Hamjambo Wote!
Leo nimepokea kwa Masikitiko makubwa Taarifa ya Msiba wa Aunt Dory, Moja ya Wamama ambao walikuwa wananikubali Sana enzi za uhai wake.
Taarifa hiyo nilipoipata moja kwa moja ikanirudisha Mwaka 2015 nilipokuwa Udsm Mwaka wa Pili.
Nikiwa na hekaheka, za ujana kukimbizana na kila raha na starehe za chuoni, huku nikiendelea na kazi ya kuandika mtandaoni. Napokea ujumbe kwenye messenger yangu, " Habari Taikon, Ninapenda sana unavyoandika. Napenda vijana kama wewe mnaojitoa kwa jamii. Naweza kuchangia sadaka yangu kama shukrani"
Ile sms nilichelewa kuiona. Ilitumwa mchana mimi nikaiona Usiku. Chapuchapu nikaingia kwenye Profile Yake. Hakukuwa na picha nyingi zaidi ya picha tatu tuu.
Picha ya kwanza ilikuwa ni picha ya Ua aina ya Waridi lenye rangi nyeusi.
Picha ya pili ilikuwa ya Magufuli, kwani ndio kilikuwa kipindi Magufuli kuchukua nchi.
Picha ya tatu mbaya huu pia ilikuwa kwenye DP yake ilikuwa ya nyumba yenye bustani nzuri ya maua.
Nilipomaliza kukagua nikaona hakuna mambo mengi. Nikamjibu kwakumshukuru, lakini nikamwambia shukurani yake kwangu ni zaidi ya Sadaka.sikuomba Hela.
Usiku wa saa tano nipo kwenye Discussion pale Mabibo Hosteli nikaona amejibu. Akisisitiza kuwa anataka kuchangia.
Basi sikuwa na sababu ya kumzuia. Nikamuwekea Namba. Akashukuru kisha tukaagana.
Zikapita kama Wiki mbili hivi, nilishasahau habari za Aunt Dory, nipo zangu Yombo 5(Udsm) nakula pindi, ujumbe wa muamala unaingia kwenye simu yangu. Kiasi cha laki tatu na thelathini kimeingizwa kwenye akaunti yangu ya voda na pesa ya kutolea hapohapo.
Mmmh! Nilishtuka sikuwa na miadi yoyote ya kupata. Nikajua kuna mtu kakosea kutuma. Sikumkumbuka Aunt Dory.
Jioni kabisa naingia Messenger nakuta Meseji ya Yule aunt, mwenyewe ananiomba radhi kwa ni kiasi kidogo. Nilishangaa sana ukitegemea kwangu kwa wakati huo ilikuwa pesa nyingi. Tena upewe na mtu usiyemjua kwa kile alichokiita ati yeye ni Fancy wangu.
Mgogoro, nirudishe pesa ya watu au niipige. Hapo ikabidi nishirikishe wadau. Vijana wenzangu wakawa wanashoboka niwape namba, wengine ati hiyo ndio zali lenyewe. Wachache wakinionya niwe mwangalifu.
Zile pesa nikazila. Hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kupokea pesa nyingi kutoka kwa mwanamke asiye ndugu yangu.
Baadaye tuliwasiliana, alikuwa akiongea kwa upole na utulivu wa hali ya juu. Sauti nyepesi kama binti na iliyopoa,kama mtu asiye na haraka.
Ikafikia hatua haiwezi kupita siku bila kuwasiliana.
Alijitoa sana Dory.
Wakati wote huo tunawasiliana naye simjui kwa sura wala kwa umbo. Na sikuwa na haraka na jambo hilo. Nilikuwa na sababu maalum. Hivyo sikumwomba picha kama ilivyo desturi yetu sisi wanaume na kama nilivyokuwa nafanya kwa wasichana wengine.
Siku moja anaongea na mimi akaniambia mimi kijana wa kipekee sana. Nikamwambia afafanue, akasema hajawahi kuona kijana kama mimi kwa umri wake. Nikamuuliza kwani unamiaka mingapi, akacheka kisha akasita alafu akajibu, ninamiaka 45. Duuuh! Kipindi hicho mimi nipo 21. Duuh! Zaidi ya miaka 24. Sio pouwa!
Akasema kwa vijana wenye umri wangu wanakuwa na hekaheka sana. Nikamwambia hata mimi ninazo sana. Akacheka, akasema ataona.
