muda naye anawaza yeye ndo amekosea masharti hadi ukamuona au wewe ndo unashida ...... Omba mungu amefanya makusud umuone lakin usimtambue
Niamini mimi sijalewa mkuuUna uhakika haujaachwa kijana? Hujatumia kilevi?
π€£
Sijafanikiwa kumuonaIlitakiwa uhakikishe unamfahamu huyo kenge ili udeal nae man to man
Kazi ipo ila simuogopiHuyo mchawi zoezi hapo ni kujua kua ulipochungulia ulimuona vizuri ja kumtambua..
Kwaio huyo mchawi atakutembea sana mazingira Yako ya kawaida..
Vitu vya kawaida sana wala hakuna haja ya kuogopa maana havina madharaHerini ya sikukuu ya Noeli, kwangu naona ilishakuwa mbaya kwa mfululizo wa yanayoendelea na hili lililonifanya niandike hapa muda huu.
Kwanza nianze kwa kusema sina utulivu kabisa usingizi umekata na hauwezi kuja kwahiyo kama ntakosea kwenye kuandika mnivumilie.
Ipo hivi nilikuwa ndotoni ghafla nikashtuka muda ilikuwa saa 04:24 , nilivyoshtuka naona reflections za mwanga wa moto, nikajua labda ni mwanga wa taa za gari lakini moyo ukasita kuliamini hilo kwa kuwa mwanga wa gari huwa ni mkali zaidi,
Nikiwa bado kitandani nashangaa zile reflections ghafla zikaanza kumove na kupotea, nikasogeza kapazia kidogo nione nje kinachoendelea. Nimeona moshi unafoka na nikapigia mstari majibu yangu kuwa ule ni moto.
Moyo ukapiga paa!! Nikazungusha macho upande wa pili wa dirisha nikaangalia kwa kunata bila kupepesa macho kama sekunde 40 na kushuhudia mtu kwa mbali kama kapigwa na butwaa akitazama uelekeo wangu kama vile ameniona (ni kama mita 10-15 kutoka nyumba ilipo) ila sikumtambua ni nani kutokana na giza.
Baada ya kuona vile nikarudishia pazia nimefanya maombi na ninaamini nipo salama ila hili limenishtua kwa kiasi fulani.
Wakuu nifanye nini zaidi?
Kuna madhara yeyote kushuhudia hilo?
Mshana Jr muongozo wako ni muhimu mkuu nna taharuki kwa lililotokea.
Kwamba nna malaria?Hivi sasa maeneo mengi mvua zinanyesha mbu wamezaliana Sana malaria π¦ yameongezeka
UsinitisheWatakula nyama yako soon
Acha zako wewewenzako hatuvutii bangi kule kunakowaka moto, tunavuta bangi kule ambako hapawaki moto!
Naamini pia havinidhuru mkuuVitu vya kawaida sana wala hakuna haja ya kuogopa maana havina madhara
shauli yako!Acha zako wewe
Uchawi huoshauli yako!
Ninaomba kwa ninaemuamini.Ujue hayo maombi unamuomba Mungu wa Israel, omba kwa kutumia mizimu yako ya jadi.
acha imani za hovyoUchawi huo
Acha wavianze vita ntapambanaNa lazima wamjadili kwenye kikao cha kata kwamba kwanini amemuona mwenzao ikiwa yeye sio Mmoja wao..? ...kama kweli kamuona.. lazima kazi anayoπππππ
Njoo sumbawanga uibeCha kufanya hapo ni kutokuwa na wasiwasi wowote ule kwa sababu hayo mambo, kiuhalisia hayapo.
Watu huwa wanadanganywa na kudanganyana tu na kuishia kuogopa mambo yasiyo na uhalisia wowote ule.
Halafu hao wanga naona huwa wanajua kusoma saikolojia za watu.
Kwa nini waje kwako ilhali mtu kama mimi ambaye nawatukana kila kuku ha na kuwakebehi, wakati mwingine hadi naenda huko kwenye makao makuu yao, hawanijaribu?
Kuna ofa yao humu na nje ya humu pia, kwamba atayeweza kunithibitishia uchawi upo kwa kuniroga, kuna dau nono hapa lililokaa tu kwa takriban miaka 16/17 sasa, likimsubiri huyo mtu wa kuniroga afanye vitu vyake.
Well, 2025 imebaki wiki moja tu iwadie na mimi bado nipo nadunda tu utadhani I own the land.
Wacha uoga wa kijinga [kwa maana halisi ya neno ujinga]. Huyo fala akirudi tena mtandike mangumi mpaka aelewe kwamba wewe hutishwi kijinga namna hiyo.
Haina shida kabisa hiyo na ni dalili kwamba nguvu zako kiroho zilikuwa kubwa kuliko zake.. Na kama angekuwa juu ya ungo angepiga bonge la mwelekaHerini ya sikukuu ya Noeli, kwangu naona ilishakuwa mbaya kwa mfululizo wa yanayoendelea na hili lililonifanya niandike hapa muda huu.