Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Hawezi kunirudia kwa sababu nimemuona ila sijamtambua ni nani.
 
Hayo ndiyo madhara ya kuwekeza kwenye ushirikina haya ona sasa
 
Kwanini unaona mtu anafanya ujinga hapo nje halafu unapiga magoti kusali, hofu imekutawala.

Kwanini usitoke nje umfukuze au kama unamuweza umpige?
Huku Mara tunabonda hao wapuuzi.
 
Bado navuta kumbukumbu ni ndoto gani nilikuwa naota ikanikurupua usingizini hadi nikashuhudia hilo.
Soma hiyo article, You will know what is behind.
 
Hahaha, mkuu uchawi upo ngoja nikuthibitishie hapa

Malaki 3:5
[5]Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
 
Chief uchaw upo mimi nmeushuhudia zaidi ya mara moja na najikutaga tu nshasali kwa imani yangu
Unakua unatamani hata ureact unashindwa unabaki kupiga fat-ha tu
Sema hapa umeushuhudia kwa namna gani?

Binafsi, sijawahi kushuhudia kinachoitwa “uchawi” toka nimezaliwa. Nyingi story tu ambazo ukichunguza unagundua hazina ushahidi wowote ule zaidi ya nilisikia au niliona hiki.
 
Sema hapa umeushuhudia kwa namna gani?

Binafsi, sijawahi kushuhudia kinachoitwa “uchawi” toka nimezaliwa. Nyingi story tu ambazo ukichunguza unagundua hazina ushahidi wowote ule zaidi ya nilisikia au niliona hiki.
Una hiyari hio lakini mimi nmeona kwa macho yangu ya nyama vitendo vya kichawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…