Ilikuwa kawaida sana, kupokea elfu 50 kama vocha, yaani umekaa zako tuu kimbwetani unashangaa titi.. meseji, umepokea elfu 50 kisha anatuma meseji hiyo ya vocha Toto!
Haaah! Nishakuwa Toto tena, hapo nasema kimoyomoyo.
Ni ngumu kupita Wiki bila Kupokea muamala. Na hiyo ikanifanya nianze kuzizoea pesa za kupewa.
Pesa za kupewa ni ngumu kufanyia maendeleo.
Pesa za kuhongwa zikanifanya nipende wanawake wenye hadhi ya juu na wenye maisha mazuri.
Yaani kuwa na mwanamke njaanjaa kwa kweli kwangu hiyo ni kipengele.
Na vile unavyojipozisheni ndivyo unavyokuwa na ndio wale unaowahitaji wanakujia.
Chuoni ni miongoni mwa vijana nilioishi to the fullest. Kwanza sikukaa Hostel, pili sikuwahi kuishiwa pesa, tatu maeneo yote ya starehe ya jiji la Dsm, na Zanzibar, Nairobi na Kwa South Afrika nilienda Durban.
Sababu kubwa ni kwamba mimi sitoi pesa kwa mwanamke asiye na pesa. Hiyo ni yangu nikiwa Sekondari huko. Niliamini Ku- date na Maskini ni njia mojawapo ya kuuvuta Umaskini.
Imeingia 2016 Magufuli anahekaheka zake, chuoni Kulikuwa na maandamano ya wanafunzi kucheleweshewa Mikopo. Hakuna kipindi nimepiga pesa nikiwa chuo kama kipindi Kile.
Nilikuwa nakopesha Wanachuo, wanaacha vitu rehani kama Laptop. Wakirudisha wanarudisha zaidi kama riba.
Ni wakati huohuo nilikuwa nimeshahitimu ufundi Cherehani huku nasoma, so muda mwingi nikiwa kitaa nakuwa napiga mzigo.
Siku moja nikaenda kununua shamba eneo fulani huko Morogoro, Aunt Dory akanipigia simu nikamwambia sipo Mjini, nimetoka kwenda kununua shamba. Akawa anashangaa ati ananiona kijana mwenye malengo. Nikawa najua ananichota tuu akili.
Akaniuliza shamba linaukubwa gani na nataka la nini. Nikamueleza shamba ni heka tano, na ni kwaajilo ya ufugaji wa kuku na mbuzi.
Akanipongeza.
Nikarudi DSM, sasa tumekaa miezi mitatu bila mimi kumjua naye ananijua kupitia picha za mtandaoni. Akaniambia tupange siku tuonane.
Hapo hofu ikaniingia.
Kwanza, nilijaribu kuchora picha ya mwanamke wa miaka 45 alafu nakutana naye kama nani.
Mazingira aliyonitajia ndio kabisa nilihisi kuona Haya na aibu. Nilihisi dunia nzima ingekuwa pale kunishuhudia.
Kwamba Mimi ni Mario, kwamba mimi ni kiserengeti Boy, kwamba nini.
Kwa kweli hiyo kwangu ingekuwa fedheha.
Hiyo mada sikuipenda na alianza kuhisi hivyo mara kwa mara alipokuwa akiileta nilikuwa nikiipotezea.
Akaniuliza, mimi napendelea tuonane wapi. Akaniuliza tena au naona aibu kubwa na mwanamke mwenye umri Mkubwa.
Kwa kweli sikumficha nilimwambia ndio. Nahofu sana, ujasiri wangu mdogo. Akaniambia nisijali nitazoea.
Kiukweli mimi niliapa sitoweza kulala na mwanamke mkubwa zaidi yangu katika maisha yangu. Tena mwanamke mwenye umri uliotosha kabisa kunizaa.
Siku zikapita ikawa kama miezi minne hivi yaani februari 2016. Aunt Dory akaniambia niende Kwake Mbezi nikachukue gari ndogo kwa ajili ya usafiri wa hapa mjini. Nikamwambia sina pesa ya mafuta, akaniambia ataweka.
Nikamwambia isijekuwa ni mtego tuonane akacheka. Akasema niache ushamba. Nikamwambia kwa kweli katika hayo mimi ni mshamba na muoga.
Ilipofika mwezi wa tatu kwenda wa nne kwenye pasaka. Nilimualika aje ofisini kwangu, ilikuwa Sinza. Tayari alikuwa anajua mimi fundi cherehani. Hakujua mimi ni mwanafunzi wa chuo kwani nilimdanganya vilivyo.
Alipofika, ilikuwa Sinza Madukani, kwa mara ya kwanza namwona aunt Dory. Alikuwa mwanamke wa makamo, mweupe, aliyepiga low cut, na kupaka bleach fulani ya kuzugia, mwenye uso wenye utulivu na macho yenye upendo uliopuuzwa kama sio kuonewa.
Alikuwa anashepu fulani ambalo lilifanya nguo aliyokuwa amevaa kumkaa vizuri. Alikuja na gari aina ya Toyota Fortuner ya kijivu, usoni akiwa kavaa miwani. Vidole vyake vya mkono hasa wa kushoto vikiwa na pete mbili zenye rangi ya gold.
Aunt Dory aliponiona alinitambua, Mimi nilimtambua baada ya kuniita nimfuate kwenye buti la gari kwani kuna mizigo ya nguo nilitakiwa nimsaidie kushusha. Sauti yake ilikuwa ileile ya kwenye simu.
Baada ya kutoa ile mizigo ambayo alinijulisha ni mapazia anataka niyatengeneze kwaajili ya Apartment zake zilizoko Kigamboni na Mbweni. Yalikuwa mapazia mengi yaliyokuwa kwenye mabanda.
Nikawaita vijana wawili waliokuwa wafanyakazi wangu kama mafundi nguo, wakanisaidia kuingiza mapazia hayo.
Nikamkaribisha Aunt Dory ndani ya ofisi akawa anazungusha macho huku na huku kuikagua ofisi yangu.
Baada ya kuketi akanipongeza. Muda huo nimepoa kama nipo na Mkaguzi.
Nilimuuliza anataka chakula na kinywaji gani ili nikamchukulie, akaagiza maji tuu. Kisha baada ya kumleta maji tukaanza kupiga stori. Alikuwa na furaha muda wote alikuwa anatabasamu, tofauti na mimi nilikuwa nahofu iliyo changanyika na aibu.
Bei ya mapazia niliokotemo pesa ya kutosha kwani ni yale mapazia makubwa. Kama Laki sita Kasoro. Hata hivyo yalikuwa mengi pia.
Sasa Aunt dory anakuja kujua kuwa mimi ni mwanafunzi wa chuo baada ya binti mmoja tuliyekuwa tunasoma chuo kimoja ila yeye alikuwa anasomea Music, akaja pale huku akisimulia mambo ya chuo na moja kwa moja mazungumzo yake yalimjulisha Aunt Dory ninasoma.
Aliniuliza kwa nini nilimdanganya, nikamjibu sikuona umuhimu wa hilo yeye kulijua.
Hatimaye akaondoka akiwa amenipa laki nne huku laki mbili akisema atamalizia.
Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kumwona Aunt Dory
Baada ya kuzoeana huku mimi nikimkwepa sana kuepusha kumpakua kwani niliapa sitokuja kumpakua mwanamke mzee(mkubwa kunizidi).
Siku moja akaniita kwake Mbezi Beach, hapo nikakuta Watoto wawili, wote mabinti, mmoja alikuwa ameingia kidato cha Sita Bwiru Girl, huyo ndiye mkubwa, mdogo alikuwa yupo kidato cha pili, Canosa.
Akanitambulisha kama Kaka🤓 ati mimi ni kakaao wale mabinti. Vibinti vyenyewe sio haba. Vilikuwa vizuri na vyakishua. Nguo zao hazikufuata maadili yetu ya kijadi.
Hivyo vile vibinti vikanitambua kama Bro. Ingawaje Aunt Dory alimchimba Mkwala Bianca ambaye ni binti yake mkubwa kuwa aniheshimu na asijeleta tabia zisizo eleweka.
Kukatisha Stori,
Baadaye Aunt Dory alinipa Shamba la Heka 20 lililoko Maeneo ya Kiwangwa, Mkoa wa Pwani. Huo ni kutokana na kuona ati nimemheshimu na kutomvunjia heshima yake licha ya kuonyesha tamaa ya ngono. Na pia amejifunza kitu kikubwa ambacho kwa madai yake kilimnadilisha.
RIP Aunt Dory.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam